Mwakyembe achukua maamuzi baada ya ajali Musoma

Mwakyembe achukua maamuzi baada ya ajali Musoma

Madege

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2011
Posts
530
Reaction score
111
Jana September 5 2014 kwenye eneo la Sabasaba hapa Musoma ilitokea ajali mbaya sana ya mabasi mawili yakiwa na abiria na kulihusisha gari jingine dogo ambapo majeruhi ni zaidi ya 70 na waliofariki ni 39 Wanawake kwa Wanaume kwa mujibu wa taarifa mpya za vifo zilizotoka muda mfupi uliopita.

Kwa kuguswa na tukio hili waziri wa uchukuzi Dr. Harryson Mwakyembe ilibidi aahirishe ratiba zake nyingine na kulazimika kuja Musoma kuwatembelea majeruhi leo asubuhi kwenye hospitali ya mkoa pamoja na kwenda kwenye eneo la ajali kutazama.
Baada ya hapo Waziri Mwakyembe akaongea na millardayo.com na kueleza yafuatayo >> ‘Inabidi niwape pole Watanzania wote ambao wamepoteza ndugu jamaa na marafiki, taarifa za ajali nimezipata nikiwa Dodoma kwenye bunge maalum ikawa sasa nitafikaje haraka Musoma kwa hiyo ikabidi nitafute ndege leo asubuhi kuja hapa'

Tunaanza na hawa waliopata ajali, nimeelekeza na najua vyombo vinavyohusika Polisi pamoja na SUMATRA watatekeleza… kwanza kuzifungia kampuni za haya mabasi ya J4 na Mwanza Coach wasijihusishe na usafirishaji wa abiria tena, hatuwezi kuwa tunapata ajali za kijingajinga namna hiyo, nimeliona eneo lenyewe liko wazi kabisa lakini ni watu tu wameamua, dereva wa huku anamuona mwenzake na kusema mimi lazima anipishe' – Dr. Mwakyembe

Tumeelekeza Wafanye uhakiki wa madereva wao wote na tunahitaji picha zao lakini vilevile tunahitaji mikataba ya kazi, hatutaki mabasi ya kupeleka abiria yaendeshwe na watu tu kwa majaribio, nataka ushahidi wa kila dereva kwamba amejiunga na hii mifuko ya akiba ya Wafanyakazi, tuone kabisa mchango wa Mwajiri na mfanyakazi kila mwezi'
Nimeagiza lazima tuangalie BIMA ya hiyo gari, unajifikiria mwenyewe tu ukipoteza gari ulipwe kidogo gari yako lakini hufikirii kuhusu binadamu…. bila comprehensive haendeshi mtu gari kuchukua abiria.

 
Amefurahishwa na ajali au nini sijaelewa!!!! kuja na ndege kuna uhusiano gani na ajali? Wanyakyusa utawajua tu.

kafurahishwa na kuahirishwa tamasha lililokuwa lifanyike huko musoma. i think ni leo so wameahirisha hadi jumanne.

kapanda ndege ili awahi kuwaona majeruhi wa ajali
 
Porojo tupu, nothing will be done. Rushwa ya jeshi la trafiki barabarani yataendelea kutokea.
 
kafurahishwa na kuahirishwa tamasha lililokuwa lifanyike huko musoma. i think ni leo so wameahirisha hadi jumanne.

kapanda ndege ili awahi kuwaona majeruhi wa ajali

good dr Mwakyembe
 
mmmh! kwa Tanzania yetu ya Chama Cha Majitaka, ... Hii inaitwa funika kombe, ili mwanaharamu aende zake!
 
FIESTA KWELI NI SHIDAAAAA NGOJA SIKU NYINGINE EL SHABABIII WAWATEMBELEE KAMA EAST GATE MALL KENYA NDIO WATU WAKOMEEE KWENDA KWENYE HAYO MATAMASHA
NI SHIDaaaaaaaaaaaaaaaaaaa ngoja waipate
ila pole sana wana musoma wakiongozwa na USTADH JUMA NA MUSOMA
Kilimanjaro tour kikwetukwetu stand upppppppppppp
 
kafurahishwa na kuahirishwa tamasha lililokuwa lifanyike huko musoma. i think ni leo so wameahirisha hadi jumanne.

kapanda ndege ili awahi kuwaona majeruhi wa ajali


Akiwaona ndiyo watapona haraka?
 
Jana September 5 2014 kwenye eneo la
Sabasaba hapa Musoma ilitokea ajali mbaya
sana ya mabasi mawili yakiwa na abiria na
kulihusisha gari jingine dogo ambapo majeruhi
ni zaidi ya 70 na waliofariki ni 39 Wanawake
kwa Wanaume kwa mujibu wa taarifa mpya za
vifo zilizotoka muda mfupi uliopita.


Kwa kuguswa na tukio hili waziri wa uchukuzi
Dr. Harryson Mwakyembe ilibidi aahirishe
ratiba zake nyingine na kulazimika kuja
Musoma kuwatembelea majeruhi leo asubuhi
kwenye hospitali ya mkoa pamoja na kwenda
kwenye eneo la ajali kutazama.

