nkanga chief
JF-Expert Member
- May 31, 2016
- 2,084
- 1,620
Waziri wa katiba na sheria, Dkt. Harrisson Mwakyembe ameitaka tume ya utumishi wa mahakama kutowarejesha kazini mahakimu 28 ambao wameshinda kesi za rushwa zilizokuwa zikiwakabili kwa lengo la kulinda imani ya mahakama kwa wananchi na badala yake mahakimu hao wakafanye kazi nyingine.
Waziri wa katiba na sheria, Dkt. Harrison George Mwakyembe amesema kumekuwepo na watumishi wa mahakama ambao walikuwa wakikabiliwa na tuhuma za rushwa mahakamani, ambapo kati yao watumishi 30 wamekutwa na hatia na kufukuzwa kazi huku mahakimu wengine 28 wakishinda kesi zao, lakini akasema kuwa hawastahili kurejeshwa kazini waendelee kutoa haki kwa madai kuwa tayari wananchi hawana imani nao.
Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye ameanza ziara ya kiserikali ya siku tatu katika mikoa ya Mbeya na Songwe, ametembelea ofisi ya msajili wa vizazi na vifo katika halmashauri ya jiji la Mbeya ambako ameitaka ofisi hiyo na nyingine nchini kuongeza kasi ya usajili wa vizazi kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ili kuiondolea Tanzania aibu ya kuwa miongoni mwa nchi tano za mwisho barani Afrika kwa kusajili vizazi vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.
Mratibu wa zoezi la usajili wa vizazi vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano wa halmashauri ya jiji la Mbeya, Vicent Msolla amezitaja changamoto zinazolikabili zoezi hilo, huku meya wa jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi akiahidi halmashauri yake kuongeza kasi ya usajili wa vizazi na vifo.
Chanzo: ITV