Mwadhamu Polycarp Pengo: Serikali mbili zinatosha

Mwadhamu Polycarp Pengo: Serikali mbili zinatosha

Pengo huenda anatumika na ccm kama ilivyo kwa mufti. Sasa tusubiri msimamo wa mufti, huenda ukawa sawa na wa pengo! Chezea maccm wewe?
 
Mkuu, Kardinali ni cheo siyo jina, ni cheo cha mkuu wa maaskofu nchi nzima na kiongozi mkuu wa kanisa katoliki nchi nzima na ndiyo yeye na makardinali wenzake dunia nzima hukutana Vatican kumchagua kiongozi wao wa dunia (Baba mtakatifu).

Mkuu kama haujui uwe unauliza. Caldinar Pengo si mkuu wa wakatoliki Tanzania bali ni askofu mkuu wa jimbo la Dar es salaam. Kule Vatican yeye ni askofu kama alivyo askofu wa Mwanza,Iringa, Kagera nk. Ila ana cheo cha u kardinali kwa maana kwamba ni mjumbe wa vikao vya Pope. Kila Askofu wa kila jimbo ana report moja kwa moja Vatican na si kwa Kardinal Pengo. Kuna nchi zina ma kardinal zaidi ya wawili, ina maana kwa tafsiri yako nchi hizo zina viongozi wakuu wa katoliki zaidi ya wawili! Amka!
 
Ni kweli baadhi ya wanachi wanataka Serikali 3 lakini sio wote; hata Ripoti ya Warioba inaonesha ni asilimia ngapi wanaotaka Serikali 3, 2, 1, na hata Muungano wa Mkataba. Pengo, kama mwananchi, atakuwa katika hao wachache wanaotaka Serikali 2; ni haki yake alimradi haongei kwa niaba ya Kanisa na, in fact amefafanua vizuri, ni maoni yake binafsi.
 
Pengo amedhihirisha ukereketwa wake kwa CCM na ku-confirm dhana inayolalamikiwa na Waislamu kuwa Serikali ya ccm inafuata sera ya mfumo Kristo.
Rasimu ya Katiba imetokana na mawazo ya wananchi yeye ni nani mpaka adharau matakwa yao? Mamlaka ya kuwasemea wananchi ameyatoa wapi?

Wakatoliki watanisamehe kwa hili, ila Mkuu wenu wa Kiroho amepotoka kuingilia na kutoa msimamo wa kisiasa!

Kufikia hapa naweza nikasema bila shaka yoyote kuwa Pengo ni mfuasi wa kambi ya Lowassa.
Kumbuka kipindi kile Lowassa amefukuzwa kazi kwa sababu ya ufisadi, baada ya muda Cardinal Pengo alimtembelea Lowassa nyumbani kwake na kuzindua kitabu cha mke wa Lowassa, Regina!!

Ni kweli baadhi ya wanachi wanataka Serikali 3 lakini sio wote; hata Ripoti ya Warioba inaonesha ni asilimia ngapi wanaotaka Serikali 3, 2, 1, na hata Muungano wa Mkataba. Pengo, kama mwananchi, atakuwa katika hao wachache wanaotaka Serikali 2; ni haki yake alimradi haongei kwa niaba ya Kanisa na, in fact amefafanua vizuri, ni maoni yake binafsi.
 
Pengo huenda anatumika na ccm kama ilivyo kwa mufti. Sasa tusubiri msimamo wa mufti, huenda ukawa sawa na wa pengo! Chezea maccm wewe?

we ndasu umeamua tu kujifyatua kichwani au,mbona mgumu sana kuelewa?
nakumbuka viboko vlikuwa vinatumika sana katika somo la hesabu ili kutengeneza uelewa kwa watoto
 
yanini uweke link, soma maelezo haya hapa chini;

A cardinal (Latin: sanctae romanae ecclesiae cardinalis) is a senior ecclesiastical official, an ecclesiastical prince, and usually an ordained bishop. The cardinals of the Roman Catholic Church are collectively known as the College of Cardinals. The duties of the cardinals include attending the meetings of the College and making themselves available individually or in groups to the pope as requested. Most have additional duties, such as leading a diocese or archdiocese or managing a department of the Roman Curia. A cardinal's other main function is electing the pope when the see becomes vacant. During the sede vacante, the period between a pope's death or resignation and the election of his successor, the day-to-day governance of the Church as a whole is in the hands of the College of Cardinals. The right to enter the conclave of cardinals where the pope is elected is limited to those who have not reached the age of 80 years by the day the vacancy occurs.

In 1059, the right of electing the pope was reserved to the principal clergy of Rome and the bishops of the seven suburbicarian sees. In the 12th century the practice of appointing ecclesiastics from outside Rome as cardinals began, with each of them assigned a church in Rome as his titular church or linked with one of the suburbicarian dioceses, while still being incardinated in a diocese other than that of Rome.[SUP][citation needed][/SUP]

The term cardinal at one time applied to any priest permanently assigned or incardinated to a church,[SUP][1][/SUP] or specifically to the senior priest of an important church, based on the Latin cardo (hinge), meaning "principal" or "chief". The term was applied in this sense as early as the ninth century to the priests of the tituli (parishes) of the diocese of Rome.[SUP][1][/SUP] The Church of England retains an instance of this origin of the title, which is held by the two senior members of the College of Minor Canons of St Paul's Cathedral.

Narudia tena Kardinali ni CHEO.

Maneno mhimu kwenye haya maelezo ni; senior, principal, chief. Sasa kama siyo kiongozi wa nchi nzima basi hata Papa siyo kiongozi wa dunia nzima na ingefaa umtaje sasa wewe kiongozi wa kanisa katoliki Tanzania ni nani.

Ni kweli ni senior ila sio kiongozi wa kanisa kwa nchi nzima. Hiko cheo amempa nani? Bishop au Arch Bishop ndio wanaongoza majimbo na wanaripoti moja kwa moja kwa Pope. Kwa maana hiyo basi Cardinal sio boss wao. Unless kwa Tanzania iwe tofauti. Ila mapadri wote boss wao ni askofu wa jimbo wanalo operate.
 
sasa hii ni nini!!???

Tulishawaachia akina warioba kazi, wakamaliza... na sasa tumewapa watu mia sita ukumbi wafanye upuuzi na maigizo, then huyu jamaa nae anakuja kivyake

where is the authorization matrix in the country, na Pengo anazungumziaje mamilioni ya wakatoliki ambao hawaungi mkono kauli yake??

HE LOST CREDIBILITY LONG AGO, AND HE SHOULD TRY TO KEEP THE SMALL RESPECT HE HAS TO HIMSELF, THIS IS A SILLY MISTAKE TO MAKE AND HE HAD NO REASON WHATSOEVER

SOMETIMES UKISHINDWA KUELEWA NAFASI YAKO, UNAISHIA KUWA KANJANJA TU KAMA KANJANJA WENGINE.... PENGO COULD AHVE MADE SOME ONE ELSE MAKE THOSE REMARKS

Kwa jinsi Pengo anavyojitetea kuwa hayo ni mawazo yake tu basi naona kuna siku pia atasema anapenda kuwe na mashoga waliohalalishwa Tanzania kwa mawazo yake na sio ya Kanisa katoliki!...anaweza huyu kwani anaonyesha kuwa anasahau kirahisi rahisi tu nafasi yake ktk jamii
 
Mkuu, Kardinali ni cheo siyo jina, ni cheo cha mkuu wa maaskofu nchi nzima na kiongozi mkuu wa kanisa katoliki nchi nzima na ndiyo yeye na makardinali wenzake dunia nzima hukutana Vatican kumchagua kiongozi wao wa dunia (Baba mtakatifu).

Mkuu umepotoka ngoja tukusaidie. Kanisa katoliki halina mkuu wake katika nchi bali kila askofu ana Mamlaka kamili ya Jimbo lake. Msemaji mkuu wa kanisa Katoliki anakuwa ni Rais wa Baraza la maaskofu Tanzania. Kwa maana hiyo raisi wa sasa ni Tarcisius Ngalalekumtwa wa Jimbo la Iringa, pengo akifika katika vikao vya baraza yy ni askofu kama maaskofu wengine na anakuwa anapaswa kumtii rais wa baraza.
 
