Mwakyembe amtaka Makonda ajibu maswali 9

Mwakyembe amtaka Makonda ajibu maswali 9

Waziri wa Habari, michezo na utamaduni Dr Harrison Mwakyembe amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Daresalaam ajibu maswali tisa ambayo yalipelekea kuvamia kituo cha habari cha Clouds televisheni, Mh Mwakyembe ameyasema hayo katika viwanja vya bunge wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari wa nipashe, kwamba kitendo cha Makonda kuvamia kituo cha luninga cha Clouds kitendo hicho
Katika majibu yake, Dk. Mwakyembe alisema suala hilo ni “zito” na haliwezi kuachwa lipite bila kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua stahiki.

Huku akiendelea kuikosoa ripoti ya kamati ya Nape ambayo amekuwa akisisitiza haijakidhi matakwa ya kikatiba na kisheria kwa kushindwa kumhoji Makonda, Dk. Mwakyembe alisema Mkuu wa Mkoa huyo atahojiwa kwa mambo tisa yanayohusiana na tukio hilo.

“Hili ni suala zito maana linahusisha uvamizi ambao ni kesi ya jinai,” alisema Mwakyembe ambaye ni daktari wa sheria na Waziri wa Katiba na Sheria mpaka wiki mbili zilizopita.

“Kuna vitu tisa ambavyo upande wa pili (Makonda) utaulizwa.”

Dk. Mwakyembe hata hivyo, alikataa kuvitaja vitu hivyo tisa huku akisita pia kutaja tarehe ambayo Makonda atahojiwa.

“Upande wa kwanza (Clouds TV) tayari umeshahojiwa na ripoti tunayo. Upande wa pili nao tutauhoji na wenyewe pengine una hoja,” alisema Dk. Mwakyembe.

“Ili kukidhi matakwa ya kikatiba na kisheria, ni lazima tuuhoji upande wa pili. Hili suala kama nilivyotangulia kusema ni la jinai. Lazima mtuhumiwa apate haki ya kujitetea.
“Ukifika mahakamani, hata yule mwenye kesi ya mauaji lazima tumpatie wakili, hata kama tunao uthibitisho kwamba ameua.”

Machi 29, wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari alipokaribishwa ofisi kwake mjini Dodoma, Dk. Mwakyembe alisema hawezi kuikabidhi kwa wakubwa wake ripoti hiyo ya kamati ya Nape bila kuwapo na maelezo ya Makonda.

“Taaluma yangu ni sheria, hivyo siwezi kufanya jambo hilo la kupeleka malalamiko ya upande mmoja kwa mabosi zangu bila kusikiliza ule mwingine,” alisema Mwakyembe siku hiyo.

Alisema hatateua kamati nyingine ya kufuatilia jambo hilo, bali yeye na viongozi wenzake watakuwa kamati hiyo ili kuuhoji upande wa pili kisha kupeleka taarifa kwa wakuu wake ambao ni Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais mwenyewe.

JELA MIEZI SITA
Kamati ya watu watano iliyoundwa na Nape kuchunguza tukio la uvamizi wa televisheni ya Clouds ilibaini kuwa kiongozi huyo aliwatishia kuwafunga jela miezi sita wafanyakazi wake endapo wasingerusha kipindi alichokitaka.

Pia Kamati hiyo ilibaini Makonda aliwatisha kuwa angewaingiza wafanyakazi hao kwenye tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya kama wasingerusha kipindi chake.

Aidha, kamati ilibaini kuwa Makonda aliwatisha wafanyakazi wa kituo hicho ili wasitoe taarifa za uvamizi wake, kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa na Katibu wa Kamati hiyo, Deodatus Balile.

Wajumbe wengine wa kamati hiyo iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Dk. Hassan Abass, ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO, ni Mhariri Mkuu wa Magazeti ya The Guardian, Jesse Kwayu, Nengida Johannes wa Upendo Media na Mabel Masasi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Ilidaiwa Makonda akiwa na askari kadhaa wenye bunduki, alivamia kituo hicho na kuwalazimisha watangazaji wa kipindi cha ‘Da Wikend Show’ kurusha taarifa ya mama anayedai kuzaa na askofu Gwajima, bila ya kiongozi huyo wa kidini kupewa nafasi ya kusikilizwa.

