Polycarp Mdemu
Senior Member
- Jun 2, 2019
- 165
- 209
Mwaka 1869 ulifunguliwa Mfereji mashuhuri wa Suez (Suez Canal), Ni mfereji ambao ulitengenezwa kwa Nguvu ya Binadamu ili Kufupisha safari ya Kutoka Bara la Ulaya Mpaka Asia.
Kabla ya kuwepo kwa mfereji huu Safari ya kutoka Ulaya, kwa mfano kutoka Bandari kubwa Ulaya iitwayo Rotterdam huko Uholanzi mpaka Dubai ni Kilomita 20,900 yaani Meli zilikua zikitembea Siku hadi 24.
Lakini ulipojengwa Mfereji huu, Meli zinatembea kilometa 12,000 kwa siku 10 pekee, Safari imekua rahisi sana, na idadi ya meli kutoka ulaya ziliongezeka, Kwa mwaka meli takribani meli 15,000 hupita mferejini hapo.
Mfereji huu ulianza Kujengwa mwaka 1859 na kampuni la Suez Canal Company na kumalizika mwaka 1869 aliyeanzisha Kampuni hilo ni bwana Ferdinand de Lesseps, Mfereji una Urefu wa 193.30 Kilomita, na Upana mpaka Mita 300.
Meli ya kwanza ilipitia mfereji mpya tarehe 17 Februari 1867 iliitwa El Mahrousa
Mfereji huu japo hapo mwanzo ulikuwa ukimilikiwa na Serikali ya Misri lakini Ni wazi waliokua wakiuendesha ni Shareholders kutoka nchi za Ulaya, Hasa Uingereza na Ufaransa.
Mwaka 1956 raisi wa Misri wakati huo Gamal Abdel Nasser alitaifisha mfereji huo ambao ulileta Vita iliyoitwa Suez Crisis.
Mawazo ya kupata mfereji huu mwanzo yalikua yakionekana hayawezekani, Hivyo Mafanikio ya mfereji wa Suez yalihamasisha ujenzi wa mwanzo ya Mfereji wa Panama.
KATIKA HISTORIA Wakati wa Vita vya Siku Sita vya Juni 1967(Six days War) kati ya Misri na Israeli, Mfereji wa Suez ulifungwa na serikali ya Misri na kuzuia kila upande kwa meli za kivita zilizovamia mfereji, Hivyo hakuna meli iliyoruhusiwa Kuingia ama kutoka.
Wakati wa kufungwa, meli 15 za kimataifa zilijikuta zimebaki katikati ya mfereji kwenye Ziwa Kuu la Bitter. Walibaki wakiwa wamekwama katikati ya mfereji katikati ya maji kwa miaka nane, wenyeji waliwaita "Yellow fleet" kwa sababu ya mchanga wa jangwa ambao ulifunika meli zao.
Watu waliokuwamo ndani ya meli hasa wahudumu, wengi walizunguka ndani na nje ya meli zilizokwama kwa kazi ya miezi 3, lakini wengine walipoteza mda kwa kuunda jumuiya yao na kuandaa hafla za michezo na kijamii ili maisha yaendelee ndani ya Mfereji licha ya Kukwama
Kadiri miaka ilivyoenda, meli zilitengeneza stempu zake na mfumo wa ndani kwa ndani wa biashara, Yaani maisha yakawa yanaendelea ili kujihisi wako nyumbani.
Meli 15 zilizokwama hatimaye ziliruhusiwa kuondoka kwenye mfereji huo mwaka wa 1975. Kufikia wakati huo, ni meli mbili tu kati ya meli 15 zilikuwa bado zinafaa kusafiri baharini kwa uwezo wake zenyewe, Nyingine zilikuwa zimekufa, Zilihitaji kuvutwa.