Wakuu, huu mwaka umevunja rekodi kuwa mbaya kwa dunia nzima, ni mwaka ambao tumeshuhudia kikundi kikatili cha ISIS kikifanya mauaji na kuwa kikundi chenye uwezo mkubwa kiuchumi ie US 2B,ni mwaka ambao ndege yenye abiria imepotelea kusikojulikana mpaka leo, ni mwaka ambao watoto wa kike wa Nigeria wamepotea na hawajulikani walipo japo wanafahamika waliowachukua, ni mwaka ambao Boko Haram wameuwa watu wengi na kupata nguvu zaidi, ni mwaka ambao Alshabab wamewapiga wakenya kwa ukatili wa hali ya juu, ni mwaka ambao Israel ilirushuwa makombora elfu 3 ndani ya anga lake, ni mwaka ambao vita kati ya Israel na Palestina imepelekea vifo vya wapalestini zaidi ya elfu mbili, ni mwaka ambao USA imeshuhudia dalili za mgawanyiko kati ya black and white, ni mwaka ambao vita baridi kati ya Rusia na Western vimekua juu sana, ni mwaka ambao dunia imeshtushwa na sakata la Tegeta Escrow Tanzania, ni mwaka ambao tatizo la ajira limekua kubwa zaidi, ni mwaka ambao tumeshuhudia Ebola ikisababisha vifo na yatima ktk West Afrika. Wadau tuendeleze zaidi matukio yaliyovunja rekodi na kufanya kua mwaka wa kipekee.... Karibuni!