Msaada ugonjwa wa kupungukiwa damu

Kuna dada alijifungua mtoto miezi mitano iliyo pita sasa ameshikwa na ugonjwa wa kupungukiwa damu sana kila akienda hospital anaingezewa damu lakini siku iyoiyo inakeisha tena na madaktari wamempima kila kitu haonekani na tatizo lolote sasa kwann damu inakauka tu??
Pole Sana mkuu mnaweza kujaribu pia hosptali nyinginge maana usitazame tu ukubwa wa hosptali ila huuduma na wataalamu hivyo ikiwa yupo Sehemu moja ila hajapata matibabu sahihi anaweza kubadilisha hosptali

Pia mfumo wa Maisha lifestyle ajaribu kuzingatia Kama kula vyakula vinavyoongeza damu na vinywaji vinavyoongeza damu.

Pia kuweni na Imani kwa kumuomba Mungu kuwa atatenda.

All the best Mungu akawatie Nguvu katika mapito yenu na amjaze mgonjwa Afya katika Mwili wake wa damu nyama na mifupa.🙏
 
Pole sana Mkuu kwa changamoto mnayopitia.

Wakati mnaendelea na matibabu jaribu kutumia option nyingine

Kama ninyi ni watu wa imani, usisite kumkabidhi kwenye maombi.

Kama mna imani ya wastani, tafuteni mtaalamu wa mambo ya Kienyeji awasaidie.

Kuna dalili mgonjwa ametupiwa kitu kinachotaka kumuondoa uhai kwa kumkausha damu.
 
Kuna kiumbe kinanyonya RBC zake nini sio upungufu wa Madini chuma kweli?

Sababu za upungufu wa damu mwilini:-

1. Upungufu wa madini ya chuma mwilini

2. Upungufu wa vitamini A na B-12 mwilini

3. Maradhi kama HIV, UKIMWI, saratani, mardhi ya figo haya huweza kuleta upungufu wa damu

4. Mfumo wa kinga mwilini kuuwa na kuharibu seli hai nyekundu (autoimmune)

5. Uharibifu wa seli hai nyekundu kufanyika kwa haraka kuliko utengenezwaji.

6. Kuwa na maradhi ya sickle cell anemia

Kazi za damu mwilini:-

1. Kusafirisha viinilishe kutoka katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kwenda maeneo mbalimbali ya mwili.

2. Kusafirisha hewa ya oksijeni kutoka kwenye mapafu kwenda maeneo mengine ya mwli.

3. Kusafirisha hewa ya kabonikaiyoksaidi kutoka kwenye seli na kupeleka kwenye mapafu kwa ajili ya kutolewa nje

4. Kudhibiti joto la mwili kwa kulipooza inapohitajika na kuliongeza inapohitajika

5. Kusafirisha homoni kwenda maeneo mbalimbali ya mwili.

Vyakula vya kuongeza damu mwilini:-

1.Nyama nyekundu kama nyama ya ng’ombe, mbuzi na Kondoo

2.Maini

3.Nyama ya figo

4.Mboga za rangi ya kijani kama mchicha na spinachi

5.Maharagwe

6.Kunde

7.Mayai

8.Nafaka nyinginezo

9.Njegere

10.Korosho na karanga

11.Samaki

12.Nyama ya ndege

13.Karoti

14.Matikiti

15.Zabibu

16.Viazi vitamu

17.Matunda yenye uchachu kama machungwa, ndimu na limao.

18.Polipili nyekundu
 
Safi kabisa. Aongeze na Juice ya beetroots.

Watu wengi wanapougua wanakimbilia kutumia dawa kwa wingi lakini wanasahau umuhimu wa lishe katika kutibu maradhi. Possibly anaweza kuwa na Iron deficiency anaemia
 
Jamaa amesema wamekwenda hospitali zaidi ya 5 na kote wanapata jibu lilelile, maana yake ni kuwa, wameambiwa ana tatizo gani, sio kukisia tena.
 
Back
Top Bottom