Mwakyembe mgonjwa; afya yake yadorora; ngozi yavimba mwili mzima

BobT

Member
Oct 7, 2011
12
21


Ndugu wana JF hizi ni taarifa za uhakika kabisa, Dr. Mwakyembe Kapewa sumu amevimba mwili mzima hali ni mbaya nilipopata habari hizi walikuwa wanafanya mpango kumkimbiza India. Nitarudi nikipata habari kwa undani

Nawakilisha

Gazeti la Mwananchi

Mwakyembe mgonjwa


  • AVIMBA MWILI MZIMA, JK AMTEMBELEA
Na Mwandishi wetu

AFYA ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe, ni tete baada ya kuugua ugonjwa uliomsababisha kuvimba mwili wote.Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na yeye mwenyewe zinaeleza kuwa, alianza kuwashwa ngozi miezi mitatu iliyopita kabla ya hali kubadilika siku za karibuni na hatimaye kuvimba sehemu kubwa ya mwili wake.

Mwakyembe alilieleza gazeti hili jana kuwa, baada ya hali yake kubadilika alianza kupata matibabu katika hospitali mbalimbali jijini Dar es Salaam akiwa nyumbani kwake Kunduchi Beach.Akizungumza na gazeti hili kwa shida, Dk Mwakyembe alisema hajui chanzo cha ugonjwa huo wa ngozi, daktari wake ndiye anaweza kuelezea kwa usahihi.

"Ni kweli naumwa nipo nyumbani, hata sura yangu imebadilika. Sasa hivi namsubiri daktari wangu, nilisikia natakiwa kupelekwa India kwa matibabu, nasubiri kauli yake si mimi niamue," alisema na kuongeza;

"Siwezi kusema nimelishwa sumu, ninachosema mimi nimevimba kweli mwili mzima naumwa kweli hapa nimelala na sijui umenipataje kwa simu kwa sababu huwa siiwashi muda huu una bahati kweli".

Mke wa Dk Mwakyembe Mkewe Linah Mwakyembe alipozungumza kwa njia ya simu na Mwananchi Jumapili, alisema kwa mujibu wa daktari wake, Dk mumewe anasumbuliwa na ugonjwa wa ngozi unaojulikana kitaalamu kama Exfoliative Dermatitis.

"Alianza kuugua muda mrefu kidogo, kama miezi mitatu iliyopita, hali hiyo ilikuwa inatokea na kupotea hadi sasa ambapo hali imekuwa mbaya zaidi," alisema.

Alisema madaktari waliomfanyia uchunguzi kwa nyakati tofauti katika kipindi hicho walitoa majibu tofauti na kuongeza kuwa wapo waliosema hali hiyo ilisababishwa na kisukari na mwingine ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema kulikuwa na chembechembe za sumu katika damu yake.

"Baada ya ngozi yake kubadilika sana na hali kuwa mbaya, tulienda hospitali na madaktari walitupa majibu tofauti, wapo waliosema ni kisukari na kuna mwingine alisema kuna chembechembe za sumu," alisema Linah na kufafanua kuwa daktari aliyedai hivyo hakuwapa maelezo zaidi.

Kwa mujibu wa Linah, ngozi ya Dk Mwakyembe inawasha na inakuwa kama inatoa mba mwili mzima hadi kichwani.

Aliongeza kuwa daktari wake ameshauri ufanyike uchunguzi wa kina zaidi ili kujua kama atahitajika kupatiwa matibabu nje ya nchi.

"Walipendekeza afanyiwe uchunguzi zaidi, hivyo kama kutakuwa na ulazima wa kupatiwa matibabu zaidi nje ya nchi basi watatueleza," alisema Linah.

Alisema kuwa leo ndio watapata jibu kama atahitajika kwenda nje au kuendelea na matibabu hapa nchini.

Alisema kumekuwa na uvumi mwingi juu ya ugonjwa wa Dk Mwakyembe na kusisitiza kuwa wao kama familia wanasikiliza kinachosemwa na madaktari na kile watakachoshauri.

"Sisi tunaendelea kusubiri kile kitakachogundulika baada ya uchunguzi huo na kama kutakuwa na mengine tutajulishwa na kujua hatua itakayofuata," alisema Linah.

Exfoliative Dermatitis Kwa mujibu wa maelezo ya kitabibu, ugonjwa huu huweza kusababisha madhara makubwa ya mwili na matatizo mengine hivyo kuhitaji uangalizi wa karibu wa kitabibu.

Ugonjwa huu ukikomaa husababisha ngozi ‘kuwaka moto' na huathiri wanawake na wanaume lakini zaidi wanaume wenye umri kuanzia miaka 55.

Dalili Dalili za ugonjwa huu ni kuwashwa, mwili kuishiwa nguvu pia sehemu ya juu ya ngozi hupukutika.

Chanzo kwa mujibu wa maelezo ya kitabibu, sababu za ugonjwa huo bado hajizulikani, hata hivyo matukio ya ugonjwa huu mara nyingi yanahusishwa na magonjwa mbalimbali ya ngozi, madhara ya dawa kama penicillin, sulfonamides, isoniazid na phenytion.

Rais Kikwete amtembelea Baadaye mchana Rais Jakaya Kikwete alifika nyumbani kwa Dk Mwakyembe Kunduchi Beach kumjulia hali.

Mwakyembe ambaye ni Mbunge wa Kyela mwaka 2008, aliongoza Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza kashfa ya Mkataba wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Richmond.

Katika baraza jipya la mawaziri ambalo Rais Kikwete aliliunda mwaka jana, alimteua Dk Mwakyembe kuwa Naibu waziri wa Ujenzi akimsaidia Dk John Magufuli.

Mikasa ya Mwakyembe

Mei 21 mwaka 2009 Dk Mwakyembe alinusurika kufa katika ajali mbaya ya gari eneo la Ihemi kilomita 40 kutoka Iringa mjini akiwa safari kutokea Mbeya kwenda Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa za Polisi, gari alilokuwa akisafiria Toyota Landcruiser T362ACH, liliacha njia saa moja asubuhi baada ya kukanyaga shimo na tairi ya upande wa kulia kuchomoka na dereva wake, Joseph Msuya (30), kupoteza mwelekeo kabla ya gari hilo kutoka nje ya barabara upande wa kushoto na kuparamia mti kisha kupinduka.

Ajali hiyo ilitokea wakati dereva wa Dk Mwakyembe akijaribu kulipita lori kabla ya kukanyaga shimo hilo.

Dk Mwakyembe na abiria wengine waliokolewa na Wasamaria wema pamoja na trafiki wawili waliokuwa kwenye basi dogo wakisafiri kutoka Iringa kwenda Njombe.

Baada ya ajali hiyo alilazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa. Ilifahamika kuwa aliumia taya kisha alihamishiwa Dar es Salaam kwa matibabu.

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) aliunda tume iliyoongozwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wakati huo, Kamanda James Kombe, kuchunguza chanzo cha ajali hiyo. Matokeo yalionesha kwamba ilisababishwa na uzembe wa dereva wake, Msuya.
NIMETOKA SASA HIVI KWA MWAKYEMBE AFYA YAKE KWELI IMEDORORA SANA LAKINI CHANZO BADO KUJULIKANA 100%

Ahsante kwa taarifa ambazo zimenifanya leo asubuhi niende nyumbani kwa Mwakyembe, (Mtongani, Kunduchi Beach, Dar es Salaam). Kwa kweli afya ya Mwakyembe ni mbaya sana. Kwa wengi waliomwona katika miezi mitatu iliyopita, afya yake ilionekana kuwa na mgogoro. It was just a question of time.

Kwa kuwa kuna conflicting medical diagnosis ya matatizo ya Mwakyembe, Wizara yake imeona akachunguzwe sehemu nyingine. Wapo madaktari wanadhani chanzo ni "food poisoning", wengine wanadai ni "exfoliative dematitis" (naomba msiniulize), wengine wanadai ni kisukarti na wengine wanasema ni "fungi infection". Ikiwa hata akina Kubenea wanapelekwa nje kwa uchunguzi na matibabu na wanaendelea kuwananga waliowapeleka, sembuse Mwakyembe?

Let's be fair. Hivi nani ata-rejoyce Mwakyembe akifa? I wish him all the best. Naona hali imebadilika hapa nyumbani kwa Mwakyembe, nawaona wasaidizi wa Mkuu nwa Nchi wakivinjarivinjari kwenye nyumba yake. Naondoka nisje nikakutwa hapa!

Jajimkuu
Nimezungumza na mke wa Dr Mwakyembe bi Lina Mwakyembe asubuhi hii amesema Mwakyembe hajalishwa wala kupewa sumu isipokuwa ni kweli kuwa anaumwa amepata inflammation kwenye ngozi lakini anaendelea vizuri.
 
Last edited by a moderator:

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,882
Mkuu kapewa sumu wapi ? Yuko wapi na wanamkimbiza India muda huu kwa ndege ipi ? Ya Rais au ndege gani ? Kwa nini India hapo Muhimbili wameshindwa ?Je atafika India kama umesema hali ni mbaya ?

Dowans hao wanaitaka ile pesa .Kazi kubwa sana .
 

OMGHAKA

Member
Aug 15, 2011
97
23
Imesemwa Freemasins wao wanaamini ni lazime watawale na atakayepinga utawala wao watamuondoa na RA ni freemason, hii sasa inaelekea kuthibitisha.
 

J4MAYOKA

Senior Member
Jul 16, 2011
147
84
Ndugu wana JF hizi ni taarifa za uhakika kabisa, Dr. Mwakyembe Kapewa sumu amevimba mwili mzima hali ni mbaya nilipopata habari hizi walikuwa wanafanya mpango kumkimbiza India. Nitarudi nikipata habari kwa undani

Nawakilisha


Kwa nini apelekwe India wakati hospitali ya maana ya MUHIMBILI ipo?

huu ndio ufisadi wenyewe...muhimbili wa avifaa na madaktari

ikishindikana si wampeleke hapo Nairobi hospital

why India?
 

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,181
7,292
Kwa kuzingatia muda ilipotumwa hii mada, na kuwa mtumaji ndo post yake ya kwanza (may be kwa ID aliyotumia), Inanilazimu nisiipuuze hata kadogo taarifa hii. Namtakia Dr afya njema popote alipo na naombea hili la sumu lisiwe la ukweli...
 

J4MAYOKA

Senior Member
Jul 16, 2011
147
84
Sasa mbeya kunaniiiii mwandosa ajarudi leo mwakyembe.DOOOO Rwanda yanukiaaaaa


Rwanda kwa sababu ya mtu mmmoja?

hebu tupumzishe sie

Mbona Kigoma Malima naye alilishwa sumu na hamkusema kuwa Rwanda itatokea?

Bila kusahau IMRAN KOMBE mlimuua na maisha yameendelea kama kawaida
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

16 Reactions
Reply
Top Bottom