Nimejaribu kufuatilia mtiririko mzima wa mada hii nikaona nina wajibu pia wa kuchangia machache. Kwanza naona kama wadau wa bandari ni wengi zaidi kuliko Bodi ya bandari, wafanyakazi wa bandari, wizara husika, TASAA, TAFFA...NK! Nitafafanua; Waziri kudeal na management au bodi ya wakurugenzi tu na kuacha wadau wengine pembeni hakuwezi kuondoa tatizo pale bandarini espcially TPA.
Meli kuchelewa kupakuliwa au kupakiwa hakuwezi kutatuliwa kwa kuondoa watendaji wa sehemu moja huku wadau wengine wakiwa kimya. Wizi kutokea ama kwa mizigo kuibwa au kodi kukwepwa hakutaisha kwa kusimamisha watu wa upande mmoja. Nafafanua....
1. Nani anajua kwamba mzigo uliobebwa kwenye Kontaina X, ndani ya Meli Y ni wa aina gani hadi ufikapo bandarini uibwe? Jibu ni Mwenye mzigo na mwenye meli. Mwenye meli(wakala wa meli) anaandaa manifest ya mzigo, hivyo anajua nini amebeba na wapi anapeleka; mwenye mzigo anajua nini amenunua na kiasi cha ushuru wa serikali. Ulinzi wa bandari upo, ni kwa namana gani mzigo utoke/ uibwe bila taarifa? Hapo Bodi/ Meneja bandari inahusika vipi hadi iwajibishwe? TAFFA wako wapi, hakuna member wao amehusika? Kama ndiyo, mwenye meli alimkabidhi delivery order? Kama hapana, yuko salama? Waziri kumsimamisha kazi meneja bandari kwa tuhuma za wizi au utendaji mbovu kutarejesha mali zilizoibwa?
TASAA, ndio wanaowakilisha wenye meli. Je, wanavyochelewa kupeleka manifet TRA hadi wakati mwingine siku moja kabla meli haijaanza kupakuwa mzigo kutamsaidia TAFFA kuwahi kutoa mizigo bandarini kabla ya kupata Storage Charges? Hapa mwenye mzigo aliyecheleshewa mzigo ataishia kumlaumu nani?
TRA kuchelewa kukagua au kutoa kibali cha kutolea mzigo bandarini kwa wakati na kusababisha usumbufu kwa wateja hadi storage nani alaumiwe, bila shaka wengi watafikiri ni Bandari!
Msongamano wa magari kuingia na kutoka bandarini kunakosababisha uchelewaji mkubwa wa mzigo, lawama zinaelekezwa kwa bandari!
Katika katika ya umeme unaosababisha System ya TRA kutokuwasiliana na members wa TAFFA( ASUCUDA +++) na kupelekea ufanisi wa bandari kushuka nao uwekwe wapi?
Kwa ujumla wadau wa bandari ni wengi, na pia mashririkiano miongoni mwao ni muhimu sana, ni kama kupeana vijiti hivyo mmoja akikosekana the whole system in shake ila mmoja ndiye atakaye nyooshewa kidole ambaye kwa sasa kwa mujibu wa Mwakembe ni TPA! WATCH OUT BRO!