Mwaka unaisha waungwana! Mwenzenu sijatimiza malengo kabisaaa! Nijiokoe vipi kikao cha familia?

Mmmmh nashukuru mungu tena na tena, katika malengo yangu niliyopanga mwaka huu mawili sijatimiza......can't complain.
[MENTION]Lara1[/MENTION] , nimependa utaratibu wa family yenu. Mbarikiweee na mimi nikumbuke kwenye maombi.
 
Yataanza maombi ya ugonjwa kwanza!!!!!!!! Then nitaambiwa niandike summary niwape madogo wasome kwa niaba yangu, hapo ndo itakuwa AIBU BIN FEDHEHAAAA!!!!!!!!!!


kwa nini usisingizie uko Preg ya huyo Mchagga ? watafoka watanyamaza
Nilitegemea Mchagga anihonge Gari (Nijifanye nimenunua), bado anasitasita na Kadi kaandika jina lake, mara anipe, mara achukue gari lake hata Nizae tuuu, wapiiiiii!!!!!
 
Wakubwa zangu shikamooni!!!!!!!!

Peopleeeeeess Niaje (Kwa Masela) Habari za jioni (Civilized), Tumsifu yesu kristu (Roman), Bwana Asifiwe(Protetistants), Assalam Alaikum (السلام عليكم) (Muslims) Mungu Ibariki Tanzania (Pagans)

Leo ni kati ya siku ambazo im more civilized than anybody! Naombeni ushauri, niko in a real familly fiasco!! Hapa natamani nistopishe jua kuwaka maana muda umeishaaaaa!

Sisi kama familia huwaga kila Mwanzo wa Mwaka 2/1 tunakaa as a family na kufanya misa pamoja na paroko na my aunt Sister/Nun ya kumshukuru mola kwa mema ya mwaka mzima, na kwa kuuona mwaka mpya!!!!! (Dnt be shocked i come frm a very religious family, huu ukuda ni kati ya zile zilizoanguka kwenye miiba, njiani na kwenye mwamba) Ni utaratibu mzuri sana kufanya as a family.

Baada ya ibada na family get together (sipendi kuosha mijombo baada ya watu kusaza!!!!! Mmmh!) tunakaa as a family NA KUREVIEW MALENGO YA KILA MMOJA ALIYOTOA MWAKA JANA!, UNAJIELEZEA UMEFIKIA WAPI?! UMEFANIKIWA YAPI!? VIKWAZO NINI?! USAIDIWAJE?! KAMA KUNA JANGA LILIKUPATA, UNAMALIZIA NA MWAKANI WAJIPANGAJE NA MALENGO MAPYA!!! Kila mtu anasema Kuanzia Mdingi hadi Beki tatu. Kila mtu manake kila mtu!!!!

Kwenye Tatizo langu sasa!!! Baada ya kila mtu kusema WALE WASHINDWAJI SUGUUUU (Hata lengo moja hamna kutimia) MNAFANYIWA MAOMBI MAALUMU sababu yawezekana si bureeeee!!!! Mizambiii imewazidii ili mpate baraka za ziada na Mungu awafanyie mizigo yenu myepesi!!!!! Sasa SAFU YA WASHIDWAJI SUGUUUU INAJULIKANAAA!!!!!!!! Ni safu ya aibu sanaaaaaa! Daaaaah! Ukikaa hii safu utafanya kazi kama mwehu usirudi tenaaa! Sasa mimi safu inaninukiaaaa! Mama yangu hapendi kabisaa mimi kukaa hii safu, hapa nae anahahahaa kuninusuru!!!


Sijatimiza hata lengo mojaaaa!!!! Nilitegemea ningekuwa Certified nimeshikwaaa!!!, Nilitegemea lile PROMO linitoe Bosi kabana ndo hivo hearing imeisha nimeshinda BONAS tuu ila PROMO badoooo sanaaa!!!! Nilitegemea Mchagga anihonge Gari (Nijifanye nimenunua), bado anasitasita na Kadi kaandika jina lake, mara anipe, mara achukue gari lake ilimradi purukushani!!!! Nilitegemea Niolewe au hata Nizae tuuu, wapiiiiii!!!!! Ningeanza hata msingi, wapiii!!! Hata hela ya kufyekea sinaaa!!!!! GUYS I GOT NOTHING TO SHOW!!!!! NOTHING!!!! NOTHING AT ALL!!!!!!!

Bora wale ambao Mungu hakuwabariki kazi nzuri( hata za mawazo kama yangu) wana cha kujikoshaaa!!! Mie zaidi ya KUTIRIRISHA MAJI YA DHAABU!!!! KUVAAAAAA!!!!! KUTREAT WATU!!!!! KUPARTY!!!!! KUPONDA MALI KUFA KWAJAAA!!!! SIJAFANYA LOLOTE LA MAANA!!!! KAZI IPO!!!! Nawaza jinsi ya kutoa USHUHUDA WA KUPOTOKA siku hiyooo!!!!!! PESA YA KUFANYA MUUJIZA HUU MWEZI ULIOBAKI SINAAAAA!!!!!

Hapa nangojea Muujiza tu, mtu anihonge Ghorofaaaa!!!! lolest!!!!!

Mwaka waishaaaa hivo wana jamvi!!!! MJIULIZE MMEFANYA NINI SIO KUJITIA MWANISIKITIKIA KUMBE NA NYIE HOLAAAAA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!?

kukosa leo sio tatizo tumia kesho yako vizuri
 
Bora nimegraduate kimasters changu cha engineering kwa mbinde japo naweza kujitutumua kwa hilo lakini kwenye mpango wa njuruku bila bila nitasema kwamba nilikuwa natetea kishule changu
 
Hii sredi imeniacha mdomo wazi...lol
Hivi kweli mwaka unaisha eh???
Kibongobongo kuwa na malengo kazi usawa wenyewe wa kulenga kwa manati!!
Mdogo wangu lara 1 kama TBL wanatoaga bonus kwa wanywaji bora huenda ndio tuzo niliyobakiwa nayo...lol



Mkuu kwenye tuzo hiyo tunaweza kuwa wote maana malengo buku umefanikisha moja aiseeee very sad
 
Last edited by a moderator:
Bora nimegraduate kimasters changu cha engineering kwa mbinde japo naweza kujitutumua kwa hilo lakini kwenye mpango wa njuruku bila bila nitasema kwamba nilikuwa natetea kishule changu

Hongera mwaya shule ilivyongumu tena hii ya masters lool sina hamu mimi kwakweli
 
Hongera mwaya shule ilivyongumu tena hii ya masters lool sina hamu mimi kwakweli



wewe acha tu mkuu yani mpaka unajuta halafu unakuwa na gf akaelewe kanakuona kama unacheza mbona alivyonipiga chini nilishukuru sana aiseeee
 
wewe acha tu mkuu yani mpaka unajuta halafu unakuwa na gf akaelewe kanakuona kama unacheza mbona alivyonipiga chini nilishukuru sana aiseeee

Haah hah pole sana ila mimi hii shule nimeona ngumu kuliko shule zangu zoote kwakweli na mawalimu yanasumbua mno,
 
Haah hah pole sana ila mimi hii shule nimeona ngumu kuliko shule zangu zoote kwakweli na mawalimu yanasumbua mno,

Hahahahahahaha.....mimi kameisha kwa mbinde na mazingira ya udsm hatari unaweza kulala mbele
 
mda bado siku nne ni nying sana in life.mabadiriko yanatokea hata kwa dk tu sijakata tamaa ntatoboa tu
 
mda bado siku nne ni nying sana in life.mabadiriko yanatokea hata kwa dk tu sijakata tamaa ntatoboa tu

Dah.....mkuu unasubiri maajabu ya siku duh...mimi nimeshakata tamaaa ngoja nisubiri mwakani hila nimecheka sana
 
Mimi nimefanikiwa kuwachangia sana TBL na sometimes wale Konyagi distillers ila mwaka ujao naahirisha kunywa kabsaaaaa
 
kwenye mwaka unaogawanyika sijawahi pata ugumu so i do expect great things

Kwangu mimi mwaka huu ulikuwa mgumu wenye vikwazo vingi sana ingawa nashukuru Mungu kuna vilivyofanyika a step forward,natumaini mwaka ujao utakuwa wa mafanikio kwangu.
 
the worst year ever...nilitundika mimba mbili kwa mwanamke mmoja na zote akatoa...cha ajabu ya pili ilikuwa ni mapacha...na akatoa bila ya kunishirikisha, ukizingatia ni 30+ ..ukimuuliza, i want to enjoy more the life..

nikakimbiza mwizi...
 
Back
Top Bottom