Mwadhamu Polycarp Pengo: Serikali mbili zinatosha

Mwadhamu Polycarp Pengo: Serikali mbili zinatosha

Pengo amedhihirisha ukereketwa wake kwa CCM na ku-confirm dhana inayolalamikiwa na Waislamu kuwa Serikali ya ccm inafuata sera ya mfumo Kristo.
Rasimu ya Katiba imetokana na mawazo ya wananchi yeye ni nani mpaka adharau matakwa yao? Mamlaka ya kuwasemea wananchi ameyatoa wapi?

Wakatoliki watanisamehe kwa hili, ila Mkuu wenu wa Kiroho amepotoka kuingilia na kutoa msimamo wa kisiasa!

Kufikia hapa naweza nikasema bila shaka yoyote kuwa Pengo ni mfuasi wa kambi ya Lowassa.
Kumbuka kipindi kile Lowassa amefukuzwa kazi kwa sababu ya ufisadi, baada ya muda Cardinal Pengo alimtembelea Lowassa nyumbani kwake na kuzindua kitabu cha mke wa Lowassa, Regina!!
Ametaja hizo serikali mbili ni ipi na ipi? Kama nilivyowahi kusema kabla, mimi pia ni muumini wa uwepo wa serikali mbili - ya Tanganyika na ile ya Zanzibar! Lau hili haliwezekani (tunataka kuendelea na muungano), basi iwepo serikali moja tu (ya Muungano), na hilo kama haliwezekani basi tuwe na serikali tatu! Serikali mbili kama zilivyo sasa ni kiini macho tu.
 
Pengo amedhihirisha ukereketwa wake kwa CCM na ku-confirm dhana inayolalamikiwa na Waislamu kuwa Serikali ya ccm inafuata sera ya mfumo Kristo.
Rasimu ya Katiba imetokana na mawazo ya wananchi yeye ni nani mpaka adharau matakwa yao? Mamlaka ya kuwasemea wananchi ameyatoa wapi?

Wakatoliki watanisamehe kwa hili, ila Mkuu wenu wa Kiroho amepotoka kuingilia na kutoa msimamo wa kisiasa!

Kufikia hapa naweza nikasema bila shaka yoyote kuwa Pengo ni mfuasi wa kambi ya Lowassa.
Kumbuka kipindi kile Lowassa amefukuzwa kazi kwa sababu ya ufisadi, baada ya muda Cardinal Pengo alimtembelea Lowassa nyumbani kwake na kuzindua kitabu cha mke wa Lowassa, Regina!!

Sidhani kama Cardinal ndio kiongozi wa wakatoliki Tanzania. Kila jimbo lina askofu wake ambaye anaripoti moja kwa moja kwa Pope. Isipokuwa Cardinal yeye anaruhusiwa kuingia kwenye curia na kuchagua pope. Kwa maana hiyo basi Cardinal Pengo ni Askofu mkuu wa Jimbo la Dar Es Salaam na siyo Kiongozi wa Kanisa Katoliki Tanzania. Kila jimbo lina kiongozi wake ambaye anaweza kuwa ni askofu au askofu mkuu.
 
pengo+px.jpg

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo akiwaonesha waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, nakala ya gazeti la Mwanachi lililoandika habari kuhusu msimamo wa Kanisa juu ya suala la serikali tatu. Picha na Venance Nestory
Na Leon Bahati na Godfrey Nyango'ro, Mwananchi

Posted Jumatano,Marchi5 2014 saa 24:0 AM

Kwa ufupi
Alisema Kanisa Katoliki lingeweza kutoa msimamo iwapo Rasimu ya Katiba ingekuwa na dosari zinazohusu imani au maadili.

Dar es Salaam/Iringa. Siku mbili baada ya Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kutoa waraka wa kulitaka Bunge Maalumu la Katiba kutopuuza mapendekezo ya muundo wa serikali tatu, Askofu Mkuu wa Jimbo Mkuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ameibuka na kusema msimamo huo siyo wa Kanisa Katoliki nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kardinali Pengo pamoja na kukiri kuwa tume ilitoa maoni hayo, alikanusha kuwa taarifa zilizotolewa na moja ya magazeti kuwa msimamo wa Kanisa Katoliki ni serikali tatu.

"Maoni ya Tume hayawezi kuwa ni msimamo wa kanisa. Kanisa Katoliki lina utaratibu wa kutoa misimamo yake na huwa inatolewa na Mwenyekiti wa TEC," alisema.

