iparamasa
JF-Expert Member
- Nov 14, 2013
- 13,437
- 14,924
Historia iko wazi na haijawahi kukanushwa,Ccm waliukataa mfumo wa vyama Vingi na waliukubali kwa shinikizo la baba wa taifa...Mwalimu nyerere....ila nafsini mwao hawakuwa tayari!
Na hii imeendelea kujidhihiri kila rais anayekaa madarakani.
Kimsingi, hata nyerere aliwahi kulalamika kwamba kila kitu alichokipangilia na kukitolea hoja nchi hii,baada ya nyerere kutoka madarakani,Ccm walikitupa,sembuse vyama vingi!!
Baada ya uchaguzi vyama hufanya Kazi ya kujijenga kwa wananchi na kuwasiliana na wanachama na kutengeneza wanachama wapya.
Sasa vyama vya siasa vimezuiwa kutafuta wanachama wapya wala kutembelea waliopo na hata kufafanua kwa wananchi kupitia mikutano ya hadhara madhumuni ya kuanzishwa kwake.
Sasa vinataka kugeuzwa vyama vya kutafuta kura na si wanachama na wafuasi....kimsingi wanacham na wafuasi hutafutwa kabla ya uchaguzi kupitia mikutano ya hadhara na huwa nguzo ya chama wakati wa kampeni kwa kusimamia maslahi yake
Kwa kuwa vyama hivi vimekuwa kero kwao japo sheria ya kuvianzisha ilitungwa na bunge lililokuwa na wabunge 100% Ccm,basi namshauri mwakyembe waziri wa sheria kwamba,apeleke muswada(kama ana ubavu)akavifute kwa kuwa bunge hili asilimia mia wanaokaa ni Ccm baada ya ukawa kuwaachia ukumbi