Mwakyembe usiwe mbuni, mchawi bandarini ni uliowaamini, WATOE

TRA ndiyo janga la taifa, TPA wanatakiwa waimarishe tu ulinzi kwenye mizigo ya wateja, wale madereva wanaoshusha magari bandarini na wale askari wanaofanya lindo kwnye mayard, janga baba ni tra tra tra, yani ni ya kufumuliwa yoteeeee, nimechoka kusikia swala la system ziko down, wakati wewe unaandikiwa storage kila siku. mimi ningekuwa mwakyembe ningeifumua tra yote yote inayohusika na utohaji wa mizigo bandarini.
 
Ni kweli tarehe imekosewa, maudhui ya barua je yako sahihi? Tujadili hoja zilizoko kwenye barua.

Kukosewa kwa tarehe kumeua maudhui yote yaliomo ndani ya barua Mkuu.. Maana yake inaonyesha barua haijatoka hapo tunapotaka kuaminishwa itoke.. Hata kama kuna madai ya kweli kama hayo..
 
Kukosewa kwa tarehe kumeua maudhui yote yaliomo ndani ya barua Mkuu.. Maana yake inaonyesha barua haijatoka hapo tunapotaka kuaminishwa itoke.. Hata kama kuna madai ya kweli kama hayo..

ndio uzuri WA jambo kuwa public... Wahusika wanafahamika ma waliopokea barua wapo kama wanataka malumbano wataendeleZA ILA hapa ni mteja na mwenye Mali, kupanga ni kuchagua
 
Uzuri ni kwamba tuna mawakili na wanataka kesi ifutwe kwa technical grounds kwamba tarehe imekosewA na sio kumshauri waziri achukue hatua badala ya kumuaminisha mambo ni safi
 
Napenda kusema vitu vitatu muhimu:1)Mwakyembe angeangalia watu wa kuwaweka kwenye Board of Directors kama wana experience ya port operations & technical details at the grass root level ya port management.Waliopita walitoka TAFFA,TASAA,TSC ila wasasa wanatoka eGov,Banks,Civil Society etc.What's the objective here?.2)Madeni Kipande hafai kwani hana good communication skills,techical skills za port & business receptivity which are critical when dealing with international HUGE companies.3)Achague haraka DG pamoja na other directors & managers kwani kwa sasa wanafanya kazi without uzalendo na kutojua fate yao baada ya report ya kamati.
 
Naona mnataka Mwakyembe ahamishie ofisi yake pale bandari na afanye kazi za hao aliowateua,na basi tumfanye CEO wa bandari
 
Bandari inahisisha wizara nyingi kama Fedha (Customs), Ujenzi (Barabara..kuna Road blocks 40+), wizara nyingine pia mipakani ile eg Tunduma TRA...iko Wizara ya Nishati na Madini Ewura (Tanks za mafuta) ilisababisha uhaba wa mafuta... Vifaa vya jeshi na Navy (Wizara ya Ulinzi), pia mfano JKT waliagiza power tiller zikachelewa kutoka kutokana na ucheleweshwaji wa mawasiliano kati ya jeshi na wizara nyingine.. wakati mwingine mbolea inahitajika haraka kutokana na msimu (Kilimo inahusika), ikifika meli unahitaji co-ordination... Waziri anakuwa spokesman wa mawaziri wengine so anahitaji kuwa makini kwa kuhusisha wenzake... TRA wamefanya mordernazation ambayo hakuna anaejua.

Tatizo la wizi pia ni lazima kuwapo na uangalifu. Mfano mama aliyeenda kulalamika aliagiza vitenge akasema ameibiwa vyenye thamani ya USD 150,000 na hajawahi hata mara moja hajawahi ku-declare mzigo wa USD 20,000 kwanini isihofiwe kwamba amejiibia mwenyewe? Kwanini asifuate taratibu? Kwanini Waziri alikurupuka? Hatuoni kwamba kuna haja ya kuangalia chanzo cha tatizo! Kuna mfumo unaangalia kama kuna fraud! Kama vile Kuwasiliana na suplier, port of loading etc
 
Wenzetu wanaaangalia stock market eg backlays uk walimsimamisha ceo wake, wengine walihamisha pesa zao, so kuna -ve na +ve wateja wanaweza kuathiriwa ma maamuzi ma kauli.

kisiasa, kenya sasa mizigo imepungua kutokana na uchaguzi, tumejipanga vipi? Instead ya kujichafua na kupoteza wateja

