Mwakyembe achukua maamuzi baada ya ajali Musoma

Nimaneno mazuri kama yakifanyiwa kazi hasa hapo kuzifungia kampuni kama fundisho kwa wengine na pia mikataba ya kazi na bima ya wasafiri
Lakini siku zote mlikuwa wapi ,jitahidini sana kwani ajali mwaka zimetisha sana

watazifungia ila watazifungulia tena kama ivyotokea kipindi kile mohamed trans na morobest haikupita mda gari zikawa zipo barabarani.

na leo angalia morobest ilivofululiza ajali za kutisha.

tuombe mungu kwa kweli yatekelezwe hayo aliyoyaahidi
 
Amefurahishwa na ajali au nini sijaelewa!!!! kuja na ndege kuna uhusiano gani na ajali? Wanyakyusa utawajua tu.

Jmn kaenda kutoa pole na kuangalia usalama mnamponda.... Acngeenda c mmgemfyonza ubongo..... Afu et wanyakyusa!! Ata usemeje yule no kiongoz wako na atabak ivo ivo
 
Hilo siyo tamko ni igizo,kwani hizo basi alizozifungia si watabadilisha rangi na kuandika kampuni mpya,labda angezitaifisha ndo tungesema katoa tamko,wizi mtupu,wadanganyika bwana!
 
Kuzifungia kampuni hizi za mabasi ni uonevu tu na kujitakia sifa za bureza kisiasa.
Wenye mabasi hawa wametumia fedha nyingi kuinvest katika biashara hii na katika kutoa huduma za usafiri.
Hakuna mtu ambaye atapoteza pesa zake kununua mabasi na kazi yake kugonga na kuyaangusha.
Kuna tatizo la msingi kuhusu ajali lakini halisababishwi na compani hizi.
Matatizo yapo kwa maderva wanao kabidhiwa magari haya kutokuwa makini juu ya kukumbushwa kufata sheria na kuendesha kwa hadhari.
Wengi wa madereva hawa wanapata vyeti feki kutoka mamlaka husika , tatizo ni wanapo pewa leseni za udereva na sio wanao waajiri.
Tatizo jengine ni barabara zetu nazo zinachangia sana sana.
Hivyo bwana mwakyembe wewe ni mwana sheria huwezi kuyafungia makampuni haya kwa makosa ya madereva walopewa vyetii feki na serikali.huu ni ubabe na uonevu tu lakini haitapunguza ajali za barabarani kama trafik wenyewe kazi yao ni kukaa barabarani na vitabu kuwakamua wenye magari kwa makosa yasio husu sheria za trafic
 
Tumbavu mnaruhusu kampuni za kikuda zinatuua kila siku,alafu mkiona tumekufa mnajifanya mnaongea.
 
Haya hapa maamuzi aliyoyatoa Waziri Mwakyembe baada ya ajali ya mabasi kuua watu 39 huko Musoma

1.jpg

Jana September 5 2014 kwenye eneo la Sabasaba hapa Musoma ilitokea ajali mbaya sana ya mabasi mawili yakiwa na abiria na kulihusisha gari jingine dogo ambapo majeruhi ni zaidi ya 70 na waliofariki ni 39 Wanawake kwa Wanaume kwa mujibu wa taarifa mpya za vifo zilizotoka muda mfupi uliopita.

Kwa kuguswa na tukio hili waziri wa uchukuzi Dr. Harryson Mwakyembe ilibidi aahirishe ratiba zake nyingine na kulazimika kuja Musoma kuwatembelea majeruhi leo asubuhi kwenye hospitali ya mkoa pamoja na kwenda kwenye eneo la ajali kutazama.

Baada ya hapo Waziri Mwakyembe metoa maamuzi yanayolenga kukomesha uzembe unaosababisha ajali hizo ‘Inabidi niwape pole Watanzania wote ambao wamepoteza ndugu jamaa na marafiki, taarifa za ajali nimezipata nikiwa Dodoma kwenye bunge maalum ikawa sasa nitafikaje haraka Musoma kwa hiyo ikabidi nitafute ndege leo asubuhi kuja hapa'

‘Ajali sasa hivi Tanzania zimechukua nafasi ya yale magonjwa tunayoyaogopa hasa kwa kuchukua maisha ya watu na kujeruhi na kuiingizia serikali gharama kubwa ya matibabu, hatuwezi kuliangalia hili swala hivihivi mimi kama Waziri wa uchukuzi nimewaambia wenzangu kuanzia sasa Watanzania wataona mabadiliko makubwa' - Dr. Mwakyembe

  • Tunaanza na hawa waliopata ajali, nimeelekeza na najua vyombo vinavyohusika Polisi pamoja na SUMATRA watatekeleza… kwanza kuzifungia kampuni za haya mabasi ya J4 na Mwanza Coach wasijihusishe na usafirishaji wa abiria tena, hatuwezi kuwa tunapata ajali za kijingajinga namna hiyo, nimeliona eneo lenyewe liko wazi kabisa lakini ni watu tu wameamua, dereva wa huku anamuona mwenzake na kusema mimi lazima anipishe' – Dr. Mwakyembe
  • Tumeelekeza Wafanye uhakiki wa madereva wao wote na tunahitaji picha zao lakini vilevile tunahitaji mikataba ya kazi, hatutaki mabasi ya kupeleka abiria yaendeshwe na watu tu kwa majaribio, nataka ushahidi wa kila dereva kwamba amejiunga na hii mifuko ya akiba ya Wafanyakazi, tuone kabisa mchango wa Mwajiri na mfanyakazi kila mwezi'
  • Nimeagiza lazima tuangalie BIMA ya hiyo gari, unajifikiria mwenyewe tu ukipoteza gari ulipwe kidogo gari yako lakini hufikirii kuhusu binadamu…. bila comprehensive haendeshi mtu gari kuchukua abiria.

MYTAKE:

1. naunga mkono poing number Mbili na hakika kama akisimamia na ikatekelezwa usafiri nchi hii utakuwa umeboreshwa sana, tatizo ni SUmatra kutosimamia hilo kwani limekuwa ni wimbo w akila siku.

2. Kuhusu BIMA nadhani anajichanganya kwani gari ikiwa na Comprehesive ndipo gari linaweza kulipwa na abiria anatakiwa kulipwa na Bima ya kawaida tu, hapo nilitegemea angasimamaia hao waliokufa na kujeruhiwa wanapata haki zao.
 
ikianza kwenye maji atatoa matamko pia?
 
Mwinyi alijiuzulu baada ya mahabusu kufa , huyu wamekuwa watu 40 anasema anataka picha za madereva , and yet mnaita uamuzi kweli?
 
Njia za ulimi wa nyoka hazifai tena Tanzania ,tunahitaji Dual carriageway ,hiyo anayotumia sio dawa ,wala si sababu ya waendesha na madereva ,sikubaliani nayo kabisa ni maonevu tu ,sasa unatarajia mabazi yaendayo mikoani yawe yanakwenda kwa speed ya 30km/h.

Uzembe wao wa kutokuzitanua barabara wasiwabebeshe watu wengine na kutafuta visingizio vya madereva ,sasa unachunguza leseni ,sijui nani alitoa nani alihonga ili kupata leseni ,ivi Tanzania hela inatumika kupata pasipoti ,watashindwa leseni mbona tunapumbazana !

Fungukeni mujenge njia za kisasa achaneni na dizaini za kizamani Tanganyika ilpokuwa na gari zinazohesabika ka gari kuminasaba . Mlisingizia madereva wanaendesha wakiwa wamelewa ikapita sasa mnakuja na leseni ni feki ,ukweli ni njia tu ,njia ni nyembamba sana sana ,Jamani Tanzania ni nchi kubwa sana kama mnaona shida kuweka njia mbili za lami basi hata za kifusi zitatosha na kupunguza ajali katikati mtapanga mawe na kupanda miti ila itajulikana njia moja ya kwendea na ingine ya kurudia.
 
This country bwana inawashinda nini kujenga dual carriageway 6 lanes on both sides? Wameshadidia kuiba fedha za walipa kodi.
 