mkuu unaonekana unajua mengi, labda ungetuelewesha kidogo, ni nini hasa kilichopo nyuma ya hii kauli ya pengo. kwani wananchi wanataka serikali 3 kwa mujibu wa tume ya warioba, na katiba ni ya wananchi, ni kwanini pengo anatumia cheo chake ndani ya mwanvuli wa usomi kuwaamulia waTz zaidi ya mil45 walioamua wawe na serikali 3?
Labda sielewi maana ya 'kuwaamulia', lakini nielewavyo mimi, Card. Pengo hajamuamulia mtu. Sasa kama Pengo 'amewaamulia' Watanzania kuwa na serikali mbili, Vyama vya CHADEMA na CUF serikali tatu, Taasisi ya Utafiti ya Vyuo Vikuu vya Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAURP) serikali moja, na baadhi ya Wapemba serikali nne, sasa unadhani maamuzi gani yatatekelezwa? Nijuavyo, hayo ni maoni, na Pengo ametoa maoni yake, maamuzi ndio kwanza yanaandaliwa kanuni huko Dodoma, bado hayajafanyika! Kwa hiyo Mkuu Abunuas, sio kweli kwamba Card. Pengo amewaamulia watanzania milioni 45 !!!
 
Kiongozi wetu wa kiroho hawezi kutuamlia masuala ya nchi kwa hisia zake na uswahiba wake kwa maccm, akichoka achie wengine huyu mzee vipi huyu ndiye anatuletea hata kelele zisizokuwa na maana ndani ya kanisa
Kauli rasmi ya kanisa katoliki hutolewa na Rais wa Baraza la maaskofu.Pengo ni Askofu wa jimbo kuu la Dar es salaam,Rais wa Baraza la maaskofu katoliki ni Tarsisius Ngalalekumtwa Askofu wa jimbo la Iringa,Ingawa naye rais wa baraza anaweza kuongea kama binafsi au kwa niaba ya baraza,akizungumza kwa niaba ya baraza hapo ndio unakuwa msimamo wa kanisa katoliki.
Hivyo basi kauli ya Pengo sio msimamo wa wakatoliki,maana yeye si msemaji wake,msemaji wake ni Rais wa hilo Baraza!
 
Labda sielewi maana ya 'kuwaamulia', lakini nielewavyo mimi, Card. Pengo hajamuamulia mtu. Sasa kama Pengo 'amewaamulia' Watanzania kuwa na serikali mbili, Vyama vya CHADEMA na CUF serikali tatu, Taasisi ya Utafiti ya Vyuo Vikuu vya Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAURP) serikali moja, na baadhi ya Wapemba serikali nne, sasa unadhani maamuzi gani yatatekelezwa? Nijuavyo, hayo ni maoni, na Pengo ametoa maoni yake, maamuzi ndio kwanza yanaandaliwa kanuni huko Dodoma, bado hayajafanyika! Kwa hiyo Mkuu Abunuas, sio kweli kwamba Card. Pengo amewaamulia watanzania milioni 45 !!!
sawa mkuu.
 
sawa, umeeleweka.
Ni kweli baadhi ya wanachi wanataka Serikali 3 lakini sio wote; hata Ripoti ya Warioba inaonesha ni asilimia ngapi wanaotaka Serikali 3, 2, 1, na hata Muungano wa Mkataba. Pengo, kama mwananchi, atakuwa katika hao wachache wanaotaka Serikali 2; ni haki yake alimradi haongei kwa niaba ya Kanisa na, in fact amefafanua vizuri, ni maoni yake binafsi.
 
Yaani hapa ni sawa na timu flani itoe mchezaji mmoja kuichezea timu ya taifa, Hii haina maana kwamba huyo mchezaji atakua boss ktk timu ile aliyotoka, ndivyo ilivyo kwa Pengo
 
Mnamsema bure kwa kuwa hamjamuelewa. Amesema Kanisa huwa halitoi msimamo kuwaelekeza Wakatoliki nini cha kuchagua, labda huo msimamo uwe unahusu masuala ya IMANI au MAADILI. Hata inapolazimika kutoa msimamo wa KANISA, ni Baraza la Maaskofu (TEC) pekee linaweza kutoa msimamo wa KANISA KATOLIKI kupitia Rais wake (ambaye sio yeye Kard. Pengo). Maoni mengine yanaweza yakatolewa na mtu binafsi (kama yeye Pengo) au vyombo vya kanisa (kama Baraza la Walei), na hailazimishi kila Mkatoliki kuifuata kwani haina uhusianao wa moja kwa moja na IMANI au MAADILI.

