Fitinamwiko
JF-Expert Member
- Aug 13, 2012
- 4,803
- 1,419
Mkuu ukisafiri pamoja na elimu uliyojaaliwa, utagundua jinsi unavyo think out of that box. I am one of themWatanzania kwa kuwa na negative trains of thought hamjambo.
Kwa hiyo kwa sababu hizo hapo juu usafiri wa treni wala usifikiriwe?
People love to live in their own boxes of thoughts!
KLM wanaposema ndege itaruka saa 11:45 basi tegemea saa11:40 ndege itaanza kutembea tayari kuelekea njia ya kurukia. Haya ndio matarajio ya kizazi hiki. Kama kuna hitilafu, tutatangaziwa ndani ya muda wa kutosha kuwa ile ndege iliyokuwa iruke saa 11:45 sasa itaruka saa 12:45...hakuna longolongo.
Mwakyembe ulisema treni zako zitaanza 'kuruka' Oktoba. Sasa kwa akili ya haraka, kama hujataja tarehe sisi tunachukulia Oktoba mosi. Leo unasema, "Nipeni muda wa miezi sita ili muweze kuona sekta ya reli itakavyokua imekamilika nchini.... "Unataka kutuzuga kuwa sio Dar bali nchi nzima hivyo tuendelee kusubiri kwa matumaini. Hii lugha haipishani na ile ya kiranja wako Pinda ambaye kila siku anakariri, tumejipanga........
Tena unaongeza bila aibu, Tuacheni tufanye kazi na nyie endeleeni kutunga ngojera kuhusiana na usafiri wa reli lakini sisi tunajua tunachokifanya kwani niliposema usafiri wa reli unaanza mwezi Oktoba sikumaanisha utaanza Oktoba Mosi kwani hata Oktoba 15 ipo ndani ya mwezi huo huo. Ndio lazima tuchonge ngonjera kwa sababu umekuwa mwongo!!! Kama hukumaanisha Oktoba mosi, sema sasa Oktoba ngapi na uache kujingata ulimi kwani heshima yako inaanza kushuka kwa kasi.
Tumeona reli za Dar zilivyotengenezwa, wametoa 2 weeks more kwa kumalizia minor issues & SUMATRA kutoa kibali...
Ila kila kitu kipo sawa any time kabla ya muda huo train itaanza kazi ya kusafirisha abiria Dar....
mie nakushangaeni siku zote mlikuwa hamjajua kama huyu ni HOT AIR?
Mimi namjua sana toka enzi zake za pale mnazi mmoja alipokuwa na na ofisi jengo la ushirika na mwenzie aliyeamua kurudi kufundisha UD bwana MVUNGI
Sasa wakati sisi tunaletewa upuuzi wa treni isyo na kichwa wala miguu tazama kule Nairobi na commuter trains zao zilivyo safi na kueleweka
[youtube]http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=FbwS8mWJT6U[/youtube]
Syokimau Railway Revolution - YouTube
[youtube]FbwS8mWJT6U[/youtube]
Halafu mnaanzisha thread kuuliza eti wakewnya wamewazidi nini
Wakenya wanatuzidi vingi kaka. 1, kiswahili kimeanzia kwao sisi tunakidandia tuu. 2, mlima Kilimanjaro wanautangaza ni wao mpaka nilimsikia mzungu mmoja akisema kuwa alidhani Tanzania ni moja ya mikoa ya Kenya sie tumkaa KIMYA ila bibi wa Malawi kufanya UTAFITI tu wa mafuta TUNAMTANGAZIA VITA. 3, barabara ya kuuunganisha Musoma na Arusha "nadhani" kupitia mbuga ya Serengeti haitajengwa kwa sababu Kenya hawaitaki. 4, katiba mpya wanayo, na kadhalika.
Mkuu wangu kwa mawazo haya hauna tofauti na wale wanaopewa pilau,tshirts,na pombe za kienyeji wakaipigia kura CCM! Pili nikujulishe kama wakati wa uongozi wa Mwalimu ulikua bado mdogo ama hujafika mjini,aliondoka madarakani mipango hii ya kuwa train kwa usafirishaji wa mizigo na abiria imeisha andaliwa! Ni watawala wavivu na dhaifu toka chama chako cha CCM waliofuata waliharibu kila kitu! Mfano kulikua na njia ya reli ya kutoka mjini kwenda Wazo,wenzako wameiua na kugawiana viwanja. Matokeo milori mikubwa inayobeba sementi inatuharibia barabara na kusababisha ajali kila siku!
KLM wanaposema ndege itaruka saa 11:45 basi tegemea saa11:40 ndege itaanza kutembea tayari kuelekea njia ya kurukia. Haya ndio matarajio ya kizazi hiki. Kama kuna hitilafu, tutatangaziwa ndani ya muda wa kutosha kuwa ile ndege iliyokuwa iruke saa 11:45 sasa itaruka saa 12:45...hakuna longolongo.
Mwakyembe ulisema treni zako zitaanza 'kuruka' Oktoba. Sasa kwa akili ya haraka, kama hujataja tarehe sisi tunachukulia Oktoba mosi. Leo unasema, "Nipeni muda wa miezi sita ili muweze kuona sekta ya reli itakavyokua imekamilika nchini.... "Unataka kutuzuga kuwa sio Dar bali nchi nzima hivyo tuendelee kusubiri kwa matumaini. Hii lugha haipishani na ile ya kiranja wako Pinda ambaye kila siku anakariri, tumejipanga........
Tena unaongeza bila aibu, Tuacheni tufanye kazi na nyie endeleeni kutunga ngojera kuhusiana na usafiri wa reli lakini sisi tunajua tunachokifanya kwani niliposema usafiri wa reli unaanza mwezi Oktoba sikumaanisha utaanza Oktoba Mosi kwani hata Oktoba 15 ipo ndani ya mwezi huo huo. Ndio lazima tuchonge ngonjera kwa sababu umekuwa mwongo!!! Kama hukumaanisha Oktoba mosi, sema sasa Oktoba ngapi na uache kujingata ulimi kwani heshima yako inaanza kushuka kwa kasi.
Mwakyembe yuko ok anaweza hakuna haja ya kumdhihaki na kumkatisha tamaa tumuunge mkono, kwani ushujaa aliouonesha tangu achukue nafasi hiyo ni mkubwa sana ebu angalia alivyowasambaratisha wale waharibifu wakubwa waliokuwa wakijifanya ni miungu wa bandari akina Mgawe,Julius Mfuko na Ahmad Koshuma.
Mungu mbariki Mwakyembe katika shughuli zake za kila siku
Basi kama hivyo kiungwana anatakiwa atoe update! ameahidi mengi watu wanasubiri kule Air tanzania alisema nako analeta ndege mpaka leo bado, banadarini nako alisema kitu sijui kafikia wapi atupe update kidogo!Ni kweli aliahidi October na bado hajafanikiwa kutimiza alichoahidi, lakini angalau tumeona jitihada alizoweka na nia ya dhati aliyonayo. Inawezekana anakwamishwa au amekwama lakini hata jitihada kidogo alizofanya ni sawa na bure? Mawaziri wangapi wamekaa pale kwenye wizara husika hata wazo wahakuwa nalo? Mnyonge mnyongeni lakini ujira wake mpatieni.