Naunga mkono jitihada zozote kupelekea kupunguza kama sio kuondoa kabisa ajali zaidi barabarani, hasa mabasi ya abiria

Naunga mkono kufungia hizo kampuni mbili, nao waonje machungu tunayopata kwa kupoteza wapendwa wetu.

Naomba isiishie kuwa maneno tu tuone action.
 
Haya hapa maamuzi aliyoyatoa Waziri Mwakyembe baada ya ajali ya mabasi kuua watu 39 huko Musoma

1.jpg
Jana September 5 2014 kwenye eneo la Sabasaba hapa Musoma ilitokea ajali mbaya sana ya mabasi mawili yakiwa na abiria na kulihusisha gari jingine dogo ambapo majeruhi ni zaidi ya 70 na waliofariki ni 39 Wanawake kwa Wanaume kwa mujibu wa taarifa mpya za vifo zilizotoka muda mfupi uliopita.
Kwa kuguswa na tukio hili waziri wa uchukuzi Dr. Harryson Mwakyembe ilibidi aahirishe ratiba zake nyingine na kulazimika kuja Musoma kuwatembelea majeruhi leo asubuhi kwenye hospitali ya mkoa pamoja na kwenda kwenye eneo la ajali kutazama.
Baada ya hapo Waziri Mwakyembe metoa maamuzi yanayolenga kukomesha uzembe unaosababisha ajali hizo ‘Inabidi niwape pole Watanzania wote ambao wamepoteza ndugu jamaa na marafiki, taarifa za ajali nimezipata nikiwa Dodoma kwenye bunge maalum ikawa sasa nitafikaje haraka Musoma kwa hiyo ikabidi nitafute ndege leo asubuhi kuja hapa'
‘Ajali sasa hivi Tanzania zimechukua nafasi ya yale magonjwa tunayoyaogopa hasa kwa kuchukua maisha ya watu na kujeruhi na kuiingizia serikali gharama kubwa ya matibabu, hatuwezi kuliangalia hili swala hivihivi mimi kama Waziri wa uchukuzi nimewaambia wenzangu kuanzia sasa Watanzania wataona mabadiliko makubwa' - Dr. Mwakyembe

  • Tunaanza na hawa waliopata ajali, nimeelekeza na najua vyombo vinavyohusika Polisi pamoja na SUMATRA watatekeleza… kwanza kuzifungia kampuni za haya mabasi ya J4 na Mwanza Coach wasijihusishe na usafirishaji wa abiria tena, hatuwezi kuwa tunapata ajali za kijingajinga namna hiyo, nimeliona eneo lenyewe liko wazi kabisa lakini ni watu tu wameamua, dereva wa huku anamuona mwenzake na kusema mimi lazima anipishe' – Dr. Mwakyembe
  • Tumeelekeza Wafanye uhakiki wa madereva wao wote na tunahitaji picha zao lakini vilevile tunahitaji mikataba ya kazi, hatutaki mabasi ya kupeleka abiria yaendeshwe na watu tu kwa majaribio, nataka ushahidi wa kila dereva kwamba amejiunga na hii mifuko ya akiba ya Wafanyakazi, tuone kabisa mchango wa Mwajiri na mfanyakazi kila mwezi'
  • Nimeagiza lazima tuangalie BIMA ya hiyo gari, unajifikiria mwenyewe tu ukipoteza gari ulipwe kidogo gari yako lakini hufikirii kuhusu binadamu…. bila comprehensive haendeshi mtu gari kuchukua abiria.

MYTAKE:

1. naunga mkono poing number Mbili na hakika kama akisimamia na ikatekelezwa usafiri nchi hii utakuwa umeboreshwa sana, tatizo ni SUmatra kutosimamia hilo kwani limekuwa ni wimbo w akila siku.