Tuwe makini tunapowanukuu viongozi wetu, hasa wanapokuwa wasomi kama Pengo, kwa maana lugha ya kisomi inaweza kumfanya mtu asimuelewe halafu akakimbilia kuanzisha thread humu kama alivyofanya huyu tpmazembe

hapana Pengo katika mwananchi kaeleza wasiwasi wake ni ulinzi na usalama. pia pengo kasema zanzibar wanaweza kubadili makosa yao katika katiba yao ya 2010, ukweli ni kwamba haiyonekani dhamira ya dhati kwa zanzibar kubadili na kujiita sio nchi naomba tuongee kisomi pia.wazanzibar hawana nia ya kubadili katiba yao juzi umesikia wawakilishi wanaongea unafiki pale dodoma kuwa spika kificho mapendekezo yake kwenye tume ni yake binafs angali tume ya uongoz ina zaidi ya wana ccm 6 akiwemo kificho hiyo yote ni kwamba znz hawako tayari kutojiita nchi. sasa what next? madai hayo tangu mwaka 2012 yanasemwa znz kujiita nchi makosa sasa mbona baraza na ccm hawajaambana kubadili?
 
Serekal 3 haziepukiki jamani naka nimzigo mbona ma shangingi yanayo nunuliwa kila siku sio mzigo?
 
Mkuu umepotoka ngoja tukusaidie.
Mkuu, katika hili jisaidie mwenyewe huwezi kunisaidia mimi.

Kanisa katoliki halina mkuu wake katika nchi bali kila askofu ana Mamlaka kamili ya Jimbo lake.
Siyo kweli, lingekuwa halina mkuu katika nchi basi lingekuwa pia halina mkuu katika dunia. Ni kweli kila askofu ana mamlaka kamili lakini kuna mkuu wao.

Msemaji mkuu wa kanisa Katoliki anakuwa ni Rais wa Baraza la maaskofu Tanzania.
Kiongozi kuwa ni msemaji mkuu haina maana yeye ndiyo mkuu elewa hilo kwanza. mfano msemaji mkuu wa jeshi la polisi siyo ndiye IGP, Msemaji mkuu wa TFF siyo ndiye mwenyekiti wa TFF, kADHARIKA MSEMAJI MKUU WA CCM siyo ndiye mwenyekiti, uelewa wenu bado ni mdogo sana.

Kwa maana hiyo raisi wa sasa ni Tarcisius Ngalalekumtwa wa Jimbo la Iringa, pengo akifika katika vikao vya baraza yy ni askofu kama maaskofu wengine na anakuwa anapaswa kumtii rais wa baraza.
Rais wa baraza la maaskofu/Tanzania Episcope Conference (TEC) ni mwenyekiti wa huo mkutano/conference kama anavyokuwaga mwenyekiti wa bunge Jenista Mhagama lakini siyo kwamba yeye ndiye spika wa bunge. Yeye ni mwenyekiti tu NA SI KARDINALI, KARDINALI NI CHEO, NI MKUU WA KANISA KATOLIKI KATIKA NCHI, NDIYE HUKUTANA NA MAKARDINALI WENGINE DUNIA NZIMA KUMCHAGUA PAPA/KIONGOZI WA KANISA KATOLIKI DUNIANI.
 
Pengo amedhihirisha ukereketwa wake kwa CCM na ku-confirm dhana inayolalamikiwa na Waislamu kuwa Serikali ya ccm inafuata sera ya mfumo Kristo.
Rasimu ya Katiba imetokana na mawazo ya wananchi yeye ni nani mpaka adharau matakwa yao? Mamlaka ya kuwasemea wananchi ameyatoa wapi?

Wakatoliki watanisamehe kwa hili, ila Mkuu wenu wa Kiroho amepotoka kuingilia na kutoa msimamo wa kisiasa!

Kufikia hapa naweza nikasema bila shaka yoyote kuwa Pengo ni mfuasi wa kambi ya Lowassa.
Kumbuka kipindi kile Lowassa amefukuzwa kazi kwa sababu ya ufisadi, baada ya muda Cardinal Pengo alimtembelea Lowassa nyumbani kwake na kuzindua kitabu cha mke wa Lowassa, Regina!!

Jamani mtaelemishwa mpaka lini? pengo sio Mkuu wa kanisa katoliki tanzania bali ni mkuu wa kanisa katoliki jimbo la dar es salaam. mweneyekiti wa baraza la maaskofu labda ndiye tunaweza kumuita mkuu wa kanisa katoliki tanzania kwa sababu ndiye mweneyekiti wa maaskofu wote. Huu ni msismamo binafsi wa pengo sio wa kanisa katoliki.
 
Back
Top Bottom