Mwaka mpya 2021, ni mwaka wa kuendelea kufanya kazi na kuwajibika kwa uweredi na utaalamu kwa kuzingatia taaluma

The Giantist

JF-Expert Member
Dec 12, 2018
214
86
Na:
Mwesa, C.W
DODOMA.
31.12.2020

Ndugu watanzania wenzangu na wanachama wenzangu wa chama pendwa cha watanzania wote na Afrika kwa jumla, Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kwa hakika tunayo mambo mengi ambayo kimsingi tumeyapitia kama taifa kwa jumla na ki-nafsi kila mmoja kwa nafasi yake. Hata hivyo, katika hayo mambo ni mengi yamekuwa shule kwetu kwani kwa hakika yalituachia elimu na maarifa, ifahamike kuwa 'mtihani wo wote usiochukua uhai wa mtu, hakika ni shule kwa mtu.'

Tumekuwa na wajibu mkubwa na kwa hakika ilitulazima kutimiza wajibu huo, kwani haikutupasa kuuacha hata kwa muda mchache na hata kuukimbia, kwani tulifahamu wote kuwa 'matatizo hayakimbiwi, na kama utafanikiwa kuyakimbia basi ni dhahiri jiandae kukumbana nayo katika siku za usoni.' dawa ya kutibu matatizo ni kuwajibika kwa lazima na sio kwa hiari binafsi. Ni lazima kuyatatua matatizo mara yanapojitokeza na hiyo ndio dhana ya safiri kwa salama, kwani matarajio yake ni mwisho ulio salama na kheri.

Kwa hakika, maisha ya kila mtanzania huwa ni maisha endelevu siku zote, ilhali bado ni mtanzania anayeishi. Na ikiwa jambo hilo ni sahihi kabisa, basi tunapozungumzia kuhusu matarajio yenye mwisho ulio na kheri, maana yake ni kuleta matokeo yenye tija kwa maisha ya mtu na jamii pana ya watanzania. Ndio kusema, matarajio yo yote yenye shabaha ya kuleta matatizo kwa mtu na jamii pana ya watanzania, matarajio hayo hayawezi kupata uhalali wa kusema kuwa ni wenye mwisho wenye kheri na salama.

Tunafahamu kuwa chama (CCM) kimefanya kazi kwa sehemu yake, kwa miongozo sahihi ya viongozi wetu wote kuanzia ngazi ya shina mpaka ngazi ya taifa. Wanachama pamoja na wapenda maendeleo wote nchini walishirikiana kwa pamoja na viongozi ili kwamba kukirahisishia chama kuweza kutimiza majukumu yake ya kikatiba kama ilivyojiwekea. Wote tunafahamu kuwa, wajibu wa chama ni kushinda katika chaguzi zote na kuunda serikali itakayoongoza dola. Na itafanya kazi hiyo ikiwa na lengo kuu moja la kuwahudumia wananchi. Hivyo basi tulishuhudia chama kikitekeleza majukumu yake hayo kwa kutimiza malengo yake hayo kuanzia uchaguzi wa 2019 na hata uchaguzi mkuu wa 2020.

Wananchi yaani watanzania wote, nao kwa nafasi yao walitekeleza wajibu wao wa msingi wa kujenga taifa lao wenyewe, kwa kutumia falsafa ya HAPA KAZI TU, iliyoasisiwa na Rais Dkt. JPM. Kwamba, ni kwa kufanya kazi tu, ndipo tutaweza kulijenga taifa letu na kuongeza mapato yetu na kujaza maghala yetu kwa chakula. Tangu kuingia kwa awamu ya Tano madarakani kuanzia 2015 mpaka 2020, watanzania wameshiriki wote katika umoja kwa ujenzi wa taifa, hivyo kulifanya taifa letu kuwa miongoni mwa mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara ambapo uchumi wake unakuwa kasi. Moja ya mafanikio makubwa ya watanzania, ni kufanikisha kuipandisha nchi kuwa katika nchi zenye uchumi wa kati.

Falsafa ya HAPA KAZI TU, ndio ambayo iliipa heshima Tanzania na watanzania wote. Kwani ni katika hiyo falsafa, Dunia imeona hatua ambayo Tanzania imepiga kiuchumi, kijamii na kisiasa. Lakini pia chini ya mwanafalsafa Rais Dkt. John P. Magufuli, watanzania waliuvuka mwaka 2020 katikati ya janga kubwa la kitaifa la Covid-19 kwa maombi ya siku tatu mfululizo. Hivyo basi falsafa ya kufanya kazi, haiwezi kuwa na tija kama haitashiriki kwa pamoja na sala / maombi kwa Mwenyezi Mungu (s.a.w). Tanzania iliweza kuwa imara kiuchumi na salama kiafya si kwa sababu haikuwa kwenye huzuni ya covid-19, ila ni kwa sababu Covid-19 ilikuwa kwenye huzuni ya kuondolewa kwa nguvu za sala ya taifa na wananchi kuendelea kuchapa kazi!

Leo tunaelekea mwaka 2021, ni wajibu wetu kama wananchi na wanachama, kushiriki kuwapa nguvu na hali viongozi wa chama (CCM) kwani ndicho chama hicho kinachoongoza dola na serikali: ili kiweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa wa kuweza kuondoa kabisa matatizo ya wananchi kwa mujibu wa miongozo yake ya kidemokrasi, haki na heshima, ujamaa na kujitegemea kwa kufanya kazi. Lakini pia mwaka 2021 ukawe ndio mwaka wa kujenga taswira maridhawa ya 2025 ya kufikia maendeleo makubwa zaidi ya kiuchumi, ambapo inatulazimu Mimi na wewe kuendelea kujituma na kuongeza weredi katika kufanya kazi kitaaluma na kitaalamu, ilo adhima yetu ya kulijenga taifa imara kiuchumi likatimie.

Kazi kubwa imekwishafanyika na CCM ndani ya miaka mitano na ikaitimishwa mwaka wa 2020, jambo hilo ni la hakika kwa kila mtu, ndani ya Tanzania na nje ya nchi. Mwaka 2021 ukawe ni mwaka wa heri na mwaka wa kufanya kazi kubwa zaidi, ili CCM iendelee kuwa ni wa mfano kwa mataifa mengine Duniani, hasa kwa mataifa ya Afrika ambayo mengi ni yanayoendelea.

Mwaka 2021 ukawe na mafanikio makubwa kwa CCM, kwa wanaCCM, kwa wananchi na taifa kwa ujumla. Ninawatakia wote heri katika mwaka mpya wa 2021. Tukafanye kazi kwa maslahi yetu na taifa letu kwa jumla.

Kheri ya mwaka mpya 2021!!!!
 
Uweredi kama ulivyoandika hapo juu katika Headline yako ndiyo Kiswahili cha wapi hiki Ndugu? au Wewe ni Mkurya Ndugu ili nisikushangae sana.
 
Uweredi kama ulivyoandika hapo juu katika Headline yako ndiyo Kiswahili cha wapi hiki Ndugu? au Wewe ni Mkurya Ndugu ili nisikushangae sana.
Hicho ni kiswahili sahihi kabisa ndugu, usifananishe na neno 'Ueledi'. 'uweredi' ni tofauti na 'ueledi'!
 
chama pendwa cha watanzania wote na Afrika kwa jumla, Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Eti chama pendwa. Kinapendwa na nani?

Mngetumia mabegi meusi kuiba kura kama kinapendwa?

Jiwe angepiga magoti kule Niombe kama kinapendwa?

Jiwe angezonewa kule Kagera na Bunda kama kinapendwa?

Mngetumia wasanii na malori kama kinapendwa?

Shubamiti!!
 
Eti chama pendwa. Kinapendwa na nani?

Mngetumia mabegi meusi kuiba kura kama kinapendwa?

Jiwe angepiga magoti kule Niombe kama kinapendwa?

Jiwe angezonewa kule Kagera na Bunda kama kinapendwa?

Mngetumia wasanii na malori kama kinapendwa?

Shubamiti!!
Ni nani aliye ndani ya ulimwengu huu na hata aliyeiumba na akaishi huko mbinguni alipendwa na wote?! Unanifurahisha sana, kwa jinsi unavyotafasiri tofauti neno kupendwa na jinsi unavyoshindwa kuelewa tofauti baina ya unyenyekevu na kupendwa 😂😂.

Kwa bahati nzuri zaidi uliyoyaandika ni misukumo ya kusimuliwa pasipokuwepo ushahidi, hili nalo linafurahisha 😂😂

CCM ni chama pendwa kwa watanzania zaidi ya 80% na waafrika wengi barani. Kinapendwa na watu wenye akili, wazalendo na wanaopenda kufanya kazi. Chama hiki haliwezi kupendwa na watu wavivu na wote wapendao kupokea kuliko kutoa, yaani kitonga. Ni kama Mungu vile, anapendwa na watu wote wanaopenda kufanya kazi na kutoa zaidi kuliko kupokea.

Endelea kujiuliza maswali ya ovyo ovyo, lakini tambua muda hautarudi nyuma tena Leo ni trh 02.01.2021....
 
Hicho ni kiswahili sahihi kabisa ndugu, usifananishe na neno 'Ueledi'. 'uweredi' ni tofauti na 'ueledi'!

Mkuu ule utumbo mrefu vile umeuleta humu ukitarajia kuna wa kuusoma? Utumbo wa vile husomwa tu na wanaccm waliopoteza ramani huko kwenye matawi yao.
 
Mkuu ule utumbo mrefu vile umeuleta humu ukitarajia kuna wa kuusoma? Utumbo wa vile husomwa tu na wanaccm waliopoteza ramani huko kwenye matawi yao.
Nafikiri wewe ulisomewa huo utumbo, maana vijana wa ufipa waliopoteza ramani hupenda zaidi kusomewa utumbo na sio kuusoma.
 
Siyo suala kuona aibu mkuu. Ubongo wa walumumba ni mdogo kama ncha ya sindano
Ninyi wenye ubongo mkubwa mfano wa simtank la kiboko la lita 3000. Mpaka hivi sasa mmefanya Jambo gani la kueleweka kwa watanzania?!
 
Back
Top Bottom