2. Kuhusu BIMA nadhani anajichanganya kwani gari ikiwa na Comprehesive ndipo gari linaweza kulipwa na abiria anatakiwa kulipwa na Bima ya kawaida tu, hapo nilitegemea angasimamaia hao waliokufa na kujeruhiwa wanapata haki zao.

nimekuwa mteja mzuri wa mabasi ya mwanza coach kwa safari zangu nyingi niwapo mwanza-musoma.hawa jamaa hawa jamaa hawana record mbaya kwenye suala la ajali.ni muda cjasikia ajili katika hii kampuni.naona kama vile kuwafungia kwa kosa la dereva naona kama vile siyo haki.kuna kampuni ngapi zinafuata taratibu lakini ajali zimekuwa zikitokea?ni sawa kufanya uhakiki na pia ningeshauri fidia ilipwe kwa waathirika
 
Bongo kwa usanii bana, mtu anaongea musoma mbali na wakati watu wakotembea kutoka kwa miguu hapo wizarani na hapo polisi wakamate magari hapo posta mpya, watakuta madereva vimeo kibao labda kati ya daladala 5 mmoja ndo atakuwa ana vigezo vya kuendesha dala dala.. Waache usanii bana..
 
Naunga mkono jitihada zozote kupelekea kupunguza kama sio kuondoa kabisa ajali zaidi barabarani, hasa mabasi ya abiria

Naunga mkono kufungia hizo kampuni mbili, nao waonje machungu tunayopata kwa kupoteza wapendwa wetu.

Naomba isiishie kuwa maneno tu tuone action.

kufungia kampuni hakuta saidia,kaa ujua kuwa kati ya madereva hao wawili lazima kuna mmoja alikwa right na mwingine alikuwa wrong.so uifunge kampuni ya dereva aliyekuwa right itakuwa ni haki?labda tu tubadili mfumo wetu wa usafirishaji.kwani kampuni haihusiki kutoa leseni kwa madereva,serikali ndo inatoa leseni baada ya kuthibitisha mpokea leseni yuko timamu kwa kazi hiyo.sasa lawama zitaendaje kwa kampuni?
 
Tunaendeshwa na matukio J3 ikifika tushasahau kabisaaaaaaa Chezea Bongo.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kuzifungia kampuni itasaidia nini au inaingilianaje na ajali husika. Wenye makampuni wanaajiri madereva wenye leseni za udereva zinazotolewa na serikali na zinalipiwa kila baada ya miaka mitatu. Uzembe wa dereva barabarani unaangaliwa na polisi wa usalama barabarani, leseni bandia zinatakiwa zitambuliwe na polisi wa usalama barabarani, haya yote hayafanywi kwa sababu ya kutamalaki kwa rushwa. Ingekuwa magari yalikuwa mabovu hapo wenye makampuni wangehusishwa lakini bado haitoshi kwani polisi wa usalama barabarani waliyaruhusu vipi yaanze safari yakiwa mabovu. Wajipime upya na waje na mbinu mpya.
 
Njia za ulimi wa nyoka hazifai tena Tanzania ,tunahitaji Dual carriageway ,hiyo anayotumia sio dawa ,wala si sababu ya waendesha na madereva ,sikubaliani nayo kabisa ni maonevu tu ,sasa unatarajia mabazi yaendayo mikoani yawe yanakwenda kwa speed ya 30km/h.

Uzembe wao wa kutokuzitanua barabara wasiwabebeshe watu wengine na kutafuta visingizio vya madereva ,sasa unachunguza leseni ,sijui nani alitoa nani alihonga ili kupata leseni ,ivi Tanzania hela inatumika kupata pasipoti ,watashindwa leseni mbona tunapumbazana !

Fungukeni mujenge njia za kisasa achaneni na dizaini za kizamani Tanganyika ilpokuwa na gari zinazohesabika ka gari kuminasaba . Mlisingizia madereva wanaendesha wakiwa wamelewa ikapita sasa mnakuja na leseni ni feki ,ukweli ni njia tu ,njia ni nyembamba sana sana ,Jamani Tanzania ni nchi kubwa sana kama mnaona shida kuweka njia mbili za lami basi hata za kifusi zitatosha na kupunguza ajali katikati mtapanga mawe na kupanda miti ila itajulikana njia moja ya kwendea na ingine ya kurudia.

Gari imetengenezwa (designed) kuendesheka katika mazingira tofauti, ndo maana kuna accelerator, brake, steering wheel nk. Sababu ya barabara kuwa nyembamba haitoshi kuwa kisingizio cha kunywa damu za watanzanka maskini wanaohangaika kusaka shilingi. Wafungiwe tu.
 
Back
Top Bottom