Hata hivyo, Rais wa TEC, Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa kutoka Jimbo la Iringa, alisema jana kuwa alikuwa na shughuli nyingi, hivyo asingeweza kuzungumzia suala hilo, labda wiki ijayo.

Akizungumza katika makazi yake mjini Iringa, Askofu Ngalalekumtwa alisema: "Mniache, nina shughuli nyingi…labda mnitafute wiki ijayo," alisema.

Vilevile, Pengo ambaye alirejea msimamo wake binafsi wa kuunga mkono Muungano wa serikali mbili, alisema kwa namna Rasimu ya Katiba ilivyo, hakuna kigezo cha kulazimisha Kanisa Katoliki litoe msimamo.

Alisema Kanisa Katoliki lingeweza kutoa msimamo iwapo Rasimu ya Katiba ingekuwa na dosari zinazohusu imani au maadili.

"Kwa mfano, (Rasimu) ingekuwa inasema, hakuna Mungu lazima tungekuja juu kwa sababu inaingilia imani yetu," alisema Kardinali Pengo na kufafanua:

"Vilevile tungeweza kusema inakwenda kinyume na maadili iwapo inaruhusu kuua wazee au inaunga mkono ndoa za jinsi moja."

Tamko la Tume

Tamko la tume hiyo inayoongozwa na Askofu Mkuu wa Tabora, Paulo Ruzoka liliweka bayana kuwa muundo wa serikali mbili haukutatua matatizo ya msingi na badala yake ulilimbikiza kero zilizosababisha Zanzibar kujiundia katiba yake mwaka 2010 bila kushauriana na Tanzania Bara.

Tamko hilo la kurasa 15 lililosambazwa kwa baadhi ya Wajumbe wa Bunge la Katiba, lilitolewa baada ya mkutano wa kitaifa wa Wajumbe wa Kamati za Majimbo za Haki na Amani za Kanisa hilo na Chama cha Wanataaluma Wakatoliki Tanzania (CPT), uliofanyika jijini Dar es Salaam Februari 5 na 6 mwaka huu.

Msimamo binafsi

Kardinali Pengo alisema katika misimamo ya kisiasa ndani ya Kanisa Katoliki, waumini wanatofautiana bila kuzingatia ni kiongozi au muumini wa kawaida na hakuna sababu ya kulazimishwa kuwa na msimamo unaofanana.

Alisema yeye anaona serikali mbili zinaweza kusaidia zaidi katika usalama wa nchi na kujenga umoja hasa katika kuzuia watu wa nje wenye nia mbaya kupenya nchini ili kuanzisha chokochoko za uvunjifu wa amani.

Alisema ana wasiwasi mfumo wa Serikali tatu utatoa mwanya kwa maadui kupenya Zanzibar na hata kuingia Tanzania Bara.

Alitoa mfano wa nchi jirani ya Kenya, ambako matukio kadhaa makubwa ya kigaidi yametokea na kuonya kuwa kamwe asingependea kuona yanafanyika hapa nchini.

Kura ya siri

Akizungumzia mvutano wa mfumo wa upigani kura kwenye Bunge la Katiba, Pengo alisema: "Kura ya siri ndiyo njia pekee ya kutenda haki katika kupitisha vifungu kwenye Bunge linaloendelea mjini Dodoma."

[h=1]Kardinali Pengo aweka wazi msimamo wa Kanisa[/h]
 
Pengine sasa Jaji Warioba aulizwe alimuhoji nani hasa katika taasisi mbali aiwezekani kila kukicha wadau wanajitokeza na kusema vingine kinyume na madai ya mapendekezo ya rasimu kuhusu msimamo wa taasisi nzima.

Hivi kama hao watu wachache kati yetu waliobahatika kutoa maoni kupitia makundi yao na kwenye kutoa mapendekezo walitofautiana kuhusu muundo wa serikali moja, mbili na tatu, iweje tudhani wabunge leo wanadhamana ya wapiga kura wao mpaka wapige kura za siri wakati wengi hawajatoa maoni yoyote directly?

Swala hili ni very complicated na wapiga kura wanahaki za kujua wawakilishi wao wamechagua nini kwa niaba yao kama Kardinali alivyojuzwa (na kuamua kutoa msimamo wake binafsi) na wawakilishi wa baraza mapinduzi walivyojuzwa na kuukana kuwa ni msimamo wa wachache. Mwisho wa siku na watanzania wanahaki hizohizo za kufahamu wawakilishi wao wamewachagulia nini.

