Hassan Mwakinyo kupanda ulingoni April, kuchangia taulo za kike. Wabunge sita kuzichapa kwenye mapambano ya utangulizi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,014
9,883
Bondia wa Kitanzania Hassan Mwakinyo anatarajiwa kuingia ulingoni tarehe 23 Aprili 2023 katika Uwanja wa Jamhuri huko Dodoma kupambana na mpinzani wake kutoka Kongo, Kuvesa Katembo. Pambano hilo, ambalo sio la ubingwa, limeandaliwa na kampuni ya Lady in Red Promotion, ambayo iko chini ya Mbunge wa Mkoa wa Mbeya, Mheshimiwa Sophia Mwakagenda, kwa lengo la kukusanya taulo za kike kwa ajili ya wanafunzi katika maeneo ya Kusini mwa Tanzania.

Katembo, ambaye tarehe 1 Julai mwaka jana alishindwa kwa pointi nchini Tanzania dhidi ya Hamis Maya, amecheza mapambano 22, ameshinda 14, amepoteza 7 na kutoa sare 1. Hii ni mara ya kwanza tangu tarehe 3 Septemba 2021, Mwakinyo anapigana katika ardhi ya Tanzania, ambapo pambano la mwisho kucheza Tanzania, alishinda kwa TKO raundi ya 4 dhidi ya Julius Indongo wa Namibia.

Kuelekea pambano lisilokuwa la ubingwa kati ya Hassan Mwakinyo na Kuvesa Katembo kutoka Afrika Kusini tarehe 23 Aprili, 2023, Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini, Mheshimiwa Joseph Msukuma ameomba kupigana katika pambano la awali na Mheshimiwa January Makamba, wakati Mheshimiwa Hamis Taletale ameomba kupigana na Mheshimiwa Kingu. Lengo la kampeni hii ni kukusanya taulo za kike kwa watoto wenye mahitaji katika maeneo ya vijijini.

Wabunge sita wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watashuhudia pambano kati ya Hassan Mwakinyo na Kuvesa Katembo litakalopigwa tarehe 23 Aprili katika Uwanja wa Jamhuri huko Dodoma. Wabunge hao watashiriki katika pambano la dakika tatu kila mmoja ambapo Joseph Kasheku 'Musukuma' atavaa gloves na kupigana na January Makamba, Babu Tale atapanda ulingoni na Elibariki Kingu wakati Salome Makamba atawapiga na Neema Lugangira. Mgeni rasmi katika pambano hilo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.

337421507_966766004489258_2438331473823271092_n.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom