Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,753
- 7,844
Hata mie imeniuma sana na kunikumbusha kisa nilichokutana nacho jana,
Dada mmoja jirani yetu jana alipewa kipigo kama kibaka...
Wakati tunatoka kanisani tukakuta majirani wanaamulia ugomvi. Dada huyo alitumia simu ya mume wake kuwasiliana na dada yake (wana simu moja ambayo wanaichangia wote mume na mke). Bahati mabaya hakumpata dada yake kwenye simu. Baadaye kidogo, dada yake akapiga na simu kupokelewa na shemeji yake. Dada wa huyo mke alimweleza shemeji yake kuwa amekuta missed call. Mume akamvaa mke wake na kumuuliza kuwa, kwa nini anabeep watu kwa simu yake? Dada wa watu akajaribu kujieleza kuwa hakubeep bali alipiga lakini akamzidishia hasira mume wake na kuanza kupata kipigo. Yaani alipigwa ngumi, mateke na vibao kama vile ni kibaka kaiba cheni!!
Basi tena, sikutaka kuongelea haya mambo ya kupigana kwa sababu yananikera sana!1
huyu dada anahitaji awe na kaka kama Asprini....
lakini kwanini na nyie hamkuamulia bana? aisee ugomvi wa mke na mume kiasi cha majirani kusikia hii haijanikalia sawa aisee...nimejiskia uchungu sana.