Mwakyembe apimwe akili nina wasiwasi sana na akili zake baada ya kutoka hospital.
bange ni kitu kibaya sana:decision:
Hata pata kitu.Hehehe sasa Mwakyembe anatafuta kura za 2015?
Huo ndio mshahara wake wa kutokusema ukweli kipindi kile bado ni mbunge 2 angesema ukweli wote katika ile ripoti kama alivyosema yy mwenyewe kwamba kuna mambo mengine ni aibu kuyasema sasa kwa sasa ni nini anataka kutuambia kwa sasa .........??leo katika mikutano miwili iliyofanyika jimboni kwake Mhe Mwakyembe amewaliza watu baada ya kuamua kuvua kofia yake na gloves na miwani waone jinsi alivyoathiliwa na sumu kali. Katika hotuba yake ametumia muda kuwasihi wananchi kuacha majungu badala yake wamuunge mkono ili amalizie kipindi chake cha uongozi. Hata hivyo hakutaja watu waliomdhuru lakini aliwashukuru wananchi kwa maombi yao na madaktari kwa juhudi zao katika kuokoa uhai wake.
amesema asijadiliwe, then anavua kofia na gloves ili watu wamuhurumie, huyu jamaa ni MNAFIKI
Mwenzake alikimbia, akasema ametukanwa sana, amedhalilishwa sana na ameonewa sana, kisa uwaziri mkuu, akasepa akabaki mbunge. Yeye anang'ang'ania nini U - naibu waziri? Kama siyo kuwa naibu waziri angelikuwa na akili zake timamu. Sasa leo nani anaamini maneno yake wakati alikuwa hospitalini? Kama alikuwa na tatizo la bone marrow, tunashindwaje kuamini kuwa ana matatizo ya akili. Hawezi kuwa VUGU VUGU, ni lazima achague either kuwa MOTO au BARIDI. Kama anabaki ccm, anakuwa BARIDI, akiwa moto watammalizia kwa sumu, kama anataka kuwa MOTO, aje ajiunge na jeshi la wapambanaji. ANAOGOPA NINI? AU ANAONA AIBU??? shauri yake.
sio 'borne marrow' ni BONE marrowHiyo borne marrow hivi inaweza kuzuru hata ubongo wakuu nijuzeni.
Kwako Mheshimiwa Mwakyembe.
Kwanza ningependa kukupa pole kwa maswahibu ya maradhi uliyopitia siku za karibuni, na pili nampa Sifa Mwenyezi Mungu kwa kukutunzia uhai wako katikati ya mtikisiko mkubwa wa afya yako.
Pili, napenda kukupa ushauri wa kuwatendea haki wana Kyera kwa kuachia nafasi yako ya Ubunge ili wachague Mbunge mwingine ambaye japo kimtazamo atakuwa ni mwenye afya na nguvu za kuweza kuwatumikia katika nafasi hiyo kwa ufanisi zaidi.
Katika hili, naendelea kukushauri kuachia nafasi ya ubunge ili kujitendea haki wewe mwenyewe vilevile, kwani utajipa fursa ya kupumzika na kuimarika kiafya zaidi achilia mbali kwamba utakuwa umejitoa kabisa kwenye maswala ya Kisiasa ambayo kutokana na Kauli zako mwenyewe na za Rafiki yako Ndugu Samwel Sitta ndiyo yaliyopelekea kujikuta katika hati hati ya kiafya na uhai ambavyo ni vitu muhimu sana kwako na familia yako kuliko fedha na madaraka.
Na zaidi utakuwa umejipa fursa adhimu ya kuwaseheme wote unaohisi walishiriki katika kukufikisha kwenye matatizo ya kiafya unayopambana nayo na hivyo kujirudishia amani katika maisha yako kwa kufungua ukurasa mpya wa maisha badala ya kujiingiza katika uovu wa kulipiza visasi mambo ambayo yanaweza kukutia matatani zaidi.
Nakuombea busara na hekima wakati ukiutafakari ujumbe huu.
Wasalaamu