Kura ya siri ni kwa sababu ya impact ya mtu mmoja hila kama unawapigia kura watu kwa niaba yao wanahaki ya kujua umewachagulia nini na waamue kama wakurudishe au wakutose na isitoshe kama hupo kwenye chama pia chama kiamue kama hupo pale kwa mawazo ya wengi au utoke kwa kutokubali misimamo ya pamoja. Ndio demokrasia yenyewe na aitaki mzaha mzaha.
 
Sidhani kama Cardinal ndio kiongozi wa wakatoliki Tanzania. Kila jimbo lina askofu wake ambaye anaripoti moja kwa moja kwa Pope. Isipokuwa Cardinal yeye anaruhusiwa kuingia kwenye curia na kuchagua pope. Kwa maana hiyo basi Cardinal Pengo ni Askofu mkuu wa Jimbo la Dar Es Salaam na siyo Kiongozi wa Kanisa Katoliki Tanzania. Kila jimbo lina kiongozi wake ambaye anaweza kuwa ni askofu au askofu mkuu.

Mkuu, Kardinali ni cheo siyo jina, ni cheo cha mkuu wa maaskofu nchi nzima na kiongozi mkuu wa kanisa katoliki nchi nzima na ndiyo yeye na makardinali wenzake dunia nzima hukutana Vatican kumchagua kiongozi wao wa dunia (Baba mtakatifu).
 
Kutokana na penetration ya wakatoliki kwenye system sina shaka serikali 3 ni ndoto
 
Pengo amedhihirisha ukereketwa wake kwa CCM na ku-confirm dhana inayolalamikiwa na Waislamu kuwa Serikali ya ccm inafuata sera ya mfumo Kristo.
Rasimu ya Katiba imetokana na mawazo ya wananchi yeye ni nani mpaka adharau matakwa yao? Mamlaka ya kuwasemea wananchi ameyatoa wapi?

Wakatoliki watanisamehe kwa hili, ila Mkuu wenu wa Kiroho amepotoka kuingilia na kutoa msimamo wa kisiasa!

Kufikia hapa naweza nikasema bila shaka yoyote kuwa Pengo ni mfuasi wa kambi ya Lowassa.
Kumbuka kipindi kile Lowassa amefukuzwa kazi kwa sababu ya ufisadi, baada ya muda Cardinal Pengo alimtembelea Lowassa nyumbani kwake na kuzindua kitabu cha mke wa Lowassa, Regina!!
Huyu mfipa mwenzangu arudi nyumbani kijijini kwao Mwazye akatulie alee na kucheza na wajuu wake huko(watoto wa nduguze) naona kashindwa kuelewa hisia za waumini wake, mimi hata kanisa langu katoriki liseme litanitimua ni Serikali tatu tu......hyu mzee anataka kuzeka vibaya mwachie baba Ngalale kumtwa. Kwanza ana mamlaka gani ya kuipinga TEC, wapi vichwa kama Pr Mapunda, Karugendo, Askofu mstaafu Dodoma Isuja , nendeni msasani mkampumzishe huyu mzee Pengo akiona majukumu mazito aachie ngazi kama papa benedict 16
 
Mimi ni muumini wa kanisa katoliki tena muumini kweli kweli lakini kwa hili Askofu Pengo amepotoka na naamini ili aendelee kuwa na heshima aliyonayo kwa waumini wake aseme huo ni masimamo wake yeye na sio msimamo wa kanisa katoliki!!! wananchi wameshaamua namna wanavyotaka kuongozwa na sio yeye kutulisha misimamo yake!!!!
 
Pengo ni Mtanzania ana haki ya kutoa maoni yake. Si kweli kwamba akisema jambo basi ni msimamo wa wakatoliki wote, wewe naona unasumbuliwa na chuki zako za kidini
 
Mkuu, Kardinali ni cheo siyo jina, ni cheo cha mkuu wa maaskofu nchi nzima na kiongozi mkuu wa kanisa katoliki nchi nzima na ndiyo yeye na makardinali wenzake dunia nzima hukutana Vatican kumchagua kiongozi wao wa dunia (Baba mtakatifu).

Kaka Pasco ni mkatoliki na mweledi sana wa hizi hierarchy za wakatoliki. Ngoja nimwite aje kuondoa huu ukakasi.
Pasco njoo uamue ugomvi huku..
 
