Mwakyembe: Hatuwezi kuruhusu TLS kujiingiza kwenye siasa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
20170308_035128.jpg
20170308_035105.jpg


Sasa sio tetesi bali ndo ukweli serikali inamwogopa Lissu katika mambo ya kisheria kuliko mtu mwingine wa upinzani.

Gazeti la serikali limetanabaisha kuwa TLS wakiruhusu Lissu kugombea kwakuwa ni mwanasiasa wa upinzani basi watakifuta, lakini kuna mgombea wao wa CCM huyo wala huwasikii wakimsema hata kidogo.

Sasa ni nini serikali inakiogopa kwa Lissu kuwa rais TLS?

Mnasema Lissu ni Mwanasiasa na kwamba akigombea ataingiza siasa ndani ya TLS, na huyu GODWIN MWAIPONGO je?

93d49fea682a0a3384464c721bc8b427.jpg
 
Sasa ntaona kama na wanasheria wetu nao ni waoga vile vile.
The fact Tundu Lissu anakataliwa na Serikali ilikuwa ni moja ya sababu kuu ya kumchagua yeye ndio aongoze TLS.
Nitakuwa nikifuatilia kwa karibu uchaguzi huu, japo namuona Lisuu akidondoshwa kwa ninavo wajua wabongo.
 
Wanasheria wala hatutishiki na hiyo mikwara ya kipuuzi. Lissu ana haki ya kugombea na ana haki ya kuchaguliwa. Na tutamchagua Lissu kwa makusudi awe rais wa TLS ili kupinga huo ukandamizaji wa seikali ya kidekta.
Serikali haiwezi kutuchagulia mtu wa kutuongoza.
Wanasheria siku zote Woga ni mwiko kwetu.
 
Wanasheria wa Tanzania hawajawahi kuwa strong hata siku moja

Sasa ntaona kama na wanasheria wetu nao ni waoga vile vile.
The fact Tundu Lissu anakataliwa na Serikali ilikuwa ni moja ya sababu kuu ya kumchagua yeye ndio aongoze TLS.
Nitakuwa nikifuatilia kwa karibu uchaguzi huu, japo namuona Lisuu akidondoshwa kwa ninavo wajua wabongo.
 
Kama CCM na serikali yake hupiga dafrao chaguzi za wanafunzi wa vyuo vikuu na kusimika vijana wao,hili la Lissu wala halishangazi ila sasa imebidi rasmi wajitokeze na mikwara mikubwa!!

Pale CWT Mkoba miaka nenda ndio raisi wa chama cha Walimu japo ameshawahi kupigwa hadi mawe na wanachama na hutosikia hata siku moja walimu wanagoma bali mikwara tu!!
 
Kama wanasheria mnakuwa waoga kutetea maslahi yenu mtakuwaje na ujasiri wa kutetea ya kwetu wateja wenu?
Komaeni ili kama wanatumia mabavu kuvunja TLS ndio itakuwa vizuri kwa jumuia ya kimataifa kujua nini kinatokea Tanzania.
Majuzi mime msikia mkulu akisema kama mtu amekamatwa na pembe halafu Wakili anakuja kumtetea weka ndani na yeye.
Kama mnafhani anatania nyie kubalini tuu kuwa na TLS dhaifu mtaona jambo hilo likitekelezwa kidogo kidogo kisha linakuwa mazoea. Na niwaambie wanasheria ukweli, nyie ni maadui wa kubwa wa Polisi kwa vile mnawadhalilisha sana katika kesi zao za kubumba lakini wanawashindwa kwa vile mnalindwa na sheria kama maafisa wa mahakama.
Sasa wanapopewa rungu hilo, bila kuwa na Rais wenu mtu shupavu asiyeogopa hata kukamatwa akiwa tetea ukweli mwafaa,kutupwa mahabusu sasa utakuwa mchezo tuu kila siku nyie na wateja wenu mtayajadili yenu huku mahabusu. Acha tuwaambie Vijana wetu kuwa sasa kazi ya uwakili waiogope maana humo tuendako itakuwa kama kuendesha Gari lililobeba wahamiaji haramu
 
Kisheria sidhani kama Waziri ana mamlaka ya kukifuta lakini ngoja tusubiri yakitokea
 
hivi huyu mwakyembe ni mwalimu wa sheria kweli?
Ni mwalimu wa sheria ndiyo lakini ukichomeka kwenye safu za uongozi CCM inabidi ukalie elimu na ufahamu wako wote kwa lazima.
Mwakyembe analazimika kujijaza upumbavu ili aendelee kuwa waziri.
 
Si itungwe sheria sasa kuwa Lissu akigombea tu TLS basi chama cha mawakili kinafutwa. Otherwise huu ni upuuzi wa mwendokasi
 
Back
Top Bottom