MWAKYEMBE 'awagwaya' WAZEE wa BANDARI...

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Hadi leo hii,tangu kuteuliwa kwake,Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe hakuwahi kuwa na mkutano wa kiofisi na wafanyakazi wa Shirika la Bandari almaarufu kama Wazee wa Bandari.

Wachambuzi wa mambo wanadai kuwa huu ni udhaifu unajidhihirisha kwa Dr. Mwakyembe ambaye alianza vyema kwa ziara zake za kushtukiza kwenye Idara za Wizara yake.

Kubwa zaidi ni ile ya kusafiri kwa treni kutoka Dar hadi Dodoma-Bungeni.

Je, Dr.Mwakyembe hajajiandaa bado kuwakabili Wazee wa Bandari?
 
uliongozana nae kwenda dodoma kwa njia ya reli....na ukamsifia sana.....sasa tueleze kwa nini hafiki hapo bandari..muulize tu atakwambia
 
Bado muda haujafika! ziara za kushtukiza hazina muda maalumu, kwa hiyo kuwa na subira!! Vipi ile Ubungo - Posta Subway ilishaanza kufanya kazi?
 
Kati ya Wizara zenye Madudu basi mimi nadhani hii ya Mwakyembe ni miongoni mwa hizo.Kuna Bandari kule Kigoma inaendeshwa kisanii na Warundi waliojipachika Utanzania wa bandia.
Kule hakuna cha kumjali mteja kila kitu ni Rushwa na ubabaishaji usio na kifani.
Chakushangaza ni kwamba hakuna Mamlaka yeyote ya Serikali Mkoani humo inayothubutu hata kuulizia ni kwa nini hali iko vile na wakati mwingine hata unajiuliza je hata akina Kafulila,Zito, Machari na Mkosamali hawana taarifa na hali hii?.
 
Back
Top Bottom