Bwana DAVIES nianze kwa kukupa pole kwa yaliyo kukuta kwani kupatwa na mambo mabaya yenye msukosuko huwa inachanganya sana na kuvuruga mipangilio mingi ya mbeleni uliyo itarajia.
Nikirudi katika Kisa na Mkasa cha Inshu yako .... kuna vitu vichache vinanipa maswali ya kuhitaji majibu ya ziadi kabla ya Mie kupiga dua kukuombea wepesi wakati labda kuna sehem ina mushkeri ili tuirekebishe kwanza kabla ya kukabidhi kwa Mola yatakayo bakia kwa uwezo wake ayakamilishe.
Maswali:
1. Huyo Mtendwa wako mmedumu nae kwa muda gani kabla ya kuvunja ndoto yenu?
2. Nini kilitokea huko nyima hadi mara kwa mara akawa anatishia kuzuia shilingi?
3. Tumesikia masimulizi yako ambayo kwa sehem kubwa yamesheheni ubaya wa Mtendwa wako, Je unaweza kutuonjesha walau kidogo episodi za kuteleza kwako pia ili tujue tunaanzia wapi kuziba kwa mapema kwaajili ya msimu ujao? Japo ni ngumu mtu kuandika mabaya yake ubaoni ili wengine wasome - jikaze kiume belezee tutakuelewa.
4. Ingawa mazoea nayo hutuponza....ilikuaje ukasema "sawa" alipokwambia muachane kwa mara ya mwisho?? Unakubali vipi kirahisi namna hiyo ilhali ukijua fika ubavu wako umeoza kwake?? Kwanini hukujitetea braza?? ni kiburi cha Kiume au?? Hujui kuwa Raha ya Mapenzi ni kubembelezana hata kama ni kwa dizaini ya "Waziri wa Gesi"??
5. Bidada anafanya kazi?? au mambo ya familia bora??
6. Unaweza kutuchungulisha Elimu yake na kabira yake japo kwa mbaaaali??....maana tumesikia sifa za kabira fulani leo kutoka pande za mgombani tukachanganyiwa kwani baadhi yetu tuliisha karibisha wawekezaji majumbani mwetu....hepu pekuapekua kwy nyuzi humu jamvini ufananishe isije kua ndio hao hao.
7. Kwa uzoefu wangu usio raxmi....wadada hubadirika na kuwa zaidi ya shetani pale anapokufuma laivu na mtu wa karibu yake sana ukigegeda...hilo huwa halifutiki maishani mwao na ingewezekana wangeomba tuwe tunakufa moja kwa moja baada ya mechi ili wasituone tena maishani mwao...Kaka, uligonga shosti wake?? au ulifuata nyayo za mume wa mtumishi wa bwana anayetumia vinubi na zumali??
8. Mwisho, ikipatikana kamati ya maridhiano na kushughulikia kero za muungano?? upo tayali kurudi kundini?? kwa kidhungu wanasema - Is ur heart still calling "baby come back" ??
Naomba andika jibu la kila swali kwenye karatasi. Ukimaliza najua itakua ni home work tosha kwa leo ulale, ukiamka asubuhi...soma majibu uliyoandika then fanya correction kwa sehem ulizokosea...but be honest unapo andika hayo majibu na uwe mkweli kabisa kabisa maana Mungu anakuona.
Majibu yako usiyatume humu jamvini ila yaweke sehem nzuri na asione mtu yeyote...rudia kuyasoma kila mara mawazo juu yake yanapokujia na kukuondoa katika reli ya unachokifanya....
Nakuahidi...baada ya wiki na kuendelea...utaona njia sahihi unayotakiwa kuifuata pasipo kumuuliza mtu. Rekebisha majibu kwa kupunguza au kuongeza kama ilivyokua ktk BMK isipokua tofauti yao na yako...wewe uwe mkweli kwa nafsi yako.
Karibu tena ukitendwa upya...jf iko live muda wowote kwaajili yako.