Mwakyembe: Mahakimu walioshinda kesi za rushwa wasirudishwe kazini, wananchi hawana imani nao

chakii;
Can I ask Why? Ulitakaje?? Warudishwe kwenye ofisi walimonyea kweli?? Sasa si watakula kwa ujanja zaidi?? Kwetu wana kausemi kuwa; Mbuzi akiisha lamba magadi, haachi kamwe.
Hao jamaa weshakula kitu ya watu, hawataacha kamwe. Kuna siku watalamba tena na this time itakuwa si haba.
Mahakama zipo kwa ajili gani mkuu? kwa mawazo yako basi hatuna haja ya kusikiliza maamuzi ya mahakama
 
View attachment 440547

Waziri wa katiba na sheria, Dkt. Harrisson Mwakyembe ameitaka tume ya utumishi wa mahakama kutowarejesha kazini mahakimu 28 ambao wameshinda kesi za rushwa zilizokuwa zikiwakabili kwa lengo la kulinda imani ya mahakama kwa wananchi na badala yake mahakimu hao wakafanye kazi nyingine.

Waziri wa katiba na sheria, Dkt. Harrison George Mwakyembe amesema kumekuwepo na watumishi wa mahakama ambao walikuwa wakikabiliwa na tuhuma za rushwa mahakamani, ambapo kati yao watumishi 30 wamekutwa na hatia na kufukuzwa kazi huku mahakimu wengine 28 wakishinda kesi zao, lakini akasema kuwa hawastahili kurejeshwa kazini waendelee kutoa haki kwa madai kuwa tayari wananchi hawana imani nao.

Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye ameanza ziara ya kiserikali ya siku tatu katika mikoa ya Mbeya na Songwe, ametembelea ofisi ya msajili wa vizazi na vifo katika halmashauri ya jiji la Mbeya ambako ameitaka ofisi hiyo na nyingine nchini kuongeza kasi ya usajili wa vizazi kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ili kuiondolea Tanzania aibu ya kuwa miongoni mwa nchi tano za mwisho barani Afrika kwa kusajili vizazi vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.

Mratibu wa zoezi la usajili wa vizazi vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano wa halmashauri ya jiji la Mbeya, Vicent Msolla amezitaja changamoto zinazolikabili zoezi hilo, huku meya wa jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi akiahidi halmashauri yake kuongeza kasi ya usajili wa vizazi na vifo.

Chanzo: ITV

Mie nadhani kwa kuzingatia "UNYETI" wa Kazi wanazo fanya mahakimu za kutoa haki za watu,

Ni vyema Serikali ikawaangalia watu hawa kwa umuhimu wa pekee kwa kuwaboreshea maslahi yao ili wasiingizwe kwenye majaribu yoyote yale,

Vinginevyo watafukuzwa wote! Hata hivyo wapo waadilifu na pia wapo ambao sio waadilifu, hivyo ni muhimu tukawatunza hao waadilifu kwa kuwa boreshea maslahi yao.

Kimbilio la kila mtu ni mahakamani lkn bado taasisi hiyo haijaimarishwa na kupewa uzito unao stahiki, mfano ktk baadhi ya mikoa na wilaya hakuna kabisa majengo ya Mahakama au kama yapo basi ni machakavu kabisaaa.
Dhamira inatusuta!!!!!
 
Mahakama zipo kwa ajili gani mkuu? kwa mawazo yako basi hatuna haja ya kusikiliza maamuzi ya mahakama

chakii;
Sijaunga mkono hoja yake kuwafukuza kazi hao mahakimu kwani hata hivyo hana ubavu huo japo yeye ndo waziri. Hii itakuja letea nchi maafa baadaye kuwalipa fidia hao mahakimu. Ila, nisingelipenda warudishwe pale pale penye kituo chao
 
Hawa watakwenda mahakamani na watashinda kesi na kudai fidia. Hizi ni gharama za kujitakia. Haya maamuzi yanasababisha kuongezeka kwa gharama za uendeshaji wa serikali. Je ni nani atakayeweza kugharamia maamuzi kama haya??!! Obvious ni mlipa kodi ndiye atakayeumia, Waziri anatakiwa atafakari kabla ya kutekeleza.

wameambiwa wapangiwe kazi zingne, hvyo wanaweza kuwa makaran au post zingne za kiutawala. inategemea na elimu aliyonayo
 
Waziri hana mamlaka yoyote ya kumfukuza hakimu.

Cha ajabu waziri mwenyewe mwanasheria, anajua mamlaka ya tume ya utumishi ya mahakama na mamlaka ya jaji mkuu.

Mbona yeye alipata kashfa ya kuleta mabehewa feki ya treni pamoja na kununua kiwanja kule,ina maana yeye ni bora sana?

Mahakama imewakuta hawana hatia,lakini waziri mwenye phd ya sheria anasema kuna mahakama ya wananchi eti haiwaamini.

Kama wasomi viongozi wako hivi,watanzania tumekula hasara,huyu ndio atasimamia utawala wa sheria kweli?matamko mengine yanadhalilisha serikali na usomi wa mtu.

Wananchi wenyewe ni hawa wana ccm ambai hunyoosha mikono na kuchongea wenzao kwenye ziara za makonda? Wakijua wana dalili za kushindwa kesi wanaandika barua ya kutuhumu kuombwa rushwa,hakimu anafukuzwa.

Kama hakuna security of tenure, basi hakuna haki.

Hii nchi itabaki kuwa gofu milele.
Nimegundua kua watu humu uelewa ni mdogo sana....kwani hapo amesema wafukuzwe au wapangiwe kazi nyingine...mbona kitu simple sana hicho.
 
O
View attachment 440547

Waziri wa katiba na sheria, Dkt. Harrisson Mwakyembe ameitaka tume ya utumishi wa mahakama kutowarejesha kazini mahakimu 28 ambao wameshinda kesi za rushwa zilizokuwa zikiwakabili kwa lengo la kulinda imani ya mahakama kwa wananchi na badala yake mahakimu hao wakafanye kazi nyingine.

Waziri wa katiba na sheria, Dkt. Harrison George Mwakyembe amesema kumekuwepo na watumishi wa mahakama ambao walikuwa wakikabiliwa na tuhuma za rushwa mahakamani, ambapo kati yao watumishi 30 wamekutwa na hatia na kufukuzwa kazi huku mahakimu wengine 28 wakishinda kesi zao, lakini akasema kuwa hawastahili kurejeshwa kazini waendelee kutoa haki kwa madai kuwa tayari wananchi hawana imani nao.

Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye ameanza ziara ya kiserikali ya siku tatu katika mikoa ya Mbeya na Songwe, ametembelea ofisi ya msajili wa vizazi na vifo katika halmashauri ya jiji la Mbeya ambako ameitaka ofisi hiyo na nyingine nchini kuongeza kasi ya usajili wa vizazi kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ili kuiondolea Tanzania aibu ya kuwa miongoni mwa nchi tano za mwisho barani Afrika kwa kusajili vizazi vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.

Mratibu wa zoezi la usajili wa vizazi vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano wa halmashauri ya jiji la Mbeya, Vicent Msolla amezitaja changamoto zinazolikabili zoezi hilo, huku meya wa jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi akiahidi halmashauri yake kuongeza kasi ya usajili wa vizazi na vifo.

Chanzo: ITV
Ok. Lakini bado sijaelewa. kama hakimu amesingiziwa tu kesi (amebambikizwa) kwa chuki na hila akashinda asirudi kazini Mheshimiwa Waziri?. Nijuavyo mimi mahakama ni chombo pekee kinachotoa haki kwa kila mtu.
 
Anajua kuwa hao mahakimu wana hasira na utawala huu hivyo hofu yake ni kuona wakiwa upande wa wananchi badala ya serikali,kwa kweli tusali tu lkn muda sio mrefu nchi itaongozwa kidikteta.
 
Kama ni hivyo tunaomba na wale wabunge wote waliowahi kushitakiwa kwa tuhuma za rushwa na kufutiwa kesi zao, nao wasirudi tena bungeni kuendelea na kazi zao za kujadili na kupitishwa sheria za nchi.. Hali kadhalika mawaziri na viongozi wengine pia.. Kusiwe na double standard kwa hili..

Tuone kama atabaki mtu..
Na wale majaji 2 wa escrow wasisahaulike
 
Wasipewe hata ukarani Wala uhudumu. Dk. Mwakyembe pia awaondoe Mahakimu Wakazi wasiojua Kiingereza maana wanaondoa imani ya utoaji haki kwa wananchi.
 
Waziri hana mamlaka yoyote ya kumfukuza hakimu.

Cha ajabu waziri mwenyewe mwanasheria, anajua mamlaka ya tume ya utumishi ya mahakama na mamlaka ya jaji mkuu.

Mbona yeye alipata kashfa ya kuleta mabehewa feki ya treni pamoja na kununua kiwanja kule,ina maana yeye ni bora sana?

Mahakama imewakuta hawana hatia,lakini waziri mwenye phd ya sheria anasema kuna mahakama ya wananchi eti haiwaamini.

Kama wasomi viongozi wako hivi,watanzania tumekula hasara,huyu ndio atasimamia utawala wa sheria kweli?matamko mengine yanadhalilisha serikali na usomi wa mtu.

Wananchi wenyewe ni hawa wana ccm ambai hunyoosha mikono na kuchongea wenzao kwenye ziara za makonda? Wakijua wana dalili za kushindwa kesi wanaandika barua ya kutuhumu kuombwa rushwa,hakimu anafukuzwa.

Kama hakuna security of tenure, basi hakuna haki.

Hii nchi itabaki kuwa gofu milele.
Pole
 
Yaani siasa za Tanzania zinapofusha sana,mi nilipoisoma hii habar juz nikacheka tu,mahakama imemsafisha ww unasema wasirud kazini!!
 
Ni yale yale ya kuendelea nung'ang'ana akina Lema waendelee kukaa mahabusu kinyume cha sheria kwa tuhuma za kuota ndoto.. Mungu ataendelea kuwafunua true colors zenu kila siku. Sasa Waziri wa sheria na Katiba naye anasema Mahakimu walioshinda kesi za rushwa wasirudishwe kazini!
 
Hii sio sawa kama wameshinda kesi zao , mahakama imeshawasafisha, Mbona Waziri mwenyewe alituhumiwa kuingiza mabehewa yasiyokidhi viwango akajieleza, leo anaendelea na kazi.
 
Back
Top Bottom