Baadhi ya nchi zinafuatilia. Sisi tunajichafua
 
Napenda kusema vitu vitatu muhimu:1)Mwakyembe angeangalia watu wa kuwaweka kwenye Board of Directors kama wana experience ya port operations & technical details at the grass root level ya port management.Waliopita walitoka TAFFA,TASAA,TSC ila wasasa wanatoka eGov,Banks,Civil Society etc.What's the objective here?.2)Madeni Kipande hafai kwani hana good communication skills,techical skills za port & business receptivity which are critical when dealing with international HUGE companies.3)Achague haraka DG pamoja na other directors & managers kwani kwa sasa wanafanya kazi without uzalendo na kutojua fate yao baada ya report ya kamati.

watu wanaona anaonewa wivu
 
Wenzetu wanaaangalia stock market eg backlays uk walimsimamisha ceo wake, wengine walihamisha pesa zao, so kuna -ve na +ve wateja wanaweza kuathiriwa ma maamuzi ma kauli.

kisiasa, kenya sasa mizigo imepungua kutokana na uchaguzi, tumejipanga vipi? Instead ya kujichafua na kupoteza wateja

Baadhi ya nchi zinafuatilia. Sisi tunajichafua

Kenya ingekua sisi ndio tuna uchaguzi, ungeona wanavyochangamkia tenda, ss malumbano
 
Kila taasisi ilitakiwa kuwa na Wajumbe at least wawili na mwenyekiti wa kamati alikuwa Katibu mkuu wa wizara ya Uchukuzi na wakati hayupo ni Mkurugenzi mkuu wa bandari. Kamati hii ilifanya kazi kubwa na msongamano ule ukapata jawabu na matatizo kupungua kwa kiasi kikubwa. Baada ya lile tatizo kubwa kupungua kamati iliona ni vema tukabadilisha jina badala ya kuwa port congestion committee tukaona iitwe PORT IMPROVEMENT COMMITTEE ili badala ya kushughulikia swala la congestion ya meli na mizigo peke yake iwe inaangalia maswala ya ufanisi katika bandari kwa kina na kitaalam zaidi.

Ila unaonekana wewe ni mwathirika wa Uamuzi wa Waziri Mwakyembe.







Barua ya Kaimu Meneja wa Bandari ni ya 15 November 2012. Sipati connection na hii Barua ya 21/10/2012 ya Executive Secretary -TASAA (E.Mallamia) .


Ila kwa ujumla.
Barua ya Mwanzo ya Kaimu Meneja wa Bandari MR.J.I.Msaki sijui ilikuwa ya malengo gani, maana hata kama alikuwa ameombwa kutolea maelezo maendeleo /Ufanisi wa Bandari bila kujalia iandikwe kwa Kingereza au Kiswahili bado ilikuwa ina mangufu ya Kiufundi /haina nyama ya kutosha kuweza kushawishi wadau/watumiaji wa Bandari kama Barua ya TASAA ilivyojieleza.
 
Mkuu punguza jazba.. Kukosea tarehe kwenye barua ya muhimu kama hiyo imeondoa uhalali wa madai yalioletwa hapa Mkuu..

Nani mwenye jazba? aliyekosea barua ni mtoa mada (kiranja) ama walioandika.? je, hakuna hoja hapo ya kujadiliwa? nadhani wenye jazba ni wale wanaokwepa hoja eti barua imekosewa tarehe! jamani tuache mapenzi katika masuala ya kitaifa.... siamini mkuu na wengine hamuoni hoja bali munapofushwa na mambo ambayo munayajua.... najitoa kujadili hoja hii, nikiamini ujumbe umefika na wahusika wataufanyia kazi kama wana nia njema na nchi hii. Naamini katika maelezo ya makala husika, kuna mambo ya msingi na kama kuna mapungufu ni ya kibinadamu ambayo wahusika watayachuja na kuchukua yale mema. Kwa wale wanaochangia kujifanya wanamtetea Mwakyembe, nao dhamira yao kama ni njema, Mungu awasaidie wapate mwanga na kuelewa wasiyoyaelewa na wafumbuke walipofumbwa na watambue walichoaminishwa ili wakichanganya na yale mema yao, sote tujenge Tanzania yetu na JF yetu yenye uhuru wa kujieleza na kupingana bila kupigana. Mungu Ibariki Tanzania.
 
Kwa hali inavyoonekana Mwakyembe ndiye mwenyekiti wa Bodi ya Tpa kwa kuwa bodi hii itafanya yale anayoyataka na si vinginevyo. Kuna mambo yamejificha ndani ya pazia hili .
 
