Mwalimu aibuka mshindi shindano la pombe

May 24, 2012
54
10
Nimetafakari sana na kujikuta nakosa majibu ya moja kwa moja, pale nilipoona katika taarifa ya habari ya ITV saa 2 usiku huu; mwalimu mmoja ameibuka mshindi katika shindano la wanywaji wa bia ya SERENGETI. Waandaaji wamempongeza na kuwataka watu kuendelea kunywa zaidi...

Nilichojiuliza mimi ni: 1.Hivi kwa mwalimu kuibuka mshindi wa unywaji wa pombe ni UMAARUFU?
2.Je! tukihusianisha na kiwango cha ufaulu wa watoto wetu tunagundua nini?
 
We kweli kilaza,kwani kuibuka yeye mshindi ina maana ndo mnywaji bora Tanzania?
We wa shule za kata bila shaka.
 
Eheeeee, kweli tunakaribia kuitwa nchi ya vilaza. Waziri tu hajuwi Tanzania ni muungano wa nchi zipo na kesho tutasikia huyu mwalimu kawa waziri wa elimu. CCM hii, kudadadeki na laana ziwafikie viongozi wake.
 
Mwalimu haruhusiwa kupiga roho brashi.......?......kwa hiyo akiwa na kiu anyamaze kisa mwalimu......? Hongera sana mwalimu kwa kushinda tunu.......kula chui chui mwalimu vile roho inataka.......nchi isha.......rwa hii.......
 
kama Serikali imemtelekeza kwa nini asijiunge na pombe inayojali mchango wake, na hatimae kupokea tuzo.?
 
Nimetafakari sana na kujikuta nakosa majibu ya moja kwa moja, pale nilipoona katika taarifa ya habari ya ITV saa 2 usiku huu; mwalimu mmoja ameibuka mshindi katika shindano la wanywaji wa bia ya SERENGETI. Waandaaji wamempongeza na kuwataka watu kuendelea kunywa zaidi...

Nilichojiuliza mimi ni: 1.Hivi kwa mwalimu kuibuka mshindi wa unywaji wa pombe ni UMAARUFU?
2.Je! tukihusianisha na kiwango cha ufaulu wa watoto wetu tunagundua nini?

Nampongeza sana huyo anayejitahidi kunywa walau bia..
Wengi wao wanakunywa pombe za kienyeji tu like misapuro, udang'a. choya, chang'aa n.k

Sasa wewe unamshangaa huyu wa bia ambaye ni afadhali?
 
Mbona mibunge yako ya ccm inavuta hadi bangi hujiulizi? Akina juma nkamia wanaingia wamelewa bungeni hujiulizi?
 
...Tatizo? Ameonyesha Kipaji chake cha Ziada zaidi ya Ufundishaji!:becky::becky:
 
jamani mnamshangaa huyu akiyejitokeza hadharani? hao wasiojitokeza je mnawajua walivyo?
 
Kumbe mwalimu ni kama imamu au mchungaji!!
kata kilauri mwalimu 'usahau' shida zako.
 
Maana ya hilo shindano ni kuwa kuna zawadi zinatolewa kwa wanywaji na zinakuwa kwenye vizibo vya bia hizo, kubahatika sio kwamba we ndo unakunywa kuliko wengine, anayekunywa zaidi anaweza asishinde vile vile na anaweza kuokota kizibo na ukatuma namba ukashinda. Kila mtu anaweza kushinda kama amebahatika, mwalimu nae ana haki ya kushinda pia. :A S thumbs_down:
 
Nampongeza sana huyo anayejitahidi kunywa walau bia..
Wengi wao wanakunywa pombe za kienyeji tu like misapuro, udang'a. choya, chang'aa n.k

Sasa wewe unamshangaa huyu wa bia ambaye ni afadhali?
Haya ni matusi yasiyovumilika kwa walimu yani mshaara wa laki 3.5 [take home], ela ya tution, kamradi ka ubuyu.halfcake,karanga, kuku, mifugo au duka inaweza kumfanya mwalimu ashindwe kupata bia jamani ,
naomba ufute kauli kwa walimu kwani umewadhalilisha.
 
Kwa tafsiri yako unaona kama nimewadhalilisha lakini huo ndio ukweli...

Wa kufuta kauli ni mtoa mada
Sio mimi mchangiaji...
 
Back
Top Bottom