Siku tulipokutana na kundi la samaki baharini

LA7

JF-Expert Member
Aug 26, 2019
457
1,746
Habari za humu wanajamii

Leo nimekumbuka kisa kimoja kilitutokea baharini, tukiwa na boti ndogo ya kubeba wastani wavuvi 15 kwa ajili ya kuvua samaki

Safari yetu siku hiyo ilianzia soko la feri mpaka kisiwa cha bongoyo mashariki yake kama km 10 hivi,

Kama kawaida tulipofika tunaanza maandalizi ya kupanga nyavu tukashusha dingi kwa jina lingine sijui,

Ni kiboti kidogo ambacho hukaa mtu mmoja na jenereta kwa ajili ya kuwasha taa zinakuwa pembezoni ubavuni na kumulika kwenye maji,

Basi giza ilipoingia tukamwachia jamaa wa dingi anakuwa nyuma yetu tukiwa tumefunga kamba ndefu,

Tukalala kama kawaida, ilipofika saa 7 usiku jamaa akatuamsha na kutuambia tuzungushe nyavu, takazungusha nyavu kama kawaida na kuanza kuipandisha juu,

Ebwanaee nyavu ilikuwa nzito hatari yaani utafikiri ni kama ilinasa chini basi bhana vuta vuta baada ya nyavu kuzidi kuwa karibu tulishangaa sana kwani kulkuwa na mzigo wa maana ndani yake kulikuwa na samaki wakubwa aina ya songolo ambao baadae walichana nyavu na kutoka,

Lakini mzigo ukawa bado tu umetushinda kunyanyua kwani boti ililalia ubavuni tunakopandishia nyavu,

Ilibidi tuanze kuwachota kidogo kidogo na kumiminia kwenye boti boti ilijaa mpaka tukavitupa vile viroba vya mchanga tunawekaga kwa nyuma kwa ajili ya boti kubalansi kwa nyuma,

Baada ya kujaza ilibidi tuwamwage tu haodagaa waliobakia kwani boti ilizidiwa na mzigo,

Basi saa 11 asubuhi tukawa tumewasili sokoni feri tukawa tu tumelala tukisubiri soko lianze asubuhi saa 12 hadi saa 1 siku hiyo ndoo moja ya dagaa ilicheza kwenye 30 hivo tuliuza dagaa wote na tulikuwa zaidi ya 16 kila mvuvi alipata 90 mimi kwasababu nilikuwa mdogo kushinda wote nilipewa 50,

Kwenye mgawo wa pesa kuna makato mengi sana hivo baada ya hayo makato ndo kila mtu akala hiyo 90 makato yenyewe ni haya hapa,

Boss
Nyavu
Boti
Mashine
Jenereta
Taa
Mashine/engine

Inayobaki ndo mnagawana,

Basi siku hiyo soko sisi ndo tulifungua na kufunga

Kama kawaida ilipofika ile saa kumi jioni muda wa kuondoka tulishangaa boti nyingi zikitegea kuondoka mpaka inafika saa moja hakuna boti inaondoka ikabidi tu tuanze kuondoka na kuelekea pa jana

Tulipofika tu na kutosa nanga tulizungukwa na boti za kutosha kila mahali ni taa tu,

Mpka kesho sikumbuki kama kuna boti ambayo ilipata ndoo zaidi ya 10,

Pia nilijifunza wavuvi ni watu wenye maisha magumu sana kwani katika watu 10 ni mvuvi 1 tu ndo unaweza kuta ana maisha ya kueleweka pia ushirikina kwa sana tu

Na pia asilimia kubwa ya wavuvi walikuwa ni wateja wa wale wanawake wanajiuza msasani mwananyamala na kigamboni

Kazi ya mvuvi kwa tanzania haina maslahi kwa wavuvi bali kwa boss au mmiliki wa boti

Fikiria tu mwezi ukiwaka wavuvi wa usiku kwao ni taabu kwani samaki hawafuati tena mwanga, wenyewe huita mwezi mchanga,

Ni kazi isiyo na uhakika kabisa sababu hawana vifaa vya kisasa vya kupatia samaki kwani siku nyingine boss huingia mfukoni na kutoa pesa kwa ajili ya mafuta,

Ni kazi ngumu kwani jua lao mvua yao.
 
Katika harakati zenu hujawahi kwenda mafia, Kigombe, Kipumbwi na Mkwaja, kazi ya uvuvi ni moja ya kazi ngumu sana na maslahi kidogo sana kwa mabaharia.
 
Uvuvi ni kada ngumu sana sana lakini ndo inatuletea vitoweo maridhawa.

Laiti idara za tafiti vyuo vikuu zingekuwa zinafanyakazi kwa ukaribu na wavuvi basi nchi yetu ingekuwa mbali sana kwenye aina ya samaki waliopotea....
 
Wao wanajua Samaki wapo wa kutosha kinachofanyika ni kuwafunika Watanzania wasijue mali zao ili iwe rahisi kuwapa meli za nje kuvua kwa vibali magumashi na wachache kupata pesa rejea samaki wa Magufuri...
 
Ni kweli kazi ngumu ila wavuvi wengi wanamatumiz mabaya sana ya pesa

Story yako inaonyesha siku hyo mlipata 90,000/- one night na wew 50,000/- ni pesa nzuri ukiamua ujikwamue kwa mwak mmoja unajenga na kumilk gari nzuri
 
Back
Top Bottom