Mwajiri hataki kuniongeza mshahara, nifanyeje?

Mwajiri hataki kuniongeza mshahara, nifanyeje?

digodigo

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2010
Posts
315
Reaction score
256
Wakuu naombeni ushauri,

Kuna mdosi ameniajiri kwenye kampuni yake kwa miaka kadhaa na kama mjuavyo hali ya maisha kadiri siku zinavyoenda inakuwa ngumu mwelekeo siujui na kuacha siwezi ni hivi majuzi tu namuuliza japo anifikirie kuniongeza kidogo mshahara niweze kujikimu, jibu alilonipa liliniacha hoi yaani anasema miundombinu ya kampuni haiko sawa yaani afanye marekebisho ya umeme,maji na vyoo kwanza ndipo atanifikiria kitu ambacho kimsingi sidhani kama kwangu mimi kina uhusiano kwani si mara ya kwanza kumuomba na kila mara hunijibu kwanza afanye kile ndipo anifikirie.

Yaani ni danadana na visingizio kibao utekelezaji ziro na sasa nimeshamstukia kuwa hana nia ya dhati.

Je, kisheria hili limekaa vipi kwenye mkataba hakukuwa na kipengele kisemacho mshahara uendane na masuala anayoyataja

Naombeni ushauri.
 
Ngoja waje watumishi wa umma maana na wao wanalalamikia kuongezewa mishahara
 
Mkuu kwan mkataba wenu unasemaje?? Kuna kipengele cha kupanda kwa mshahara etc??
 
Mkuu tulikubaliana kila mwaka atatoa nyongeza na mimi nikikumbusha juu ya hilo basi ni visingizio kibao hadi kero.
Mkuu katika hiyo entity kuna chama chochote cha wafanyakazi? je, na wewe ni mwanachama wa hicho chama? je, kwenye mkataba mlikubaliana kwamba asipoongeza kiwango cha mshahara ni hatua gani utapitia kudai haki yako? kuna kitu kinaitwa Commission for mediation and arbitration unaweza kupeleka madai yako Kama unajua ni dispute of interest (mgogoro wa maslahi). kikubwa mtafute mwanasheria atakupa mwongozo wa nini cha kufanya
 
Usimwombe akuongezee mshahara kwa mdomo.
Mwandikie barua na umpe sababu za kutaka kuongezewa mshahara.
 
Wakuu naombeni ushauri,

Kuna mdosi ameniajiri kwenye kampuni yake kwa miaka kadhaa na kama mjuavyo hali ya maisha kadiri siku zinavyoenda inakuwa ngumu mwelekeo siujui na kuacha siwezi ni hivi majuzi tu namuuliza japo anifikirie kuniongeza kidogo mshahara niweze kujikimu, jibu alilonipa liliniacha hoi yaani anasema miundombinu ya kampuni haiko sawa yaani afanye marekebisho ya umeme,maji na vyoo kwanza ndipo atanifikiria kitu ambacho kimsingi sidhani kama kwangu mimi kina uhusiano kwani si mara ya kwanza kumuomba na kila mara hunijibu kwanza afanye kile ndipo anifikirie.

Yaani ni danadana na visingizio kibao utekelezaji ziro na sasa nimeshamstukia kuwa hana nia ya dhati.

Je, kisheria hili limekaa vipi kwenye mkataba hakukuwa na kipengele kisemacho mshahara uendane na masuala anayoyataja

Naombeni ushauri.
Achana na hiyo kazi. Jipe kazi nyingine ya kutafuta kibarua kingine.
 
Kwa nini ufanye kazi isiyokuwezesha kujikimu?? Achana na hiyo kazi na utafute itayokuwezesha kujikimu.
Wewe mwenyewe unakiri kwamba hali imekuwa mbaya, unadhani kwa mdosi ni nzuri kukuongeza wewe mshahara??
Tuvumiliane katika hiki kipindi kigumu, tulilikoroga na acha tulinywe kwa pamoja.
Na ukiendelea kumsumbua kuna siku utaleta uzi wa kupunguzwa kazini kwa sababu zitakazosemekana ni hali mbaya ya kiuchumi ya kampuni.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom