Mwadhamu Polycarp Pengo: Serikali mbili zinatosha

Mwadhamu Polycarp Pengo: Serikali mbili zinatosha

na wasiwasi ccm wasije kuwa wanamtumia. mbona wakati zanzibar wanabadili katiba hakutoa onyo kwa kikwete.
 
Kiongozi wetu wa kiroho hawezi kutuamlia masuala ya nchi kwa hisia zake na uswahiba wake kwa maccm, akichoka achie wengine huyu mzee vipi huyu ndiye anatuletea hata kelele zisizokuwa na maana ndani ya kanisa
 
Yanini umwite Pasco, soma hiyo makala ya mwanacnhi hapo juu inasema Pengo amekataa huo si msimamo wa kanisa katoliki, kwanini pengo akatae kwa niaba ya kanisa nzima na si askofu mwingine yeyote?.

Hata Ruzoka alipotoa ule Waraka alisema ni Waraka wa Kanisa Katoliki. Ruzoka amepata wapi mamlaka ya kuwasemea wakatoliki wote?
 
Ni mawazo yake ,upande wangu namsupport kwa asilimia mia,kama serikali mbili haiwezekani basi moja,na kama moja itashindikana basi kila mtu aende kwake maana ndoa itakuwa ndoana.Serikali Tatu hatuziwezi kama hizi mbili ni mgogoro tatu zitawezekana?
 
Hata Ruzoka alipotoa ule Waraka alisema ni Waraka wa Kanisa Katoliki. Ruzoka amepata wapi mamlaka ya kuwasemea wakatoliki wote?

Sasa huoni amepingwa na Pengo kwamba huo si msimamo wa kanisa?. Kama ulishawahi kuhudhuria ibada ya misa takatifu wakiwepo maaskofu wengi na Kardinali awepo ndipo utagunduwa yeye ndiye mkubwa wao kwanza hili halina hata haja ya kubishana kama watoto wakati inajulikana wazi.
 
Kuna baadhi ya watu wanatumia njia zote hata zile za kilaghai ili kupitisha ajenda zao. Wanashindwa kusimama wao wenyewe ili wahesabiwe kwa kutoa maoni yao kwa sababu pamoja na mambo mengine, wanasumbuliwa na inferiority complex. Hawajiamini kama kauli zao zinakubaliwa/zitakubaliwa na wanachi.

Huwezi kulitumia kanisa Katoliki kwa mambo ya kilaghai hasa ikichukuliwa kuwa kanisa ni kioo katika jamii kwenye maswala ya ubinadamu.

Kuelekea upatikanaji wa Katiba mpya, tutawasikia wengi wakija na matamko huku wakidai yametolewa na taasisi zinazo heshimika katika jamii.

Tunashukuru Baba Askofu kwa kutoa ufafanuzi mzuri kulingana na tamko la Tume ya Haki na Amani.
Unajua sisi wabongo tunaangalia maslahi,yakitajwa maslahi yako unafurahi yakitajwa maslahi ya mwingine unachukia

Mfano mdogo ni wewe Mwanadiwani umekuja na thread hii na kumpongeza baba askofu kwasababu tu kaunga mkono hoja yenye maslahi kwako na chama chako ila naye angeunga mkono serikali tatu hapa tungesikia matusi na kejeli za kila aina

Lakini pia unasahau kuwa Pengo katoa maoni yake yeye kama yeye tena mtu mmoja na upande wa pili wametoa msimamo wao kama baraza hivyo ulipaswa tu kutafakari ni vupi au wepi wanamashiko hoja ya mmoja na hoja ya wengi

Pia unaposema kuna watu wamekosa ushawishi kwa kutaka kupenyeza maoni yao kupitia taasisi zenye heshima unataka kutuaminisha nini? Je ccm wamekosa ushawishi kiasi cha kumuomba Pengo awapenyezee hoja yao ya serikali mbili ambayo hata hivyo licha ya kutokuwemo kwenye rasimu ya Warioba lkn pia wananchi wengi waliotoa maoni yao waliona kuwa haifai?

Twende polepole tu tutafika msitake kujenga hoja zenu kwa mgongo wa watu wengine mtu anaye jiamini hutoa hoja yake bila kuzingatia mwingine atasema nini na kama inamashiko itaungwa mkono na wengi. Kama rasimu ya pili ya Katiba ya mzee Warioba.
 
Mnamsema bure kwa kuwa hamjamuelewa. Amesema Kanisa huwa halitoi msimamo kuwaelekeza Wakatoliki nini cha kuchagua, labda huo msimamo uwe unahusu masuala ya IMANI au MAADILI. Hata inapolazimika kutoa msimamo wa KANISA, ni Baraza la Maaskofu (TEC) pekee linaweza kutoa msimamo wa KANISA KATOLIKI kupitia Rais wake (ambaye sio yeye Kard. Pengo). Maoni mengine yanaweza yakatolewa na mtu binafsi (kama yeye Pengo) au vyombo vya kanisa (kama Baraza la Walei), na hailazimishi kila Mkatoliki kuifuata kwani haina uhusianao wa moja kwa moja na IMANI au MAADILI.

Tuwe makini tunapowanukuu viongozi wetu, hasa wanapokuwa wasomi kama Pengo, kwa maana lugha ya kisomi inaweza kumfanya mtu asimuelewe halafu akakimbilia kuanzisha thread humu kama alivyofanya huyu tpmazembe
 
"...Alisema ana wasiwasi mfumo wa Serikali tatu utatoa mwanya kwa maadui kupenya Zanzibar na hata kuingia Tanzania Bara..." amenukuliwa Pengo!

Ninataka nielewe msimamo wa Kardinali Pengo katika kauli hii! Nataka niamini sasa kilicho ndani ya moyo wake ni hofu hii hasa baada ya kumpoteza Padri mmoja kule Zanzibar na wengine kushambuliwa. Naona mantiki ya msomi huyu (maana Askofu kwa wakatoliki ni lazima awe na digrii kadhaa! na walau PhD).

Lakini pamoja na kuwa mnyanikifu(pragmatism) naogopa simuungi mkono Kardinali Pengo! Simuingi maana tunajenga katiba ya miaka kadhaa. Tatizo la watu wenye siasa kali kama kina Shabbab au wale kina Osama zitapita, katiba itakuwepo. Matatizo ya leo yasitukwaze katika kufikiria Tanzania tuipendayo. Na hili ndilo tatizo kubwa la CCM - wao wanafikiri katiba mpya ni ya mahitji ya sasa tu, yenye kuwaweka pazuri kwa miaka michache wale wazee wenye kushika mpini sasa waliobaki nayo - wakiwa na nguvu bado. La hasha! Mhashamu mpendwa Kardinali Pengo- tuangalie sisi tunaoanza maisha- tunahitaji hifadhi zaidi ya miaka 10 ijayo, tunaomba katiba ya kukidhi maisha ya watoto na wajukuu wetu. Tunahitaji Katiba yenye kuzuia kina Shabab kuja na kutusumbua. Kama Zanzibar huru itakwenda kinyume ikawaruhusu hao watenda uhalifu----lakini watawezaje hali Serikali ya Muungano ndiyo yenye Jeshi na wakithubutu, basi Tanganyika itaingia kama ilivyoingia Uganda (mamaaaa nimeharibu hoja yangu nini!!!?)
 
... na Pengo anazungumziaje mamilioni ya wakatoliki ambao hawaungi mkono kauli yake??...
Ungetulia na kusoma, basi ungemuelewa Card. Pengo, na wala usingeandika hayo. Hebu rudia kusoma kipande hiki, hasa hapo kwenye bolded red font:
... Aliongeza kuwa anatumia nafasi hiyo katika mkutano na waandishi wa habari kutoa msimamo wake kama Mtanzania wa kawaida kuwa mapendekezo yake ni kuendelea kuwepo kwa serikali mbili yaani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar....
 
Pengo amedhihirisha ukereketwa wake kwa CCM na ku-confirm dhana inayolalamikiwa na Waislamu kuwa Serikali ya ccm inafuata sera ya mfumo Kristo.
Rasimu ya Katiba imetokana na mawazo ya wananchi yeye ni nani mpaka adharau matakwa yao? Mamlaka ya kuwasemea wananchi ameyatoa wapi?

Wakatoliki watanisamehe kwa hili, ila Mkuu wenu wa Kiroho amepotoka kuingilia na kutoa msimamo wa kisiasa!

Kufikia hapa naweza nikasema bila shaka yoyote kuwa Pengo ni mfuasi wa kambi ya Lowassa.
Kumbuka kipindi kile Lowassa amefukuzwa kazi kwa sababu ya ufisadi, baada ya muda Cardinal Pengo alimtembelea Lowassa nyumbani kwake na kuzindua kitabu cha mke wa Lowassa, Regina!!


Tulia acha jazba na papara uandike unachotaka kuandika kwa utulivu utaeleweka tu. Kasema haya ni maoni yake yeye kama Pengo. Pengo ni askofu wangu (Jimbo Kuu la DSM) lakini pamoja na kuwa kiongozi wangu katika hili la serikali mbili hanishawishi wala hawezi kunibadilisha kamwe. Hayo yatabaki kuwa maoni na mtazamo wake nami nina maoni na mtazamo wangu. Ni kweli kama tunataka muungano wa dhati ni Serikali moja tu. Haya mengine ni njia ya kuachana in a long run. Lakini tufanyeje ikiwa beneficiaries wa muungano hawaoni kuwa wana benefit na ndio wa kwanza kulalama na kuufifisha huo muungano kwa vitimbi vya kila siku?

Hayo ya Mfumo Kristo ni wasiwasi wa wasiokwenda shule na wenye uwezo mdogo wa kuona na kuchambua mambo. Angekuwa sehemu ya huo mfumo mnaoudai unadhani angetoka hadharani na kusema aliyosema? Tumieni vichwa kuhifadhi ubongo na sio kufugia nywele na kuvaa kofia. Kwa hiyo serikali inayoongozwa na Muislamu na msaidizi wake inafuata mfumo kristu miaka yote? Basi utakuwa na mfumo wenye faida kubwa kwa jamii na wao wamekosa alternative ya mfumo unaofaa kufuatwa!!

Haya ya ufuasi wa Lowasa sijui yanaingiaje hapa.... Kwani Lowasa ndiye muasisi wa dhana ya serikali 2?
 
Ana yake huyu mzee, sio hivi hivi.

KANISA Katoliki limekanusha taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari kuwa msimamo wa kanisa hilo ni kuwepo kwa serikali tatu katika katiba mpya.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amesema taarifa hiyo si sahihi bali ilitolewa na Tume ya Haki ya Baraza la Maaskofu pasipo kumshirikisha.

"Wao kama Watanzania wanayo haki ya kutoa maoni, hivyo si kosa wakiwa kama Watanzania maoni yao kuwa ni kuwepo serikali tatu, ilichokosea tume hiyo ni kusema kwamba huo ni msimamo wa Kanisa Katoliki jambo ambalo si kweli," alisema.

Pengo alisema anakanusha vikali taaifa hiyo iliyotolewa juzi na vyombo mbalimbali vya habari hususan magazeti na kuwa Kanisa Katoliki lina wajibu wa kutoa msimamo wake katika mambo mawili tu yanayohusu imani na maadili.

"Kwa mfano ikitokea hoja kwamba kuwepo na vipengele kwenye katiba vinavyosema hakuna Mungu, kuwepo kwa ndoa za jinsia moja au kuhalalisha utoaji mimba hapo kanisa lina haki ya kusimama na kutoa msimamo wake kwani masuala hayo yanagusa imani na maadili,"alisema.

Aliongeza kuwa anatumia nafasi hiyo katika mkutano na waandishi wa habari kutoa msimamo wake kama Mtanzania wa kawaida kuwa mapendekezo yake ni kuendelea kuwepo kwa serikali mbili yaani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar.

"Kama kuna dosari zozote zilizojitokeza wakati wa kuasisi Muungano zinazotishia umoja wa kitaifa ni heri zikarekebishwa ili uendelee mfumo wa serikali mbili kwani serikali tatu ni mzigo," alisema.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ilitoa tamko ikitaka Bunge Maalumu la Katiba kuepuka kukashifu mapendekezo ya muundo wa serikali tatu.
Chanzo:Habarileo.
 
Mimi ni muumini wa kanisa katoliki tena muumini kweli kweli lakini kwa hili Askofu Pengo amepotoka na naamini ili aendelee kuwa na heshima aliyonayo kwa waumini wake aseme huo ni masimamo wake yeye na sio msimamo wa kanisa katoliki!!! wananchi wameshaamua namna wanavyotaka kuongozwa na sio yeye kutulisha misimamo yake!!!!

Kwani mkuu si amesema ni msimamo wake.. Au hujamuelewa...
 
mkuu unaonekana unajua mengi, labda ungetuelewesha kidogo, ni nini hasa kilichopo nyuma ya hii kauli ya pengo. kwani wananchi wanataka serikali 3 kwa mujibu wa tume ya warioba, na katiba ni ya wananchi, ni kwanini pengo anatumia cheo chake ndani ya mwanvuli wa usomi kuwaamlia waTz zaidi ya mil45 walioamua wawe na serikali 3?

Mnamsema bure kwa kuwa hamjamuelewa. Amesema Kanisa huwa halitoi msimamo kuwaelekeza Wakatoliki nini cha kuchagua, labda huo msimamo uwe unahusu masuala ya IMANI au MAADILI. Hata inapolazimika kutoa msimamo wa KANISA, ni Baraza la Maaskofu (TEC) pekee linaweza kutoa msimamo wa KANISA KATOLIKI kupitia Rais wake (ambaye sio yeye Kard. Pengo). Maoni mengine yanaweza yakatolewa na mtu binafsi (kama yeye Pengo) au vyombo vya kanisa (kama Baraza la Walei), na hailazimishi kila Mkatoliki kuifuata kwani haina uhusianao wa moja kwa moja na IMANI au MAADILI.

Tuwe makini tunapowanukuu viongozi wetu, hasa wanapokuwa wasomi kama Pengo, kwa maana lugha ya kisomi inaweza kumfanya mtu asimuelewe halafu akakimbilia kuanzisha thread humu kama alivyofanya huyu tpmazembe
 
Yaani huyu hana hata aibu, anaonyesha msimamo wake wa kisiasa kabisa.

Soma katiba mkuu, kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake... Sasa yale si maoni yake? Hajawaambia wa catholic wawe kama yeye
 
Mnamsema bure kwa kuwa hamjamuelewa. Amesema Kanisa huwa halitoi msimamo kuwaelekeza Wakatoliki nini cha kuchagua, labda huo msimamo uwe unahusu masuala ya IMANI au MAADILI. Hata inapolazimika kutoa msimamo wa KANISA, ni Baraza la Maaskofu (TEC) pekee linaweza kutoa msimamo wa KANISA KATOLIKI kupitia Rais wake (ambaye sio yeye Kard. Pengo). Maoni mengine yanaweza yakatolewa na mtu binafsi (kama yeye Pengo) au vyombo vya kanisa (kama Baraza la Walei), na hailazimishi kila Mkatoliki kuifuata kwani haina uhusianao wa moja kwa moja na IMANI au MAADILI.

Tuwe makini tunapowanukuu viongozi wetu, hasa wanapokuwa wasomi kama Pengo, kwa maana lugha ya kisomi inaweza kumfanya mtu asimuelewe halafu akakimbilia kuanzisha thread humu kama alivyofanya huyu tpmazembe

Mkuu umenena sahihi kabisa, na hicho ndicho alichokisema Pengo; hata kama hatutakubaliana naye kwa msimamo wake "binafsi" lakini tusipotoshe alichokisema. Labda nirudie kwa faida ya wale wapotoshoji akina LB7;

Kasema: Kanisa Katoliki haliwaelekezi waumini wake cha kufanya isipokuwa pale suala husika linapogusa IMANI na MAADILI, hapo Kanisa linakuwa halina jinsi bali kutoa maelekezo. Pia kasema yeye BINAFSI anaunga mkono Serikali Mbili. Najua kuna ile "mitambo" ya Lumumba itakuja na "Waraka wa Kanisa, 2010" kama rejea kwa ajili ya kupotosha alichokisema Kardinali, karibuni.
 
Tuwe makini tunapowanukuu viongozi wetu, hasa wanapokuwa wasomi kama Pengo, kwa maana lugha ya kisomi inaweza kumfanya mtu asimuelewe halafu akakimbilia kuanzisha thread humu kama alivyofanya huyu tpmazembe[/QUOTE]

mkuu unena vema sana hasa hapo uliposema lugha za kisomi huwa inakuwa na ugumu sana wa kueleweka kwa kuwa lugha yake inayotumika ni ngumu na ni ya kitaalam sana sasa ili uielewe yakupasa uwe msomi si kukariri tu bal uwe msomi wa kujenga hoja.
thanx!!
 
mkuu unaonekana unajua mengi, labda ungetuelewesha kidogo, ni nini hasa kilichopo nyuma ya hii kauli ya pengo. kwani wananchi wanataka serikali 3 kwa mujibu wa tume ya warioba, na katiba ni ya wananchi, ni kwanini pengo anatumia cheo chake ndani ya mwanvuli wa usomi kuwaamlia waTz zaidi ya mil45 walioamua wawe na serikali 3?

Ni kweli baadhi ya wanachi wanataka Serikali 3 lakini sio wote; hata Ripoti ya Warioba inaonesha ni asilimia ngapi wanaotaka Serikali 3, 2, 1, na hata Muungano wa Mkataba. Pengo, kama mwananchi, atakuwa katika hao wachache wanaotaka Serikali 2; ni haki yake alimradi haongei kwa niaba ya Kanisa na, in fact amefafanua vizuri, ni maoni yake binafsi.
 
Kufikia hapa naweza nikasema bila shaka yoyote kuwa Pengo ni mfuasi wa kambi ya Lowassa.
Kumbuka kipindi kile Lowassa amefukuzwa kazi kwa sababu ya ufisadi, baada ya muda Cardinal Pengo alimtembelea Lowassa nyumbani kwake na kuzindua kitabu cha mke wa Lowassa, Regina!!
Mkuu Lidelele, kwanza haitwi Pengo, anaitwa Mwandhama Policarp, Cardinali Pengo. Huyu ni kiongozi wa kiroho wa Wakatoliki, ila pia yeye kama Pengo, ni raia wa Tanzania mwenye haki zote sio tuu kutoa maoni bali pia kushiriki katika siasa, au serikali, toka serikali za mitaa hadi serikali kuu kwa mujibu wa katiba!.

Amebainisha wazi huo ni mtazamo wake yeye binafsi kama Polycarp Pengo na sio msimamo wa Kanisa Katoliki!.

NB. Kwa vile viongozi wa dini ni trend setters wazuri kwa wafuasi wa dini zao, msimamo huu ni msumari wa moto kwa mashabiki wa serikali tatu, kwa sababu waumini watiifu wa Kanisa Katoliki waliomo ndani ya Bunge Maalum la Katiba, watapigia kura serikali mbili ili kumuunga mkono kiongozi wao wa kiroho kwa imani kuwa kile anachokiona yeye ndio right.

Japo Eddo ni Mlutheri, mkewe Regi, ni Mkatoliki, hivyo Mwandhama Policarp, Cardinali Pengo, did the right thing, kumtembelea muumini wake na kuzindua kitabu chake!. Hata mimi kama Mkatoliki, nina haki ya kumualika Mwandhama Policarp, Cardinali Pengo aje nyumbani kwangu au kwenye studio yangu pale PPR-Mkwepu kuja kuzindua kipindi kipya kiitwacho "Kwa Maslahi ya Taifa!".
Kitakachoanza hivi karibuni!.

Sasa kama imetokea mume wa muumini wake ni Eddo, then ujio wake ukautafakari kuwa Mwandhama Policarp, Cardinali Pengo, ni mfuasi wa Eddo, rukhsa kuamini vyovyote unavyoamini, na mimi naweza kuamini hata wale wageni fulani muhimu, waliokaribishwa Ikulu kupata juice, chai na vitafunwa, ni wafuasi wa JK, hence wafuasi wa CCM!!, nitakuwa niko huru kuwaza hivyo, kufikiri hivyo na kusema hivyo as long as long ukweli unabaki ni ukweli tuu!.
Pasco.
 
hata mimi nimemshangaa kiongozi wa kiroho kuwasemea waTz zaidi ya mil45 kile anachotaka yeye. hii ni ajabu kweli kweli. hata kama ni maoni binafsi nani asiyejua nafasi ya pengo kwa wakatoliki?

sasa hii ni nini!!???

Tulishawaachia akina warioba kazi, wakamaliza... na sasa tumewapa watu mia sita ukumbi wafanye upuuzi na maigizo, then huyu jamaa nae anakuja kivyake

where is the authorization matrix in the country, na Pengo anazungumziaje mamilioni ya wakatoliki ambao hawaungi mkono kauli yake??

HE LOST CREDIBILITY LONG AGO, AND HE SHOULD TRY TO KEEP THE SMALL RESPECT HE HAS TO HIMSELF, THIS IS A SILLY MISTAKE TO MAKE AND HE HAD NO REASON WHATSOEVER

SOMETIMES UKISHINDWA KUELEWA NAFASI YAKO, UNAISHIA KUWA KANJANJA TU KAMA KANJANJA WENGINE.... PENGO COULD AHVE MADE SOME ONE ELSE MAKE THOSE REMARKS
 
Back
Top Bottom