Last edited by a moderator:
Serikali mbili kila mtu afanye mambo yake,ndo mpango mzima...
 
Si kweli mkuu...soma vizuri hiyo link hapo Cardinal (Catholicism) - Wikipedia, the free encyclopedia. Cardinal siyo kiongozi wa kanisa katoliki nchi nzima.

yanini uweke link, soma maelezo haya hapa chini;

A cardinal (Latin: sanctae romanae ecclesiae cardinalis) is a senior ecclesiastical official, an ecclesiastical prince, and usually an ordained bishop. The cardinals of the Roman Catholic Church are collectively known as the College of Cardinals. The duties of the cardinals include attending the meetings of the College and making themselves available individually or in groups to the pope as requested. Most have additional duties, such as leading a diocese or archdiocese or managing a department of the Roman Curia. A cardinal's other main function is electing the pope when the see becomes vacant. During the sede vacante, the period between a pope's death or resignation and the election of his successor, the day-to-day governance of the Church as a whole is in the hands of the College of Cardinals. The right to enter the conclave of cardinals where the pope is elected is limited to those who have not reached the age of 80 years by the day the vacancy occurs.

In 1059, the right of electing the pope was reserved to the principal clergy of Rome and the bishops of the seven suburbicarian sees. In the 12th century the practice of appointing ecclesiastics from outside Rome as cardinals began, with each of them assigned a church in Rome as his titular church or linked with one of the suburbicarian dioceses, while still being incardinated in a diocese other than that of Rome.[SUP][citation needed][/SUP]

The term cardinal at one time applied to any priest permanently assigned or incardinated to a church,[SUP][1][/SUP] or specifically to the senior priest of an important church, based on the Latin cardo (hinge), meaning "principal" or "chief". The term was applied in this sense as early as the ninth century to the priests of the tituli (parishes) of the diocese of Rome.[SUP][1][/SUP] The Church of England retains an instance of this origin of the title, which is held by the two senior members of the College of Minor Canons of St Paul's Cathedral.

Narudia tena Kardinali ni CHEO.

Maneno mhimu kwenye haya maelezo ni; senior, principal, chief. Sasa kama siyo kiongozi wa nchi nzima basi hata Papa siyo kiongozi wa dunia nzima na ingefaa umtaje sasa wewe kiongozi wa kanisa katoliki Tanzania ni nani.
 
Mkuu, Kardinali ni cheo siyo jina, ni cheo cha mkuu wa maaskofu nchi nzima na kiongozi mkuu wa kanisa katoliki nchi nzima na ndiyo yeye na makardinali wenzake dunia nzima hukutana Vatican kumchagua kiongozi wao wa dunia (Baba mtakatifu).

Kaka Pasco ni mkatoliki na mweledi sana wa hizi hierarchy za wakatoliki. Ngoja nimwite aje kuondoa huu ukakasi.
Pasco njoo uamue ugomvi huku..
Tafadhali, asije Paschal Mayalla aje Pasco
 
Last edited by a moderator:
Pengo kapotoka maana wizara ya ulinzi na usalama bado inabaki kuwa ya muungano hata katika serikali tatu.
 
Tume ya Warioba iliweka wazi kuwa wizara ya ulinzi na usalama itabaki kuwa ya Muungano, yeye wasiwasi wake ni ulinzi na usalama .Mbona hilo limetatuliwa katika rasimu tayari.TUNATAKA TANGANYIKA au Zanzibar ife tubaki na kimoja Tanzania.
 
Tume ya warioba iliweka wazi kuwa wizara ya ulinzi na usalama itabaki kuwa ya Muungano, yeye wasiwasi wake ni ulinzi na uslama .mbona hilo limetatuliwa katika rasimu tayari.TUNATAKA TANGANYIKA. au zanzibar ife tubaki na kimoja Tanzania.

Msamehe, anazeeka vibaya!
 
Kaka Pasco ni mkatoliki na mweledi sana wa hizi hierarchy za wakatoliki. Ngoja nimwite aje kuondoa huu ukakasi.
Pasco njoo uamue ugomvi huku..

Yanini umwite Pasco, soma hiyo makala ya mwananchi hapo juu inasema Pengo amekataa huo si msimamo wa kanisa katoliki, kwanini pengo akatae kwa niaba ya kanisa nzima na si askofu mwingine yeyote?.
 
Back
Top Bottom