PreGE2025 Mwabukusi: Tunamtaka Mdude akiwa hai

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kama wewe ni mmoja wao anza kujitafakari matendo mnayowafanyia waTanzania na ubadilike.

"Hakuna cha kuwafanya"?
Chukulia mfano wewe mwenyewe hapo; unadhani hakuna cha kukufanya kwa misimamo yako hii ya kuwafarakanisha waTanzania kwa misingi ya kidini tu?
Mbona ni rahisi sana kumdhibiti mtu kama wewe!
nyie yule dada simlimpiga ngumi ya jicho, zitto simlimtega sumu, yule mlinzi wa dr.slaa mlimhasi kwa kumkata korodani ndani ya ofisi za cdm, niongeze? tulieni kuweni wapole
 
and most likely wamemuua ndiyo maana wanajichanganya eti kutoa milioni tamo, mala kuunda task force ya kumtafuta etc etc
Nchi ngumu sana hii. Ukitaka kuishi nunua kufuli la mdomo. Ukitaka kusema sifu na kulamba viatu.
 
Mtihani uko sehemu moja tu; kama wamemuua!!
Ninatamani vita ya viongozi na raia iibuke, yaani magari ya viongozi yashambuliwr, yaani kinuke.
Huu ni unyama kumuua kijana wa watu kisa kuongea tu
 
Wewe nyumbu unauwezo huo? Mtandao Warrior!
Ninayo orodha ya watu wa aina yako. Sihitaji kusumbuka na kujibishana na shetani kama wewe humu., kama huyo mwenzie unayemjibia. Nyinyi ni kuwapa taarifa tu mbaki mkijua nafasi zenu.
 
nyie yule dada simlimpiga ngumi ya jicho, zitto simlimtega sumu, yule mlinzi wa dr.slaa mlimhasi kwa kumkata korodani ndani ya ofisi za cdm, niongeze? tulieni kuweni wapole
Sijui unaweweseka na kitu gani. hayo siyajui, ninayoyajuwa ni ushetani wenu, kundi lenu na wengi wenu mkija humu JF kueneza chuki kwa waTanzania.
hilo pekee ndilo linalonihusu mimi.
 
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniphace Mwabukusi, amevitaka vyombo vya dola kuhakikisha kuwa mwanaharakati Mdude Nyagali anapatikana akiwa hai, huku akilaani vikali kauli ya kutolewa zawadi ya Shilingi milioni tano kwa atakayesaidia kupatikana kwake akiwa hai au mfu.

“Tumesikia na kuona maafisa wa polisi kutoka Makao Makuu wakishughulikia suala la Mdude, lakini pia tumeshuhudia tangazo lililosambazwa mitandaoni kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akiahidi zawadi ya Shilingi Milioni Tano kwa atakayefanikisha kupatikana kwa Mdude – eti akiwa hai au amekufa. Hili haliingii akilini,” amesema Mwabukusi kupitia chapisho lake katika mtandao wa X siku ya Jumanne.

Amesisitiza kuwa Mdude siyo jambazi, mwizi wala mhalifu wa kawaida, bali ni mwanaharakati ambaye adui zake wakuu ni wale wasio na uvumilivu wa kukosolewa.

“Msimamo wetu kama Rafiki za Mdude ni mmoja: Tunamtaka Mdude akiwa hai. Kama kuna kosa lolote, ashitakiwe kwa mujibu wa sheria. Hatuwezi kuvumilia taifa linalogeuka kuwa la mateso na vitisho kwa wanaoikosoa serikali,” ameongeza.

Aidha Mwabukusi ametahadharisha kuwa uvumilivu wa wananchi unafikia ukingoni, na kama ukweli kuhusu kupotea kwa Mdude hautatolewa haraka, hatua kali zaidi zitachukuliwa.

“Tunaendelea kujitahidi kuwa na hekima kabla ya kufikia ukomo wake. Bila Mdude na majibu yanayoeleweka kuhusu nani anawateka Watanganyika, punde tutafikia mahali pa kuchora mstari na kutafuta suluhisho mikononi mwetu. Mungu atakuwa upande wetu, Katiba itakuwa upande wetu, sheria itakuwa upande wetu, na jumuiya za kimataifa zitakuwa upande wetu”, ameeleza huku akimalizia kwa maneno yenye hamasa kubwa: “Sisi siyo njiwa tunduni, sisi ni tai kichaa.”

Siku ya Jumatatu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dkt. Juma Homera alisema kuwa tayari amelielekeza Jeshi la Polisi kuongeza jitihada za kuwatafuta wahusika waliomshambulia kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mdude Nyagali, huku akiahidi Tsh Milioni 5 kwa atakayesaidia kumpata kada huyo alipo akiwa hai au amekufa.

Akizungumza baada ya viongozi wa CHADEMA mkoani humo na Kanda ya Nyasa kufika ofisini kwake kujua hatua zilizochukuliwa, Dkt. Homera alisema yupo pamoja na chama hicho kuhakikisha
View attachment 3326037
Source: Jambo TV

Soma pia Pre GE2025 - RC Mbeya atoa TSh 5 Milioni kwa atakayetoa taarifa za Mdude, aagiza Polisi kuwasaka waliomteka

Ile barua ya Mdude ilitueleza ni nani anayetaka aondolewe.
 
Sijui unaweweseka na kitu gani. hayo siyajui, ninayoyajuwa ni ushetani wenu, kundi lenu na wengi wenu mkija humu JF kueneza chuki kwa waTanzania.
hilo pekee ndilo linalonihusu mimi.
nyie ndo mlianzisha chuki kwa kutangaza uasi na uhaini mkatutishia kukinukisha, tuliwambia hizi rebelion hakuna ziliposhinda, hamkusikia
 
'eddy' sina nia wala hamu ya kuendeleza mjadala na wewe; kwa sababu ninakufahamu siku nyingi kwa michango yako humu. Niliyo kwisha eleza kwako yanajitosheleza. Ukitaka kuyatafakari na kujitafakari wewe mwenyewe katika mchango wako katika kufarakanisha nchi hii, hiyo ni shauri yako mwenyewe.
 
mkuu, amani na utulivu uliopo ni manmade, haujaja byitself, unaona wale kule wamebadili mwenyekiti wameparanganyika
 
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniphace Mwabukusi, amevitaka vyombo vya dola kuhakikisha kuwa mwanaharakati Mdude Nyagali anapatikana akiwa hai, huku akilaani vikali kauli ya kutolewa zawadi ya Shilingi milioni tano kwa atakayesaidia kupatikana kwake akiwa hai au mfu.

“Tumesikia na kuona maafisa wa polisi kutoka Makao Makuu wakishughulikia suala la Mdude, lakini pia tumeshuhudia tangazo lililosambazwa mitandaoni kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akiahidi zawadi ya Shilingi Milioni Tano kwa atakayefanikisha kupatikana kwa Mdude – eti akiwa hai au amekufa. Hili haliingii akilini,” amesema Mwabukusi kupitia chapisho lake katika mtandao wa X siku ya Jumanne.

Amesisitiza kuwa Mdude siyo jambazi, mwizi wala mhalifu wa kawaida, bali ni mwanaharakati ambaye adui zake wakuu ni wale wasio na uvumilivu wa kukosolewa.

“Msimamo wetu kama Rafiki za Mdude ni mmoja: Tunamtaka Mdude akiwa hai. Kama kuna kosa lolote, ashitakiwe kwa mujibu wa sheria. Hatuwezi kuvumilia taifa linalogeuka kuwa la mateso na vitisho kwa wanaoikosoa serikali,” ameongeza.

Aidha Mwabukusi ametahadharisha kuwa uvumilivu wa wananchi unafikia ukingoni, na kama ukweli kuhusu kupotea kwa Mdude hautatolewa haraka, hatua kali zaidi zitachukuliwa.

“Tunaendelea kujitahidi kuwa na hekima kabla ya kufikia ukomo wake. Bila Mdude na majibu yanayoeleweka kuhusu nani anawateka Watanganyika, punde tutafikia mahali pa kuchora mstari na kutafuta suluhisho mikononi mwetu. Mungu atakuwa upande wetu, Katiba itakuwa upande wetu, sheria itakuwa upande wetu, na jumuiya za kimataifa zitakuwa upande wetu”, ameeleza huku akimalizia kwa maneno yenye hamasa kubwa: “Sisi siyo njiwa tunduni, sisi ni tai kichaa.”

Siku ya Jumatatu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dkt. Juma Homera alisema kuwa tayari amelielekeza Jeshi la Polisi kuongeza jitihada za kuwatafuta wahusika waliomshambulia kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mdude Nyagali, huku akiahidi Tsh Milioni 5 kwa atakayesaidia kumpata kada huyo alipo akiwa hai au amekufa.

Akizungumza baada ya viongozi wa CHADEMA mkoani humo na Kanda ya Nyasa kufika ofisini kwake kujua hatua zilizochukuliwa, Dkt. Homera alisema yupo pamoja na chama hicho kuhakikisha
View attachment 3326037
Source: Jambo TV

Soma pia Pre GE2025 - RC Mbeya atoa TSh 5 Milioni kwa atakayetoa taarifa za Mdude, aagiza Polisi kuwasaka waliomteka
Kama marafiki wa Mdude mwambieni awe na akili. Akijifanya mjuaji na kutukanatukana watu,atabaki anatafutwa kama Saatisa!
 
mkuu, amani na utulivu uliopo ni manmade, haujaja byitself, unaona wale kule wamebadili mwenyekiti wameparanganyika
Duh!
Nilisema sitahitaji kuendeleza majibizano; lakini ulicho andika hapo juu kunakunyesha wazi wewe ni mtu wa aina gani; na naona nimalizie tu kwa haya machache:

