Iyokopokomayoko
JF-Expert Member
- Sep 15, 2011
- 1,785
- 443
Mkuu Ikwete, naunga mkono hoja ya Iyokopokomayoko,kuwa Pengo ni Jina, Cardinali ni cheo!.Pasco.
Ahsante Pasco, kazi njema na mimi natoka sasa kwenye huu uzi.
Last edited by a moderator:
Mkuu Ikwete, naunga mkono hoja ya Iyokopokomayoko,kuwa Pengo ni Jina, Cardinali ni cheo!.Pasco.
Mkuu kama haujui uwe unauliza. Caldinar Pengo si mkuu wa wakatoliki Tanzania bali ni askofu mkuu wa jimbo la Dar es salaam. Kule Vatican yeye ni askofu kama alivyo askofu wa Mwanza,Iringa, Kagera nk. Ila ana cheo cha u kardinali kwa maana kwamba ni mjumbe wa vikao vya Pope. Kila Askofu wa kila jimbo ana report moja kwa moja Vatican na si kwa Kardinal Pengo. Kuna nchi zina ma kardinal zaidi ya wawili, ina maana kwa tafsiri yako nchi hizo zina viongozi wakuu wa katoliki zaidi ya wawili! Amka!
Mkuu, katika hili jisaidie mwenyewe huwezi kunisaidia mimi.
Siyo kweli, lingekuwa halina mkuu katika nchi basi lingekuwa pia halina mkuu katika dunia. Ni kweli kila askofu ana mamlaka kamili lakini kuna mkuu wao.
Kiongozi kuwa ni msemaji mkuu haina maana yeye ndiyo mkuu elewa hilo kwanza. mfano msemaji mkuu wa jeshi la polisi siyo ndiye IGP, Msemaji mkuu wa TFF siyo ndiye mwenyekiti wa TFF, kADHARIKA MSEMAJI MKUU WA CCM siyo ndiye mwenyekiti, uelewa wenu bado ni mdogo sana.
Rais wa baraza la maaskofu/Tanzania Episcope Conference (TEC) ni mwenyekiti wa huo mkutano/conference kama anavyokuwaga mwenyekiti wa bunge Jenista Mhagama lakini siyo kwamba yeye ndiye spika wa bunge. Yeye ni mwenyekiti tu NA SI KARDINALI, KARDINALI NI CHEO, NI MKUU WA KANISA KATOLIKI KATIKA NCHI, NDIYE HUKUTANA NA MAKARDINALI WENGINE DUNIA NZIMA KUMCHAGUA PAPA/KIONGOZI WA KANISA KATOLIKI DUNIANI.
Hata haya pia ni ya kwako.Hayo ni ya kwako.
Likoje sasa? kama lina kiongozi wa dunia litakosaje kuwa na kiongozi wa nchi?, cardinali ndiye huteua askofu wa jimbo ambapo jina hupelekwa vatican na papa hutangaza kuwa ndiye amemteua, lakini yeye papa anamjulia wapi askofu wa Iringa? mnakuwa wabiiiiiiiiiiiiiiiishi ili tu muonekaane mnajuwa.kanisa katoliki haliko hivyo.
Kardinali si mkuu wa kanisa katika nchi. Ndio maana sio nchi zote zina makadinali. Kandinali ni cheo kinachohusianan na mambo ya kumshauri pope huko roma. Walutheir wao wana mkuu wao wa kanisa tanzania malasusa lakini mfumo wa kikatoliki hauko hivyo. Gazeti la habri leo ni gazeti la ccm hivyo wanaandika kipropaganda zaidi ili kuwachanganya wananchi.
mbili ni mpango,huku ZNZ na huku Tanganyika,hakuna muungano wa kitu kimoja,wanaofikir hivyo ni vipofu.
KANISA Katoliki limekanusha taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari kuwa msimamo wa kanisa hilo ni kuwepo kwa serikali tatu katika katiba mpya.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amesema taarifa hiyo si sahihi bali ilitolewa na Tume ya Haki ya Baraza la Maaskofu pasipo kumshirikisha.