Baada ya hapo Waziri Mwakyembe akaongea
na millardayo.com na kueleza yafuatayo >>
‘Inabidi niwape pole Watanzania wote ambao
wamepoteza ndugu jamaa na marafiki, taarifa
za ajali nimezipata nikiwa Dodoma kwenye
bunge maalum ikawa sasa nitafikaje haraka
Musoma kwa hiyo ikabidi nitafute ndege leo
asubuhi kuja hapa’
Kuhusu Wasanii wa bongofleva na Clouds
Media Group kufanya maamuzi ya kuahirisha
tamasha ambalo lilikua lifanyike jana hapa
Musoma, Waziri Mwakyembe amesema >> ‘hii
imenifurahisha sana… inaonyesha Utanzania
tulionao Watanzania, ni vizuri wamefanya hivyo
na ninawapongeza sana Clouds Radio kwa
kuguswa na maswala ya jamii’

‘Ajali sasa hivi Tanzania zimechukua nafasi ya
yale magonjwa tunayoyaogopa hasa kwa
kuchukua maisha ya watu na kujeruhi na
kuiingizia serikali gharama kubwa ya matibabu,
hatuwezi kuliangalia hili swala hivihivi mimi
kama Waziri wa uchukuzi nimewaambia
wenzangu kuanzia sasa Watanzania wataona
mabadiliko makubwa’

ukiangalia eneo la ajali ni sehemu ambayo dereva aliekua anatokea huku na
mwingine anaekuja walikua wanaonana wazi
kabisa na haikuwa usiku

1. Tunaanza na hawa waliopata ajali,
nimeelekeza na najua vyombo vinavyohusika
Polisi pamoja na SUMATRA watatekeleza…
kwanza kuzifungia kampuni za haya mabasi
ya J4 na Mwanza Coach wasijihusishe na
usafirishaji wa abiria tena, hatuwezi kuwa
tunapata ajali za kijingajinga namna hiyo,
nimeliona eneo lenyewe liko wazi kabisa
lakini ni watu tu wameamua, dereva wa huku
anamuona mwenzake na kusema mimi
lazima anipishe’ – Dr. Mwakyembe

2. Tumeelekeza Wafanye uhakiki wa
madereva wao wote na tunahitaji picha zao
lakini vilevile tunahitaji mikataba ya kazi,
hatutaki mabasi ya kupeleka abiria
yaendeshwe na watu tu kwa majaribio,
nataka ushahidi wa kila dereva kwamba
amejiunga na hii mifuko ya akiba ya
Wafanyakazi, tuone kabisa mchango wa
Mwajiri na mfanyakazi kila mwezi’

3. Nimeagiza lazima tuangalie BIMA ya hiyo
gari, unajifikiria mwenyewe tu ukipoteza gari
ulipwe kidogo gari yako lakini hufikirii kuhusu
binadamu…. bila comprehensive haendeshi
mtu gari kuchukua abiria.

Chanzo: millardayo

Nimaneno mazuri kama yakifanyiwa kazi hasa hapo kuzifungia kampuni kama fundisho kwa wengine na pia mikataba ya kazi na bima ya wasafiri
Lakini siku zote mlikuwa wapi ,jitahidini sana kwani ajali mwaka zimetisha sana
 
FIESTA KWELI NI SHIDAAAAA NGOJA SIKU NYINGINE EL SHABABIII WAWATEMBELEE KAMA EAST GATE MALL KENYA NDIO WATU WAKOMEEE KWENDA KWENYE HAYO MATAMASHA
NI SHIDaaaaaaaaaaaaaaaaaaa ngoja waipate
ila pole sana wana musoma wakiongozwa na USTADH JUMA NA MUSOMA
Kilimanjaro tour kikwetukwetu stand upppppppppppp

Daaah!! Sijaelewa ili nimejikuta nimekupa like mkuu
 
yani mi nakereka mpaka majanga yatokee ndio matamko yatoke.
Atujachelewa nina iman na kauli yako.
 
Idara ya Traffic Police nayo imeoza! Wao ndo wenye jukumu la kuhakikisha competitive drivers wanapatikana. Wamekuwa wakiwapa hata madereva watoto class ambazo kisheria hawaruhusiwi. Traffic wanaona na wanachukua hongo tuu na kuwaacha waendeshe wanavyotaka. Nao wawajibishwe pia. I do believe before every departure of any bus there is officer in charge anayekagua dereva anayeendesha bus husika. Some of drivers wanakunywa pombe asubuhi wanatakiwa wapimwe! Wengine ni wagonjwa je wanapimwa! If I was in the government its high time sasa kuweka camera with database ambayo ni vigumu kuhongwa!
 
R.I.P Wote Walio Tangulia Mbele Ya Haki.Na Pia Serikali Hii Iliyo Katwa Masikio ione Uchungu Juu Ya Suala Hili .Kufungia Magari Sio Njia Yakutatua Tatizo ,kwasababu Magari Haya Jiendeshi .Ni Uzembe Wa Madereva Na Polisi Kupenda Rushwa Huku Watu Wakiendelea Kupoteza Maisha Kwa Uzembe Wao.
 
Too little too late. Nahisi Mh Malecela angepewa nafasi tusingefika huku. Ndiye aliyebuni mpango wa mabasi kusafiri mchana na speed governor. Wajanja wakafanya yao matokeo twayaona
 
njia pekee ya kukomesha tatizo la ajali za kizembe barabarani ni kuweka sheria kali kama vile kifungo cha maisha au kunyongwa kabisa lakini rushwa sasa kwenye izo idara husika ni balaa!mtu anafanya uzembe anaua watu kwa ajari za kizembe kesho utamkuta yupo na gari jingine anatamba duniani.inaniuma sana kuua watu wasio na hatia Kwa nini kila siku ni Tz?
 
Back
Top Bottom