Mwakyembe,peleka muswada bungeni kufuta mfumo wa vyama vingi vya siasa!!

Kwa kweli huu uzi umegusa penyewe "HAKUNA MAENDELEO BILA UPINZANI"Tuangalie mf Marekani wanakinzana kwenye uchaguzi ukishapita kila chama na raia ana haki ya kutoa maoni yake
Hakika
 
Vyama vya upinza vipo kimkakati ili kulidhisha wafadhiri ccm wakifanya hivo dunia itawaandama wanasema wataishi ivoivo kwa manyanyaso na mwishowe ni vurugu nchi nzima
 
Hivi ule uzee wa ghafla alioupata Mwakyembe akasema anamuachia Mungu ulisababishwa na nini?
 
Naunga mkonyo hoja ohh!!!. mfupa hauna ulimi jamani.
 
Ninavyoona vyama hivi vifutwe tu!Mtu kama prof angalia anavyofanya michezo ya darasa la tatu ilihali anajina kuubwa!Angalia jinsi wabunge wa ccm wanavyotamba na mizaha bungeni huku wabunge makini wakizuiwa hata kuongea tu angalau basi nje ya bunge!Ona naibu spika anavyojibebea sifa kwa kuwafanyia ubabe wapinzani wakati huo huo yeye na wenzake wakizima kabisa ndoto za kuangalia bunge live badala yake linaoneshwa usiku kama muvi za utata zisizofaa kuangaliwa na watu wote.Waachieni ccm nchi wapigane,warogane wao kwa wao.Sisi tuchape kazi atakayeleta dhuluma,anapelekwa mahakamani,akipendelewa huko pia,unamalizana naye hapa hapa duniani

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Historia iko wazi na haijawahi kukanushwa,Ccm waliukataa mfumo wa vyama Vingi na waliukubali kwa shinikizo la baba wa taifa...Mwalimu nyerere....ila nafsini mwao hawakuwa tayari!

Na hii imeendelea kujidhihiri kila rais anayekaa madarakani.
Kimsingi, hata nyerere aliwahi kulalamika kwamba kila kitu alichokipangilia na kukitolea hoja nchi hii,baada ya nyerere kutoka madarakani,Ccm walikitupa,sembuse vyama vingi!!
Baada ya uchaguzi vyama hufanya Kazi ya kujijenga kwa wananchi na kuwasiliana na wanachama na kutengeneza wanachama wapya.

Sasa vyama vya siasa vimezuiwa kutafuta wanachama wapya wala kutembelea waliopo na hata kufafanua kwa wananchi kupitia mikutano ya hadhara madhumuni ya kuanzishwa kwake.
Sasa vinataka kugeuzwa vyama vya kutafuta kura na si wanachama na wafuasi....kimsingi wanacham na wafuasi hutafutwa kabla ya uchaguzi kupitia mikutano ya hadhara na huwa nguzo ya chama wakati wa kampeni kwa kusimamia maslahi yake

Kwa kuwa vyama hivi vimekuwa kero kwao japo sheria ya kuvianzisha ilitungwa na bunge lililokuwa na wabunge 100% Ccm,basi namshauri mwakyembe waziri wa sheria kwamba,apeleke muswada(kama ana ubavu)akavifute kwa kuwa bunge hili asilimia mia wanaokaa ni Ccm baada ya ukawa kuwaachia ukumbi
sababu nyiengine ya kuvifuta ni hasara tunayo ingia kama taifa kupitia ruzuku za kila mwezi. Selekali ya ccm itoe majibu pia, unawalipaje wanasiasa ruzuku kila mwezi wakati umewazuia kufanya kazi zao?, huu kama siyo ubadhirifu ni nini?, haya nayo ni malipo hewa kama ya watumishi hewa!. Natoa wito ruku za kila mwezi kwa vyama vya siasa vilivyo zuiliwa kufanya siasa zikome.
 
Naunga mkono hoja.
Zirudi zile zama za zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM.
 
Back
Top Bottom