Mwakyembe anauza bandari

Weka source ya habari ,au wewe ni mmoja wa wale walotimliwa huko bandarini na ndo mana unaleta povu apa.

Ikiwa wewe ndo ungekua mfanyakazi wa bandarini ungeleta source gani hapo mkuu?
Infact watu tunaamini makaratasi hata kama yataandikwa na waongo wa ccm, mara ngapi miccm imepiga pesa na kuandika taarifa za uongo ambapo unaambiwa mfano mradi wa barabara umegharim bilioni kadhaa wakati ukiangalia ubora wa hiyo barabara hauendani na gharama unayoambiwa ila kwa akili kama zako utaomba source najua
 
Nilipomuona mwakyembe kuwa ni gamba,ni pale alipokana maandishi yake pale DODOMA kwenye BMK. Bora angekaa kimya.
 
Nalaumu sana wazazi kunipeleka shule, maana najitambua na kuumia sana ninapopata taarifa hizi, mbaya zaidi wenye bandari hawajielewi na hawajitambui.

Mwakyembe ni kanafiki sana kale kajamaa, anajifanya kuwa mtetezi wa wananchi kumbe anawaandaa kisaikolojia ili akipiga dili zake ba kugundulika wananchi wasio na upeo wasiamini.
Correctly nakuunga mkono kuna wakati wajinga wana Raha sana maarifa wakati mwingine mzigo unaweza kufa kabla ya siku zako sababu ya stress na hasira
 
Nikiwaambia mwakyembe mwizi mnasema wivu wa kisiasa. Huyu jamaa hafai! Michongo yote ya bandari ni hela zake za mfukoni na kaipanga safu nzuri sana ya upigaji. Toka aingie kashapiga zaidi ya bilioni 200 watu hawajui tu! Tushamchoka sie huku Bandarini

Du hizo ni zaidi ya zile za EPA jamaa kiboko hebu tupe ushahidi tumkomalie basi
 
Huyo homeboy Mwakyembe awajibishwe tu. Tungekuwa na sheria za kunyonga watu kama hawa.
 
Hivi IKULU wanakuwa hawajui kwelii dili kama hizo?
 
Nilimdharau Mwakyembe na kuanza kumfuatikia kwa karibu baada ya kukata kitabu chake alichokiandika mwenyewe. Na hasa baada ya kuona ukanaji wake huo ulikua na lengo la kulinda udikteta na maslahi ya wachache ndani ya Chama chake
 
Kikao kimoja bilion 9. Na bado unamtetea mwakyembe!

Kikao kipi hicho au na wewe umedaganywa na kichwa cha habari? isome habari kamili iliyobandikwa baadae hapo hapo post #1 kutoka habari leo, halafu unioneshe kwenye hiyo habari kama kuna sentensi hata moja inayosema "kikao kimoja".

Ngojeni kamati ya bunge ihitimishe kazi yake tuujuwe ukweli. Msikurupuke.
 
Leta ushahidi wa mabaya aliyofanya Mwakyembe. Ninavyojua mimi Harrison amesafisha uchafu uliokuwa bandarini na wewe unaweza kuwa mmojawapo. Mwakyembe ni mkombozi wa watu kama sisi ambao tulikuwa tunaumizwa na wizi wenu
 
Taratibu wanafiq wanaanza kujionyesha kwa sura yao halisi! Wakati ule wakishupalia issue ya Richmond kuna mzee aliwahi kuniambia unachokisikiliza na kukishabikia kutoka kwa Mwakyembe haina uhalisia na ukweli wowote kwani Mwakyembe ameficha Ukweli kwa kiasi kikubwa na kushindwa kuwaambia Watanzania kuwa Lowassa alikuwa Upande wa Watanzania kwenye ile Deals na kuwa Taifa kubwa lenye Nguvu nyingi Duniani ilikuwa imejipenyeza kupitia ngazi ya Juu Zaidi!!!! Munkari niliyokuwa nayo wakati ule sikumuanini asilani!!! Ila Mzee alienda mbali zaidi kwa kuniambia nifuatilie Deal la kufua Umeme kwa njia ya Upepo ambayo Mwakyembe et al walikuwa tayari wamejipenyeza kuikomba TANESCO kama kawaida yao!!! .... Mungu si Athumani sasa MAFISADI hali wanajionyesha mchana kweupee...
Kati ya watu ambao tuliwaamini katika nchi hii na waziri makini ni dr. Mwakyembe. Kumbe wapi nae fisadi tu. Kaimu mkurugenzi wa bandari bw. Kipande alimweka yeye kumbe kwa faida yake,leo Mwakyembe na wenzake wanauza bandari kwa mkataba wa hovyo.

Moja ya masharti ya mkataba mwekezaji huyo asilipe kodi 30yrs na asiingiliwe na serikali kwa jambo lolote.

Watanzania tumshukuru mkuu wa mkoa wa Mtwara mh. Simbakaria kwa kuwa mzalendo kugomea mkataba huo,bila yeye bandari ilikuwa inauzwa.

Asante RC Mtwara, Mungu akupe uhai na tuwashukuru TAKUKURU kwa kuingia kazini. Mwakyembe ni mwizi tu.
 
Ha yani badala ya serikali itoe masharti ndio mwenye kununua atoe masharti. Nina uhakika kwamba kuna makampuni mengi tu wangeweza kununua hiyo bandari na bila kotoa masharti. Tanzania inauzwa sasa
 
Hivi habari kama hiyo isiyoeleweka, wala kuwa na ushahidi inapataje nafasi humu?? Napata shida kuwa mwishowe hili litakuwa jamvi la kila mwenye hisia tofauti na mtu then ni sehemu yake (jukwaa lake). Hembu toa maelezo ya maana yenye ushahidi tuelewe unamaanisha nn!
 
Back
Top Bottom