Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,440
- 1,029
Mpitanjia mmoja alimkuta mvuvi kakaa chini ya mti akipumzika huku akiwatazama wavuvi wengine wakiendelea na kazi,mazungumzo yakawa kama ifuatavyo; (MPITANJIA):We mvuvi acha uvivu,nenda kafanye kazi! (MVUVI):Nifanye kazi ili iweje? (MPITANJIA):Upate pesa nyingi! (MVUVI):Na hizo pesa zitanisaidia nini? (MPITANJIA):Utanunua boti yenye injini,utapata samaki wengi zaidi,utapata pesa nyingi zaidi na utanunua boti nyingi zaidi. (MVUVI):Na hizo boti zitanifaa nini? (MPITANJIA):Utaajili wafanyakazi wengi halafu wewe utakaa chini ya mti ukipumzika na kuwatazama wakikufanyia kazi yako! (MVUVI):Kumbe mwisho wa yote ni kukaa chini ya mti na kupumzika,kwani hapa umenikuta nafanya nini?