Mwakyembe apigwa changa la macho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakyembe apigwa changa la macho

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rosemarie, Mar 29, 2012.

 1. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  WAKATI NAIBU Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, akiamini kwamba kuna tume imeundwa kuchunguza chanzo cha ugonjwa wake, imebainika kuwa hakuna tume kama hiyo, Tanzania Daima Jumatano limebaini.Hali hiyo imebainika juzi baada ya Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Isaac Natanga, kulieleza gazeti hili kwamba hakuma tume wala chombo kilichoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, kuchunguza sakata la ugonjwa wa Dk. Mwakyembe.“Napenda kukujulisha kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, hajaunda tume yoyote kuhusu Mwakyembe,” ulieleza ujumbe mfupi kwenye simu ya mkononi uliotumwa na msemaji wa wizara hiyo, Isaac Natanga.Hata hivyo kauli ya msemaji huyo inaweza kuibua mjadala mwingine kwani inatofautiana na ile iliyotolewa na Waziri Nahodha kwamba serikali imeunda tume kuchunguza suala hilo.Kauli ya Waziri Nahodha ndiyo iliyompa nguvu Dk. Mwakyembe kujipa matumaini kuwa serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inafanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha ugonjwa wake ambao kwa muda mrefu umekuwa ukihusishwa na sumu.Akizungumza na waandishi wa habari Machi 18 mwaka huu ofisini kwake siku chache baada ya kurejea kutoka India kwenye matibabu, Dk. Mwakyembe alisema hawezi kuzungumzia uvumi ulioenea nchini kuwa amelishwa sumu na badala yake anakiachia chombo chenye mamlaka ya kufanya uchunguzi huo, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Dk. Mwakyembe alisema anasubiri na ana matumaini makubwa na matokeo yatakayotolewa baada ya uchunguzi ulioagizwa na Waziri Nahodha kuhusu afya yake na uvumi huo kwa ujumla.Dk. Mwakyembe ambaye pia ni Mbunge wa Kyela (CCM), alisema kuwa angependa kuona uchunguzi huo unakamilika haraka na ripoti yake inatangazwa kwa umma na kuongeza kuwa yuko tayari kutoa ushirikiano kwa tume hiyo katika uchunguzi wao.Dk. Mwakyembe ambaye ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Mbunge wa Kyela, alipatwa na gonjwa huo mwaka jana lililosababisha kubadilika kwa ngozi yake huku nywele zote zikinyofoka.Kutokana na hali hiyo, kumekuwa na uvumi mwingi ulioenezwa kuwa amelishwa sumu na mahasimu wake kisiasa.Uvumi huo umekuwa ukikolezwa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC), Samuel Sitta, ambaye alisisitiza kuwa yuko tayari kutoa ushahidi kwenye chombo chochote cha serikali kuhusu kulishwa sumu kwa Dk. Mwakyembe.

  Serikali yamkaanga Dk. Mwakyembe
   
 2. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Sie hatusemi kitu yeye kasema tuufyate sasa basi..............wameunda hawajaunda watajuana huko sisi tulilumbana akiwa mgonjwa huko India.............amerudi katuona sis ni ma "kachonchi kapanka" yaani wazabazabina fulani hivi..........
   
 3. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #3
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Where is your take?!!!
   
 4. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  akafie mbali........
   
 5. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #5
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  kazi ipo
   
 6. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Heshimuni ombi lake la kuufunga mjadala wa afya yake!
   
 7. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,102
  Likes Received: 6,565
  Trophy Points: 280
  Tume ya nn.
   
 8. +255

  +255 JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,908
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Kwani ni lazima?
   
 9. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Aisee umenifanya nicheke sana! Hawezi kuwa na his/her take manake Mwakyembe mwenyewe alishatupiga stop.
   
 10. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #10
  Mar 29, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Tume iundwe ya nini?yeye anajua anachoumwa na ameshasema hataki kiherehere yyt azungumzie afya yake.
   
 11. uttoh2002

  uttoh2002 JF-Expert Member

  #11
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,679
  Likes Received: 2,740
  Trophy Points: 280
  Wangapi wanaumwa Tanzania? Wangapi wanakufa? Wangapi wanakufa kwa Umeme kukatika na kukosa oxygen, Wangapi wanakufa kwa kuonewa na policy Wa CCM? Ye ni nani? Mie Nimechoka kumhurumia, Hana Msimamo, ajielezi, anatuzuga, na Wasiwasi Sumu utakuwa imeathiri akili yake.
   
 12. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #12
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,865
  Likes Received: 2,806
  Trophy Points: 280
  Wa-TZ kwa unafiki bwana! Jamaa keshawapiga stop mikanjanja yetu bado inachokonoa tu! Nyamba...f zake huyo mwandishi!! Hata isipoundwa inatusaidia nini? Watajuana wenyewe huko!
   
 13. J

  Juma Hamis Member

  #13
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tatizo si wewe ila ufinyu wa mawazo yako,na fikra za mihemko,tumia akili kujadili mambo,nlizani umepevuka kumbe bado.Hivi unaweza kufikri kuwa wewe u mzima kiakili kujijumia watu kufariki.
   
 14. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #14
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama hili ni adenga nyeti sana katika mstakabali ya nchi yetu hasa ukizingatia kuwa Mh. Waziri anaendelea vizuri, zaidi Mungu ashukuriwe na kama kutakuwa na haja sana wale waliokwishajitokeza na kusema wana ushahidi itakuwa nafasi yao kulalamika mbele ya sheria kuliko kuendelea kuliibua suala hilo utafikiri nalo ni lina tija yoyote.
  Pole sana Mh. Harrison Mwakyembe
   
 15. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #15
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  mwenyewe hapendi mmzungumzie mwacheni apumnzike
   
 16. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #16
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Bora wewe, tatizo watu wengine wagumu wa kuelewa, wepesi wa kusahau. Imekuwa vigumu kuelewa mh. alikuwa na maanna gani kusema mjadala umefungwa au tumesahamu mapema sana kuwa mh. alisema mjadala umefungwa?
   
 17. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #17
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  No comment!!Tuliambiwa mjadala wa hii issue uko CLOSED
   
 18. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #18
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  aundiwe tume ya nini wakati yeye mwenyewe alisema mjadala wa ugonjwa wangu upigwe stop?sioni kama kuna haja ya kuudwa tume wakati yeye mwenyewe alishasema ugonjwa wake usijadiliwe.
   
 19. Kakulwa P

  Kakulwa P JF-Expert Member

  #19
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani huyu jamaa kasema hataki kujadiliwa, sasa tukianza TENA atasema tunaifanya familia yake isiwe na amani.
  Tuache kumjadili maana maumivu ni yake mwenyewe akifa watakaofiwa ni wanafamilia yake, akifanikiwa ni familia yake kwanza itakuwa juu.
  Sasa ya nini kuendelea naye wakati amejivua gamba, tuendeleee na mambo mengine ndugu zangu wapendwa wana JF.
   
 20. J

  Juma Hamis Member

  #20
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nahisi unachangamoto za kifra ukipona utaacha,taratibutaratibu usikate tamaa naona unaelekea kubaya aza kunywa dawa tena
   
Loading...