1. Uko sahihi kabisa, unaposema "amani na utulivu uliopo ni man made; haujaja byitself". Natamani sana ungeelewa umuhimu wa hayo maneno na kuuelewa sawasawa, na isiwe kuyasema tu.
Lakini sina hakika kama unaelewa vizuri maana yake
Utulivu hauwezi kuwepo kwa njia za mabavu. Unaposema: man made usije ukafikiri utulivu unakuwepo kwa kuwakandamiza watu watulie. Hapana. Huwezi kupata utulivu kwa njia hiyo
Man made; yes; kwa kuhakikisha kuwa kunakuwepo na haki katika jamii husika. Huwezi ku-enforce utulivu. Wape watu HAKI na UHURU, utapata utulivu.

2. "...unaona wale kule wamebadili mwenyekiti wameparaganyika"? Wrong!
CHADEMA hawaparaganyiki kwa kuwachagua viongozi wao kwa uhuru na HAKI. Wanaotafuta kuwaparaganyisha CHADEMA toka nje ndio wanapigana juu chini iwe hivyo; na wanajulikana ni nani hao. Ni viongozi wa CCM wasiotaka HAKI ya wananchi wa Tanzania wafanye uchaguzi huru na HAKI kama walivyofanya CHADEMA. Hao ndio wanawaparaganyisha CHADEMA.
Bila ya mkono wa CCM, CHADEMA sasa hivi kungekuwa shwari kabisa. Hivi unafikiri ndani ya CCM kuna UTULIVU? Man made UTULIVU? Huo ni utulivu wa kimaslahi tu, tena ni wa muda mfupi sana.
Mwalimu Nyerere na wenzake walijitahidi kuweka misingi ya UTULIVU (manmade); ambao sasa unabomolewa na warithi wake ndani ya CCM hiyo hiyo.

Kwa hiyo, kwa maneno yako machache hayo uliyo andika hapo, umezidi kujitambulisha vizuri zaidi unako simamia wewe kama wewe.
Lakini nimalize kwa kusema kuwa binafsi nisingekuwa na tatizo kubwa na wewe kwa uamini wako tu wa hayo maneno hapo juu.
Tatizo lako na baadhi ya wenzio ninaowasoma humu, siyo swala la ukinzani wa kisiasa tu unao wafanya muonekane tofauti zaidi na waTanzania wenzenu wengi. Mnaweka maswala ya imani zenu kuwa mbele zaidi ya uTanzania wenu; hili pekee ndilo tatizo nililo nalo kwenu.

Nimemalizana nawe mkuu. Sina la ziada.
 
Hujui lolote wewe!

Unasema wakati wa Nyerere kulikuwa na utulivu? Unawajua wakina Kambona, Tuntemeke Sanga na yule Mnyamwezi, Kaselabantu ambaye alikaa kizuizini mpaka akaja kutolewa na Mwinyi? Just to mention few tena wakati huo vyama vya siasa ilikuwa marufuku.

Nyerere amekoswakoswa kupinduliwa zaidi ya mara tatu wakati mwingine jaribu kusoma historia ya nchi yako siyo kubwabwaja tu kama zuzu.
 
Hayo pekee ndiyo unayoyajuwa kuhusu UTULIVU wa nchi tokea uhuru?
Wewe ni kati ya watu nisiokuwa na muda wa kueleza chochote, kwa sababu akili imegota tokea mwanzo. Hata ukielezwa jambo lililo wazi akili yako inalazimisha liwe tofauti na lilivyo elezwa. Hii bangi ya dini vichwani mwenu imewaathiri vibaya.
Mimi siwezi kukusaidia kuhusu hilo, ni wewe mwenyewe kuamua.
 
Halipo kosa nchi hii kwenye katiba na Sheria za nchi yetu zinazoruhusu mtuhumiwa kupotezwa bila kupelekwa Mahakamani.

Na Waziri husika, IGP wangekuwa na uwajibikaji, wangeshajiuzulu kwa matukio haya ya watu kupotezwa bila kupelekwa court.

Na kwa kuwa damu ya mtu ni nzito kuliko maji,

Na kwa kuwa damu ya mtu huongea na kupaza sauti kudai kisasi kwa waliohusika kufanya hujuma dhidi yake,

Damu hiyo ipige kelele huko iliko na ikibidi wahusika walazimishwe na damu hiyo kusema Nini kilifanyika.

Mwisho, wananchi tunamtaka Mdude Nyangali akiwa hai, maana haki ya KUISHI ni haki ya kikatiba ipasayo kulindwa.

Na alaaniwe aliyehusika kumwaga damu ya mtu yeyote asiye na hatia.

Mungu ibariki nchi YANGU nzuri niipendayo Tanzania 🇹🇿.
 
Back
Top Bottom