Wao kama Watanzania wanayo haki ya kutoa maoni, hivyo si kosa wakiwa kama Watanzania maoni yao kuwa ni kuwepo serikali tatu, ilichokosea tume hiyo ni kusema kwamba huo ni msimamo wa Kanisa Katoliki jambo ambalo si kweli, alisema.
Pengo alisema anakanusha vikali taaifa hiyo iliyotolewa juzi na vyombo mbalimbali vya habari hususan magazeti na kuwa Kanisa Katoliki lina wajibu wa kutoa msimamo wake katika mambo mawili tu yanayohusu imani na maadili.
Kwa mfano ikitokea hoja kwamba kuwepo na vipengele kwenye katiba vinavyosema hakuna Mungu, kuwepo kwa ndoa za jinsia moja au kuhalalisha utoaji mimba hapo kanisa lina haki ya kusimama na kutoa msimamo wake kwani masuala hayo yanagusa imani na maadili,alisema.
Aliongeza kuwa anatumia nafasi hiyo katika mkutano na waandishi wa habari kutoa msimamo wake kama Mtanzania wa kawaida kuwa mapendekezo yake ni kuendelea kuwepo kwa serikali mbili yaani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kama kuna dosari zozote zilizojitokeza wakati wa kuasisi Muungano zinazotishia umoja wa kitaifa ni heri zikarekebishwa ili uendelee mfumo wa serikali mbili kwani serikali tatu ni mzigo, alisema.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ilitoa tamko ikitaka Bunge Maalumu la Katiba kuepuka kukashifu mapendekezo ya muundo wa serikali tatu.
Chanzo:Habarileo.
Ungetulia na kusoma, basi ungemuelewa Card. Pengo, na wala usingeandika hayo. Hebu rudia kusoma kipande hiki, hasa hapo kwenye bolded red font:
hata mimi nimemshangaa kiongozi wa kiroho kuwasemea waTz zaidi ya mil45 kile anachotaka yeye. hii ni ajabu kweli kweli. hata kama ni maoni binafsi nani asiyejua nafasi ya pengo kwa wakatoliki?
unafikaje level ya ukadinali halafu unakua kwenye position ya kujitetea-tetea??Kwa jinsi Pengo anavyojitetea kuwa hayo ni mawazo yake tu basi naona kuna siku pia atasema anapenda kuwe na mashoga waliohalalishwa Tanzania kwa mawazo yake na sio ya Kanisa katoliki!...anaweza huyu kwani anaonyesha kuwa anasahau kirahisi rahisi tu nafasi yake ktk jamii
Jamani mtaelemishwa mpaka lini? pengo sio Mkuu wa kanisa katoliki tanzania bali ni mkuu wa kanisa katoliki jimbo la dar es salaam. mweneyekiti wa baraza la maaskofu labda ndiye tunaweza kumuita mkuu wa kanisa katoliki tanzania kwa sababu ndiye mweneyekiti wa maaskofu wote. Huu ni msismamo binafsi wa pengo sio wa kanisa katoliki.
hay sure, ndio maana majimbo yote Tanzania yakishaombea asskofu wao, basi humuombea pengo.... think about itJamani mtaelemishwa mpaka lini? pengo sio Mkuu wa kanisa katoliki tanzania bali ni mkuu wa kanisa katoliki jimbo la dar es salaam. mweneyekiti wa baraza la maaskofu labda ndiye tunaweza kumuita mkuu wa kanisa katoliki tanzania kwa sababu ndiye mweneyekiti wa maaskofu wote. Huu ni msismamo binafsi wa pengo sio wa kanisa katoliki.
Sawa mkuu, mimi ningependelea zaidi serikali 1, zanzibar unakuwa tu mkoa kama ulivyo Mbeya au Mwanza halafu waZanzibar wengi wahamasishwe kuhamia bara.
pengo katoa msimamo wake kama mtanzani wa kawaida toa cheo chakePengo amedhihirisha ukereketwa wake kwa CCM na ku-confirm dhana inayolalamikiwa na Waislamu kuwa Serikali ya ccm inafuata sera ya mfumo Kristo.
Rasimu ya Katiba imetokana na mawazo ya wananchi yeye ni nani mpaka adharau matakwa yao? Mamlaka ya kuwasemea wananchi ameyatoa wapi?
Wakatoliki watanisamehe kwa hili, ila Mkuu wenu wa Kiroho amepotoka kuingilia na kutoa msimamo wa kisiasa!
Kufikia hapa naweza nikasema bila shaka yoyote kuwa Pengo ni mfuasi wa kambi ya Lowassa.
Kumbuka kipindi kile Lowassa amefukuzwa kazi kwa sababu ya ufisadi, baada ya muda Cardinal Pengo alimtembelea Lowassa nyumbani kwake na kuzindua kitabu cha mke wa Lowassa, Regina!!
yanini uweke link, soma maelezo haya hapa chini;
A cardinal (Latin: sanctae romanae ecclesiae cardinalis) is a senior ecclesiastical official, an ecclesiastical prince, and usually an ordained bishop. The cardinals of the Roman Catholic Church are collectively known as the College of Cardinals. The duties of the cardinals include attending the meetings of the College and making themselves available individually or in groups to the pope as requested. Most have additional duties, such as leading a diocese or archdiocese or managing a department of the Roman Curia. A cardinal's other main function is electing the pope when the see becomes vacant. During the sede vacante, the period between a pope's death or resignation and the election of his successor, the day-to-day governance of the Church as a whole is in the hands of the College of Cardinals. The right to enter the conclave of cardinals where the pope is elected is limited to those who have not reached the age of 80 years by the day the vacancy occurs.
In 1059, the right of electing the pope was reserved to the principal clergy of Rome and the bishops of the seven suburbicarian sees. In the 12th century the practice of appointing ecclesiastics from outside Rome as cardinals began, with each of them assigned a church in Rome as his titular church or linked with one of the suburbicarian dioceses, while still being incardinated in a diocese other than that of Rome.[SUP][citation needed][/SUP]
The term cardinal at one time applied to any priest permanently assigned or incardinated to a church,[SUP][1][/SUP] or specifically to the senior priest of an important church, based on the Latin cardo (hinge), meaning "principal" or "chief". The term was applied in this sense as early as the ninth century to the priests of the tituli (parishes) of the diocese of Rome.[SUP][1][/SUP] The Church of England retains an instance of this origin of the title, which is held by the two senior members of the College of Minor Canons of St Paul's Cathedral.
Narudia tena Kardinali ni CHEO.
Maneno mhimu kwenye haya maelezo ni; senior, principal, chief. Sasa kama siyo kiongozi wa nchi nzima basi hata Papa siyo kiongozi wa dunia nzima na ingefaa umtaje sasa wewe kiongozi wa kanisa katoliki Tanzania ni nani.
pengo katoa msimamo wake kama mtanzani wa kawaida toa cheo chake
Kwa jinsi Pengo anavyojitetea kuwa hayo ni mawazo yake tu basi naona kuna siku pia atasema anapenda kuwe na mashoga waliohalalishwa Tanzania kwa mawazo yake na sio ya Kanisa katoliki!...anaweza huyu kwani anaonyesha kuwa anasahau kirahisi rahisi tu nafasi yake ktk jamii
Wewe ndiyo unaona habari hii ni ujinga lakini kuona ujinga lazima pia ufahamu ujinga wako uko kiasi gani!.Mtoa mada una ukurutu kwenye ubongo,sidhani kama mtu mwenye akili timamu anaweza kuandika ujinga huo,liondoe tope zito kwenye akili zako,pengo sii saizi yako kumuingiza katika huo ujinga wako,shame on you.