Mwaka 2015 ulipewa miaka mitano na kwa kweli tumeona maajabu mengi.

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
FB_IMG_1599297243416.jpg


Mwaka 2015 ulipewa miaka mitano na kwa kweli tumeona maajabu mengi.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu watumishi wa umma wakasota miaka mitano bila kupata nyongeza ya mshahara ambayo ni haki yao kisheria. Gharama za maisha zikapanda lakini kipato cha watumishi kikabaki kilekile. MAAJABU.

Kwa mara ya kwanza tukashuhudia wahitimu wa kada muhimu kama udaktari na ualimu wakisota mtaani bila ajira lakini hospitali hazina madaktari na shule hazina waalimu. MAAJABU.

Tukashuhudia watu wa Kimara wakivunjiwa nyumba bila kulipwa fidia kwa kutumia sheria ya kikoloni ya mwaka 1932. Wakaenda mahakamani, na mahakama ikaweka zuio, lakini amri ya mahakama ikapuzwa na nyumba zikavunjwa. MAAJABU.

Tukashuhudia bunge likifanyiwa "shooting" kama bongo movie. Hotuba za wabunge zinakua censored kwanza. Walioongea maneno makali wanakatwa, walioipamba serikali wanaenda hewani. Bunge likapoteza focus na kuanza kuipongeza serikali wakati kazi ya bunge ni kuisimamia serikali. MAAJABU.

Tukashuhudia RC akivamia studio na mitutu ya bunduki kulazimisha "clip yake ya umbea" irushwe hewani. Chombo husika kikaamua kuzingatia maadili na kukataa kurusha clip hiyo. Waandishi wakavamiwa na kutishwa. Waziri aliyeunda Kamati ya kuchunguza suala hilo akafurushwa. MAAJABU.

Kwa mara ya kwanza mifuko ya hifadhi ya jamii ikafuta fao la kujitoa. Watumishi wa mikataba na wa muda mfupi wakaambiwa hadi miaka 60. Mtu mwenye akiba ya 5M na kwa sasa ana maika 25 unamwambia hadi afikishe miaka 60? Yani miaka 35 ijayo? Akifikisha miaka 60 hiyo 5M si itakua ya kununulia mkate tu? MAAJABU.

Kwa mara ya kwanza tukashuhudia Hakimu aliyekua kwenye likizo ya kustaafu akiteuliwa kuwa Jaji wa mahakama kuu. MAAJABU.

Kwa mara ya kwanza tukashuhudia mbunge akipigwa risasi kwenye makazi yenye CCTV camera. Lissu akasema camera ziliondolewa baada ya tukio. Hakuna mshukiwa hata mmoja aliyekamatwa hadi sasa. MAAJABU.

Tukashuhudia mikutano ya siasa ikipigwa marufuku kinyume na katiba na sheria za nchi. Viongozi wa upinzani walipofanya vikao vya ndani walikamatwa lakini CCM walifanya mikutano ya hadhara na vikao bila bughudha. MAAJABU.

Binafsi naona maajabu yametosha baba. Hatutaki maajabu mengine.!
 
Mpe credit basi mwandishi wa andiko hili bwana Malisa gj sio vibaya
 
Back
Top Bottom