Mwaka 2015 umekuwa mbaya kwangu

Mwaka 2015 umekuwa mbaya kwangu

Hayo yote ni maisha ipo siku yataisha
 
Kwanza naanza kwa kukupa pole, nasema hivi pole sana.

Pili ondoa dhana uliyo nayo hivi sasa kwa kusema mwaka 2015 umekuwa mbaya kwako ni mapema sana huwezi jua ni jambo gani jema lilipo mbele yako.

Kumbuka kwenye maisha kila mmoja inatokea/inamtokea jambo zito na mengine yanakuwa mazito zaidi, ni kutofautiana tu lakini kila binaadam ana mazito yanayomtokea kiasi kwamba unaposikia la mwenzako unaona nafuu ya wewe. Ni changamoto tu za kimaisha.

Muhimu kama hivyo upo salama(mzima wa afya mshukuru sana Mungu wako).

Ondoa moyo na mawazo ya wasiwasi ili uweze kuishinda mitihani ya hapa na pale.

Kwa yangu machache na ya wengine watakaonifuata nina uhakika utakuwa umepata ufunuo kiasi fulani.

Kila la kheri
 
Hayo yote ni maisha ipo siku yataisha

Kweli kabisa Mkuu, vumilia sisi binadamu ndivyo tulivyo na kuna changamoto kubwa zaidi zinakusubiri zaidi ya hiyo. Maisha ni kujifunza jinsi ya kukabili changamoto kila zinapojitokeza na nyingi huwa zinakuja bila kutegemea. You have to be big than your problems...Mweleze ukweli wote na mpe plan ya jinsi utakavyomlipa ikiwezekana muende wote kwa Mwenyekiti wa serikali za mitaa au Polisi kama unaona imekuwa kero na utamlipia kwa kupitia huko. Usikubali opportunity uliyonayo ya shule ikakupita na ukachanganyikiwa kwa vitu vidogo kama hivyo...more big challenge are coming your way.....BUT yoou are bigger than those problems...You are strong my friend...Munngu yupo nawe....Ndio maisha....
 
cha kufanya kaka achana nae mazima... muombe mungu akuepushe na mabalaa hiyo ni mitihani tu.. usikate tamaa ndio maisha haya kila jambo linalokukuta unapaswa kumshukuru mungu.., mazuri yote yanatoka kwake na mabaya pia yanatoka kwake....
huyo mawanamama hakufai kata mawasiliano nae hata akirudi kuomba msamaha potezea...
bado mwaka ni mchanga kabisa "after a hurricane comes a rainbow"
 
10906144_10155085458160584_5264015514914923840_n.jpg



Kunawakati unakua na matatizo mpaka unasema "nimemkosea nini Mungu?" Ushukuru sana umejua kuwa huyu mwanamke hakufai mapema.
Be strong and stay focused.
 
Habarini wana jamvi
hongereni sana kwa kazi ya kuelimishana na kushauriana ama hakika kwa jukwaa hili linakuwa faraja sana kwetu sisi sote.
Kuna wakati unaweza jilaumu kwanini una maisha ya ajabu ajabu na mara nyingine unahisi ni laana hata kufikia kumkufuru Mungu hasa unapoona mfululizo wa mambo mabaya kukuzonga.
mnamo trh 27/12 laivu nilitamkiwa na aliyekuwa mpenzi wangu/mchumba kuwa hataki tena mahusiano nami nilimjibu sawa kwa sababu najua huwa anakuwa na maamuzi kama hayo mara kwa mara na anapogundua kuwa ana makosa hurudi na huwa namsikiliza na kusolve tena upya yapata kama mara nne hivi ila hii ya tano imekuwa kweli sasa naamini na sina budi kukubaliana na mawazo yake, najua ana madhaifu makubwa sana na ukizingatia yeye ni 28 by age na mi pia ni 28 kwa hali ya kawaida yeye umri umesogea sana hivyo nilitaka nifanye taratibu za mahari mwezi wa 12 mwka huu ili mwanzo tuu wa mwaka 2016 niweze kumuoa japo ndoto imefia mbali sasa naamini. jambo zuri kwa mwaka 2014 ni mimi kupata chuo cha afya kujiendeleza kimasomo japo nimeajiriwa kwenye taasisi ya gvt mwaka wa tatu 3 sasa tatizo hapa ni moja aliniongezea pesa kwaajili ya kuongezea ada ila sasa najuta sana kusimangwa na mwanamke ambaye pengine angekuwa mke wangu kunidharau kiasi hiki kisa laki 4 nne tuu mpk kuniita maskini, unadhiki, mtoto wa uswazi, nikamuuliza laki nne tuu ndio yamekuwa hayo yote basi nisamehe nakurudishia pesa zako basi nilipopata tuu salary nilimpa kiasi kidogo sasa leo kaniamulia mpk nimekosa amani moyoni mwangu nahitaji ushauri wenu wanajamvi si kwamba siwezi kumpa pesa yake maana salary tuu napata zaidi ya laki 7 kwa mwezi ni mambo ya chuo na kodi ya nyumba ndio yameingilia tuu. Haikuishia hapo tarehe 1 kuamkia 2 nilivamiwa na wezi usiku wa saa nane 8 walinikata panga mkononi na kuiba laptop iliyokuwa na notes za chuo muhimbili pia na kuiba tv yangu flat screen 21" je kwa maelezo hayo si inadhihirisha kuwa nimeuanza mwaka vibaya? nikitegemea yeye kwa tukio hilo angekua faraja kubwa kwangu matokeo yake alionekana kufurahia sana jambo hilo na kuniambia alimuomba sana Mungu na huenda ni jibu au pigo toka kwa Mungu nilimjibu nashukuru sana Mungu huyu huyu kaniokoa pengine ningeuawa ahsante Mungu kwa hili
WANAJAMVI KWA HAYO YOTE SASA HIVI NAISHI SINA AMANI KABISA MOYONI NASHINDWA KUSOMA NA END OF SEMESTER NI MWEZI UJAO. NAHITAJI USHAURI WENU WA KUNITIA MOYO NAJUA KUNA WENGI ITAWAGUSA KWA NAMNA MOJA NA WENGINE WATA ANDIKA WAJUAVYO ILA YOTE NIMEUMBWA KUYAPOKEA KWA WAKATI HUU NILIONAO AHSANTENI SANA KUNISIKILIZA GODBLESS U ALL
Pole sana brother. Hayo yote ni majaribu na yatapita tu. Shukuru kwa kuwa na afya njema. Usisahau kuwa mojawapo ya chanzo cha magonjwa ya moyo kwa wanaume siku hizi ni wanawake. Kuwa makini na viumbe hawa. Ni pasua kichwa mno.Waone tu wanatembea barabarani usiguse utajuta. NDIO MAANA MKE WANGU SASA HIVI NI BIA hata nikichelewa kurudi nyumbani haniulizi na nikienda baa namkuta hajatumiwa na mtu mwingine yeyote.
 
Kwanza kabisa jambo msingi la kumshukuru Mungu ni kukuonyesha rangi halisi ya huyo mtarajiwa wako mapema kabisa....
Pili matatizo katika maisha ni jambo la kawaida sana hata sisi hapa JF kila mmoja ana matatizo yake...na kila mmoja akiolodhesha mlolongo wa matatizo yake unaweza ukazimia kwa mshangao...lakini tunayasolve yale ambayo yanauwezekano wa kutatuliwa na yale yaliyokuwa sugu tunayaacha kama yalivyo na kuyapa kisogo na kufungua ukurasa mpya....huku tukitabasamu.....jambo la msingi ni kuvumilia na kujaribu kuyasahau.....kwani kama kutokea ndio yameshatokea.....
Bado una nafasi ya kuyafurahia maisha....amka uishi maisha yako....
 
DUh! Mkuu pole sana, Usifike kwenye laana wala adhabu kwa sababu ya maombi maovu ya mtu kwa sababu
kama Mungu akiamua hivyo tusingeishi
Find her money and Ignore her (asijekukuharibia mwaka).

Pia mwaka is just an amount of time God has granted us just like any second u live
hauna any evil implication on your life
 
Mungu akikupa mzigo wa kubebea hukupatia na "mabega" ya kuubebea. Kaa chini na upage mikakati ya jinsi ya kulipa deni na kujiandaa na mitihani. Mungu ni mwema atakutangulia.
 
Hayo ya kawaida wala usife moyo ila malengo yako yawe pale pale yaani kama ulitaka mwakani uoe fanya hivyo ili ajue hata bila yeye maisha yanaendelea kama kawaida ila kama utaahirisha utajidhoofisha mwenyewe na kuona amekurudisha nyuma, unachotakiwa ujue hakuwa wako ila alikuwa amejiegesha ndo maana umesema sio mara ya kwanza kukufanyia hivyo, cha msingi songa mbele usigeuke nyuma ni hayo tu
 
