Mwakyembe aishukia benki ya NMB | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakyembe aishukia benki ya NMB

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Jun 22, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe

  Kizito Noya, DodomaMBUNGE wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe amedai bungeni kuwa benki ya NMB imemtapeli Rais Jakaya Kikwete kwa kutoa ahadi hewa ya Sh20 milioni mbele yake kwa Chama cha Kuweka na Kukopa cha Kimbaru (Sacco) miaka mitatu iliyopita, lakini haijatimizwa hadi leo.

  Mbunge huyo, maarufu katika vita dhidi ya ufisadi, alitoa tuhuma hizo wakati akichangia hotuba ya makadirio ya matumizi ya ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

  Mwakyembe Alisema Oktoba 11 mwaka 2008, Rais Jakaya Kikwete alitembelea wilaya ya Kyela ambako alizindua jengo la maktaba na pia jengo la kisasa la Saccos hiyo.

  “Kabla ya ujio huo wa rais, Saccos hiyo ilikuwa imeanza kuprocess (mchakato wa) mkopo kutoka NMB, lakini ulikuwa bado haujaiva,” alisema Dk Mwakyembe.

  “Lakini siku ambayo rais alifika, ikaletwa check (hundi) kuubwa ya Sh20 milioni na akakabidhiwa rais. Walisema kwamba fedha hizo tayari zimepatikana, kilichobaki ni kuchukuliwa tu.

  “Rais aliuliza hii hela ni mkopo au msaada? Wakajibu ni mkopo. Akaishika hundi hiyo na kuinyanyua juu kuwaonyesha wana-Saccos hao," alisema Dk Mwakyembe.

  “Cha ajabu, tangu tarehe hiyo 11 mwezi Oktoba mwaka 2008 hadi ninavyozungumza hapa, ile hela haijapatikana na kila wakienda benki wanaambiwa masharti ambayo hayatekelezeki.”

  Dk Mwakyembe alisema: “Hii ni aibu kwa benki na taifa kumdanganya rais. Ni kumfanya rais wetu aonekane mwongo mbele ya wananchi wake.

  Kama suala ni dhamana, tayari yeye amekuwa dhamana kwa kuishika hundi hiyo hivyo hela hiyo ni bora ikatolewa kuondoa aibu hiyo kwa rais.”

  Awali kabla ya kutoa maelezo hayo ya hundi, Dk Mwakyembe aliishukuru serikali kwa kupeleka mbolea ya ruzuku wilayani humo mwaka jana akisema imeongeza kiwango cha mavuno kwa kiasi kikubwa.

  “Naomba sasa nichukua fursa hiyo kuiomba serikali iongeze kiasi cha mbolea hiyo isiwe ya kuwatosha wakulima 25,000 tu bali iongezeke ili iwafae wakulima wengi zaidi,” alisema Dk Mwakyemba.

  “Naomba mtuongezea mgawo wa mbolea ya ruzuku na msihofu mbolea kudokolewa Kyela. Mbolea haidokolewi labda aje mbunge mdebwedo kwa propaganda za mafisadi.”


  Chanzo Mwakyembe aishukia benki ya NMB


  Mwakyembe waambie ukweli Wabunge hao wenzako nakupongeza.
   
 2. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  MziziMkavu acha kutuchanganya maana avatar yako ya kuzimu while signature yako ya maneno ya Mungu aliye hai, wewe wa wapi?
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Mkuu unanifurahisha Mkuu wangu N-handsome Usijali na Avatar yangu mimi ni mtu wa mungu nampenda Mwenyeezi mungu. Hiyo Avatar nimeipenda haina maana yoyte usiniogope sasa hiyo Avatar unataka niitowe?Huipendi kwani?
   
Loading...