Mwaka Wa 20 Sijaugua Malaria

Umejaliwa sana ndg yetu. Hii ni sawa na watu wetu kule vijijini hunywa maji yasiyochemchwa, maziwa mabichi, matunda hawayaoshi, wananawa wote ktk chombo kimoja nk, lakini hawapatwi na maradhi kama typhoid nk kwa miaka nenda rudi. Hudhani labda mwili hujijengea kinga.
 
Ni miaka ishirini imepita tokea nimepata tiba ya Malaria.Na mbu kila siku wananingata....Je kuna tatizo lolote?Nahitaji mawazo yenu Madaktari

Wewe badala ya kumshukuru Mungu kwa kutokuugua unaleta hoja ambayo kwangu naiona haina msingi, au umesahau kuwa adui mmojawapo wa mtu ni magonjwa? Pia umesau kuwa malaria inaongoza kwa kuua kuliko ukimwi? Tafuta ile thread ya yule mtu aliyetangaza DAU kwa yeyote atakayemsadia kupata tiba ya malaria iliyomsumbua kwa miaka 20, mwombe Mungu akusamehe kwa kutokujua uliwazalo kwani kuugua siyo jambo la kufurahisha wala kupendeza
 
Ni miaka ishirini imepita tokea nimepata tiba ya Malaria.Na mbu kila siku wananingata....Je kuna tatizo lolote?Nahitaji mawazo yenu Madaktari

Mkuu mimi nadhani kuna damu hazishiki malaria,mimi sijawahi kuugua malaria wala sikumbuki labda nlipokuwa mdogo lakini sasa nakata miaka 30 na ushee sijawahi kuugua malaria,alhamdulillah namshukuru mungu
 
Upo sawa kabisa, mie nina mwaka wa 25+ sijaugua malaria,
na nimeishi dar, mtwara, tabora na kiasi tanga sikuwahi
kupata huo ugonjwa,sijawahi kupima group la damu na wala
sielewi kwanini sipati malaria ingawa namshukuru mungu kwa hilo.
Labda madaktari waseme madhara ya hali hii.
 
Back
Top Bottom