Ingawa taarifa ni ya upande mmoja, kwa mujibu wa Balile mtuhumiwa alikubali kuwaona, lakini wakati wakipanda ngazi kwenda ghorofani iliko ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ilala jijini, Makonda aliteremka kwa kutokea mlango wa nyuma.

hakikubaliki, hivyo anapaswa kujibu maswali kadhaa katika kuhoji upande wa pili maana kitendo hicho kimelaaniwa sana na jukwaa la wanahabari Tanzania na wadau wengine wa habari ndani na nje ya nchi.

Nipashe.

Rais Magufuli kwa kumfukuza Nape kazi kwa kosa la kukemea uhalifu wa Mkuu wa Mkowa na kutetea haki za watumishi wa clouds kwa vitisho vya Mkuu wa Mkowa, ambaye alitumia polisi wanaotakiwa kutetea haki na sheria, akawatumia kuvunja sheria. Kitendo hiki watu aliyekuwa amewapa hope kuwa yeye uongozi wake na kutetea haki kwa Watanzania wote bila kuchaguwa.
 
Mwenye mashitaka mbona halalamiki??? mimi naamini kuna namna nyingi za kuhakikisha suala linafikishwa mahakamani. Siamini kwamba kuna mtu katika nchi hii yuko juu ya sheria, tatizo ni kwamba the majority of us are so paranoid tunapoona watu wenye madaraka, na tunapenda kuwaona viongozi kama miungu watu bila sabababu za msingi. Nikimkatama Mkuu wa mkoa akizini na mke wangu, niishie kulalamika tu na kumwacha kwa sababu ana cheo kikubwa serikalini???? ndivyo tunavyofanya sasa... tunabaki kuilalamikia tu serikali kama vile kuna mtu anaitwa "serikali" aliyenda kosa hilo. No, let's deal with the issue. Aliyeongoza uvamizi hapo Clouds si serikali. Ni mtu, na ni raia asiye na haki kuliko raia mwingine yeyote. Tuacheni woga wa karne ya 4, waliovamiwa wamfikishe mahakani....
Na hicho ndicho kinachotokea.
Ndiyo maana Ruge alikomaa sana kusema wanamsubiri aje aombe msamaha ili urafiki wao uendelee. Hiyo inaonyesha hawana nia ya kuweka mkazo juu ya hatua zozote za kisheria dhidi ya "mvamizi" wao. Bado "wanautamani" ukaribu waliokuwa nao na huyo mvamizi.
 
Mke anauma sana huyo Mwakyembe atamfuata Nape muda sio mrefu ila Mwakyembe ni mnafiki kama wanafiki wengine anauma na kupuliza
 
...utawajua tu, vipi kolomije wazima!?
Naamini ni wazima. Japokuwa sijui ramani ya kufika huko. Nasikia tu.
Nafikiri utawala wa kijiji hicho ungetumia umaarufu huu katika kuwavuta watalii wa ndani Maana kimetajwa sana.
Unaonaje mkuu?
Hiyo ni business opportunity.
 
Mwakyembe mbona ripoti ya Richmond haikukidhi vigezo vya kikatiba Kwa kutomwoji Lowassa lakini uliitoa?
 
Clouds na Makonda wanajuana,ndio hizo pilipili usiozokula zakuwasha nini?
Wanachogombania hatukijui,jiulize kwanini Mkuu wa Mkoa alikuwa amezoea kwenda Clouds kama kijiwe chake.Kaingilia Nape kichwa kichwa na kwa kutojua source ya mtafaruku,wakamtemesha uwaziri.
Sasa na Bw Mwakyembe naona anaerekea huko huko.
 
Naamini ni wazima. Japokuwa sijui ramani ya kufika huko. Nasikia tu.
Nafikiri utawala wa kijiji hicho ungetumia umaarufu huu katika kuwavuta watalii wa ndani Maana kimetajwa sana.
Unaonaje mkuu?


Hiyo ni business opportunity.

Wazo zuri sana mkuu
 
Nitakua wa mwisho,kumwamini mwakyembe ! Mtendaji yyte/kada yyte wa ccm,co wakuaminiwa.wanaweka jambo utadhani ndivyo litakavyofanyiwa kz,baadae wanaanza komedi.hasa mwakyembe ni mnafiki,kupitiliza !
 
Back
Top Bottom