Hata kabla Mwakyembe hajapindua uongozi hapo TPA, bado bandari haikuwa inafanya vizuri, wizi ni kweli ulikuwapo, rushwa na urasimu wa utoaji mizigo uliokisiri, na majirani zetu wanatuzidi kwa ubora.
Hatua ya Mwakyembe ya kutifuatifua pale TPA ni ya kupongezwa. Inamaana watu wameisha kabisa ili arudishe wezi wa zamani? Hudhani kuwa inaweza iwe ni hujuma ya wale waliotimuliwa kuonyesha kuwa wao wanaweza na waziri amekurupuka kuwatimua?
Kama hawa walioteuliwa hawakidhi, ni kumshauri Waziri aweke wengine wapya wa mpito lakini sio wale aliowatimua......!
Kibanga Msese
Nenda zako! Mlivyokula vinawatosha ww ni mmoja ya walioondolewa km vp mwandikie barua humu haitakusaidia.
As usually tukishampenda mtu basi hata mapungufu yake hatujali.
Nina imani michango itakayofuata itakuwa ni ya kumtetea Mwakyembe kana kwamba yeye hafanyi makosa.
Mengi yatasemwa lakini mimi kama mteja mojawapo ambaye ametumia bandari ya Dar kwa miaka kadhaa namuunga mkono Dr. Mwakyembe kwa kiasi fulani. Nilitegemea awe mkali zaidi. Nimeagiza mizigo yangu kupitia badnari ya Dar mara zote kitu lazima kinyofolewa. JK mwenyewe aliwahi kuwatishia tu kuwa ana majina ya wezi wa pale bandarini lakini hakurudi tena. Kitu cha ajabu kabisa kwa mkuu wa nchi kufanya hivyo.
Hata kabla Mwakyembe hajawatimua hao wezi wateja wengi tayari walikwishaikimbia bandari ya DSM. DRC na Zambia hata baadhi ya Watanzania wanaona afadhali kuingiza magari kupitia Durban kuliko DSM. Kuingiza magari kupitia Durban siyo bei chini hata kidogo kwani inabidi ukodi gari la kuibeba hiyo gari ndani ya Afrika Kusini mpaka mpakani. Lakini ukilinganisha na adha za wizi hapo bandari ya DSM wengi wanasema afadhali wagharamie lakini wapate kitu chao kikiwa katika hali nzuri.
Nadhani Mwakyembe anatakiwa aende mbali zaidi. Ni vizuri kama akifanya yale yaliyofanywa TRA, wote waombe kazi upya na siyo lazima waajiliwe tena. Usalama wa taifa wakifanya kazi vizuri watajua kabisa ni nani anaihujumu bandari kwa wizi, n.k. Hao waondolewe wote bila huruma. Tutakosa wateja leo lakini watarudi kwa wingi zaidi bandari itakapokuwa imesafishwa.
Tatizo la Watanzania wengi wana akili na wanafikri kama samaki by Karume Jr,Bandari itakuwa effecient kama tu TRL na TAZARA zitafanya kazi vizuri na pia TRA kuwa free corruption institution.TRA ni janga la Taifa system walizoweka sijui wanazihujumu au makusudi kupata rushwa mambo ni balaa kabisa. Kwa kiasi kikubwa TPA ilikuwa imeimarika sana na wadau wote wanakiri.Tatizo ni kupata release kutoka TRA ambapo inachukua muda mrefu na mara tu release inapotolewa TPA hawana hiana.DR Mwakyembe kiasi anakurupuka na hana strategic mission na Idara na taasisizilizo chini yake.Mengi yatasemwa lakini mimi kama mteja mojawapo ambaye ametumia bandari ya Dar kwa miaka kadhaa namuunga mkono Dr. Mwakyembe kwa kiasi fulani. Nilitegemea awe mkali zaidi. Nimeagiza mizigo yangu kupitia badnari ya Dar mara zote kitu lazima kinyofolewa. JK mwenyewe aliwahi kuwatishia tu kuwa ana majina ya wezi wa pale bandarini lakini hakurudi tena. Kitu cha ajabu kabisa kwa mkuu wa nchi kufanya hivyo.
Hata kabla Mwakyembe hajawatimua hao wezi wateja wengi tayari walikwishaikimbia bandari ya DSM. DRC na Zambia hata baadhi ya Watanzania wanaona afadhali kuingiza magari kupitia Durban kuliko DSM. Kuingiza magari kupitia Durban siyo bei chini hata kidogo kwani inabidi ukodi gari la kuibeba hiyo gari ndani ya Afrika Kusini mpaka mpakani. Lakini ukilinganisha na adha za wizi hapo bandari ya DSM wengi wanasema afadhali wagharamie lakini wapate kitu chao kikiwa katika hali nzuri.
Nadhani Mwakyembe anatakiwa aende mbali zaidi. Ni vizuri kama akifanya yale yaliyofanywa TRA, wote waombe kazi upya na siyo lazima waajiliwe tena. Usalama wa taifa wakifanya kazi vizuri watajua kabisa ni nani anaihujumu bandari kwa wizi, n.k. Hao waondolewe wote bila huruma. Tutakosa wateja leo lakini watarudi kwa wingi zaidi bandari itakapokuwa imesafishwa.
Kiranja, kuvishtakia vyombo vya umma dhidi ya wanaohujumu uongozi uliopo, na hatua stahiki kuchukuliwa dhidi ya wanao hujumu ni vitu viwili tofauti. Kwani vyombo vya dola havifahamu kuwa mkataba wa TICTS ni wakifisadi, hatua gani zimechukuliwa?
Ni kumtia moyo Mwakyembe ili akaze buti wala siyo kumvunja moyo, kama viatu alivyojaribu vinapwaya......tumshauri taratibu bila jazba, wala makandokando ya kufutwa kazi.....kuwa; badilisha hawa viongozi tena na weka wengine. Kama umeweza kuandika waraka mrefu hivi....unaweza kumshauri na majina unaodhani wanafaa.....humu humu.....!
Kibanga Msese
Mwacheni Mwakymbe afanye kazi.....mpeni muda ili muweze kumsahihisha.....! Bandari imekimbiwa tangu siku nyingi hata kabla ya uongozi huu unaokaimu, wafanya biashara wanatolea mizigo mombasa kwajili ya urasimu uliokisiri. Kila ICD inatoza bei yake katika handling jumlisha port charges.
Hizo ICD zinashirikiana na TRA ili mradi mzigo uwe na storage kubwa. Mara mtando upo down, cost zake anapewa mteja....TBS wameweka makalio yao ofisini kwao uwapelekee documnts, badala yakuwa na ofisi kwenye ICDs na Bandrini badala ya kuja ubungo. TOOOOOOOOO MUCH documentation.
Kibanga Msese
sina hakika hata kama hata kama umesoma kwa umakini.... maswali mazito majibu mepesi.... umetumwa, umenunuliwa, fisadi, wivy wa kike.... hiii ndio Tanzania yetu na CCM yenu
Mkuu Kiranja umesema wanao hujumu wachukuliwe hatua kwa kuwashitaki kwenye vyombo vya usalama....nikakwambia TICTS ni moja ya wahujumu uchumi wa nchi na bandari kwa ujumla......vyombo vya dola vinajua hilo pia....sasa, ni hatua gani zimechukiliwa dhidi ya hiyo TICTS?
Kama vyombo vya dola havijafanya kitu dhidi ya TICTs, na kwa upande wake Mwakyembe ameamua kuchukua hatua stahiki dhidi ya wezi...kwa kuanzia.....sasa lawama ya nini dhidi yake badala ya kumuunga mkono..... ikiwa hata wewe mwenyewe huji jina la mtu unayetaka achukue nafasi ya anayekaimu.....lol
Kibanga Msese
Kiranja, sijasema asikosolewe na wala sina nia ya kukufunga mdomo, ila nilidhani tuangalie zaidi nia yake (Mwakyembe), kwani underperfomnce ya hao aliowaweka sio kusudio la Waziri. Ndiyo maana nimeshauri kuwa, tumshauri waziri, tumfungulie aone kinachoendelea bandarini ili afanye mabadiliko kwa kuwaweka wengine (kama inafaa) lakini siyo kwa kuwarudisha waliofukuza kama ulivyoshauri.....watu hawajaisha bado, na tunahitaji kusonga mbele.
Kibanga Msese