Mwakyembe asitafute umaarufu wa kuleta ufanisi bandarini kwa kukimbizana na vitu vidogo kama mafuta machafu (sludges ), pesa kulipiwa bank badala ya cash office as if ana ushahidi wa fedha kuibiwa nk. Atumie reports za both internal and external auditors na pia reports za kamati ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma , kamati ya bunge ya miindo mbinu nk ili zimsaidie kwenye maamuzi vinginevyo atakwama tena mapema .Awe mahiri wa kujiuliza kwa nini TRL Ilala good shed terminal kwa nini haifanyi kazi , Cargo Freight Station ya Tpa iliyokodishiwa TICTS kule Ubungo karibu na UFI kwa nini inafanya kazi chini ya malengo yake yaliyokusudiwa ya kupunguza msongamano wa malori kuingia bandarini. Kwa nini Dry Ports za ISAKA kule Shinyanga na Malawi cargo centre kule Mbeya haifanyi kazi zilizokusudiwa.Tpa walikuwa wanununue hata Locomotives za service kwenye hizi dry ports . Mizigo yote ya Rwanda, Burundi na Uganda ingechukuliwa Isaka na ile ya Zambia ,Malawi na Congo kwa sehemu kubwa ingechukuliwa Mbeya Dry Port. Waziri alidai apatiwe concept paper na Bodi na Management anayotaka kuifukuza walikaa Tanga kwa siku tatu na waziri akapewa concept hiyo .
 
Hahahaha mwaka wenu huu,nampongeza sana Dr mwakyembe kwa hatua madhubuti aliyochukua
ya kuwafukuza wezi waliokithiri hapo bandarini,naona kila siku mnakuja kulalamika humu jf
na bado,moto unawachomaaa.Nina imani mambo yatanyooka very soon!!
wewe na wezi wenzako to hell...........!

Mimi kinacho nisikitisha ni kitendo cha kutaka kutumia JF kwa lengo la kutaka kumchafua Dr.Mwakyembe, reading between the lines inaonekana kinacho endelea hapa ni kutaka kumkwamisha Ndugu Mwakyembe; mbona tulikuwa hatujawahi kuona uzalendo kama huo wa kuanika kila kitu adhalani huko siku za nyuma! Mnataka kutwambia TPA was a bed of roses kabla ya Mwakyembe kutembeza panga lake, tujaribu kuwahoji wafanya biashara wa DRC, UGANDA, RWANDA, BURUNDI, ZAMBIA na wa hapa nchini watueleze kama kabla ya Dr.Mwakyembe kuwa waziri mambo yalikuwa yanakwenda kwa ufanisi mkubwa pale BANDARINI - come Mwakyembe everything went BOOOOM!

Tusitafute mbinu za kuwavuruga wafanyakazi wabunifu na wazalendo bila ya kujali kama ni mfanyakazi wa kawaida au Waziri - Watanzania tuachane na mambo ya majungu, tukiendekeza tabia hizi maendeleo ya taifa letu yatabaki ni ndoto za mchana. Watanzania tunapoteza manhours nyingi katika mambo ya malumbano, majungu, hila, just to mention a few.
 
Kwa hali inavyoonekana Mwakyembe ndiye mwenyekiti wa Bodi ya Tpa kwa kuwa bodi hii itafanya yale anayoyataka na si vinginevyo. Kuna mambo yamejificha ndani ya pazia hili .

Mimi sioni tatizo katika hilo, na wala siamini kama Dr. Mwakyembe hajuhi vizuri anacho fanya - kama Chairman na Board yake ingekuwa makini katika utendaji wake TPA hisingekuwa inalalamikiwa kutoka kwa majirani wetu wanao tumia Bandarini hiyo, bandarini haiwezi kuendeshwa kama mali ya UKOO alafu Waziri akakaa kimya, wakati mwingine watu walio pewa dhamana ujisahau sana na kujiona bila wao Bandari itasimama - hiyo si kweli kuna watanzanai lukuki wenye uwezo wa kuendeleza bandari bila mizengwe.
 
Sekta ina wataalamu na ndio maana inawekwa kitaalamu, huko hakuna propaganda bali ni facts za kitaalamu. Kama mtu anakupa facts jibu ni moja halina majibu mengi, sio siasa na propaganda na kwa vigezo vya kitaalamu... Kama ww ni mhandisi jibu hoja, kama ni mhasibu... Huko kuna wahandisi wa meli, wachumi wa mambo ya meli na kuna wataalamu wamekaa chini wakatoa hoja na wanategemea majibu yenye mashiko sio majibu mepesi yasiyo na hoja
 
Back
Top Bottom