Kweli kabisa Mkuu, vumilia sisi binadamu ndivyo tulivyo na kuna changamoto kubwa zaidi zinakusubiri zaidi ya hiyo. Maisha ni kujifunza jinsi ya kukabili changamoto kila zinapojitokeza na nyingi huwa zinakuja bila kutegemea. You have to be big than your problems...Mweleze ukweli wote na mpe plan ya jinsi utakavyomlipa ikiwezekana muende wote kwa Mwenyekiti wa serikali za mitaa au Polisi kama unaona imekuwa kero na utamlipia kwa kupitia huko. Usikubali opportunity uliyonayo ya shule ikakupita na ukachanganyikiwa kwa vitu vidogo kama hivyo...more big challenge are coming your way.....BUT yoou are bigger than those problems...You are strong my friend...Munngu yupo nawe....Ndio maisha....

thanx much nyamchele your comment imenifanya kujihisi ninanguvu sasa ahsante sana nimesoma mpk machozi yamenilengalenga but i appreciate u much
 
Hayo ya kawaida wala usife moyo ila malengo yako yawe pale pale yaani kama ulitaka mwakani uoe fanya hivyo ili ajue hata bila yeye maisha yanaendelea kama kawaida ila kama utaahirisha utajidhoofisha mwenyewe na kuona amekurudisha nyuma, unachotakiwa ujue hakuwa wako ila alikuwa amejiegesha ndo maana umesema sio mara ya kwanza kukufanyia hivyo, cha msingi songa mbele usigeuke nyuma ni hayo tu

mmmh!!! utamfanya afanye maamuzi atakayoyajutia mbeleni eti kisa tu anamkomoa mwafulani, hakuna rehesal kwenye maisha aisee, ye etulie tu na amuombe sana Mungu na atampa tu wa kwake kwa wakati aliopanga yeye,huwezi jua kakuepushia balaa gani kwa kuachwa na huyo binti, cha msingi sasa afocus zaidi ktk masomo yake na malengo mengine makubwa zaidi, maisha lazima yaendelee, kuanguka sio mwisho wa safari, inuka jikung'ute vumbi na useme 'am not a looser', binadamu akifunga mlango mmoja Mungu anakufungulia mwingine ulio bora zaidi, aliona unaliweza hilo ndio maana akaruhusu ulipitie, usikate tamaa your stronger than your fears!
 
Kwanza pole sana,nadhani ni jambo jema hili Mungu kakufunulia mapema Sana kuwa ni mtu wa aina gani,we songa mbele and don stress yoself
 
Kwanza pole sana,nadhani ni jambo jema hili Mungu kakufunulia mapema Sana kuwa ni mtu wa aina gani,we songa mbele and don stress yoself

thanx much nashukuru kwa ushauri wako mzuri kwangu
 
mmmh!!! utamfanya afanye maamuzi atakayoyajutia mbeleni eti kisa tu anamkomoa mwafulani, hakuna rehesal kwenye maisha aisee, ye etulie tu na amuombe sana Mungu na atampa tu wa kwake kwa wakati aliopanga yeye,huwezi jua kakuepushia balaa gani kwa kuachwa na huyo binti, cha msingi sasa afocus zaidi ktk masomo yake na malengo mengine makubwa zaidi, maisha lazima yaendelee, kuanguka sio mwisho wa safari, inuka jikung'ute vumbi na useme 'am not a looser', binadamu akifunga mlango mmoja Mungu anakufungulia mwingine ulio bora zaidi, aliona unaliweza hilo ndio maana akaruhusu ulipitie, usikate tamaa your stronger than your fears!


ahsante sana nashukuru kwa hilo pia ni wazo jema na kweli sasa natengeneza na Mungu pekee ndie atanisafirisha salama katika safari hii pili sasa nimeamua kuangalia masomo maana nimetetereka lakini nimegundua hasara ni yangu nimetumia muda mwingi sana hata kumshauri jinsi ya kujiajiri hata sasa anakaribia kufungua duka la dawa maeneo ya bunju nilijitahidi sana kumsaidia njia kimawazo kumtia moyo ajiamini hata sasa kafikia sehemu nzuri sana ila sijawahi kumkatisha tamaa hata mara moja je kulikuwa na ubaya kwangu hana professional yeyote ya medicine ila nimemuaminisha anaweza mi sinilikuwa nyuma ya program atakapokwama sio!!
 
Hayo ya kawaida wala usife moyo ila malengo yako yawe pale pale yaani kama ulitaka mwakani uoe fanya hivyo ili ajue hata bila yeye maisha yanaendelea kama kawaida ila kama utaahirisha utajidhoofisha mwenyewe na kuona amekurudisha nyuma, unachotakiwa ujue hakuwa wako ila alikuwa amejiegesha ndo maana umesema sio mara ya kwanza kukufanyia hivyo, cha msingi songa mbele usigeuke nyuma ni hayo tu

ahsante sana daudi nitayafanyia kazi pia brother thanx Much much
 
Back
Top Bottom