Mvuvi ajinasua kinywani mwa kiboko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mvuvi ajinasua kinywani mwa kiboko

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jun 23, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  James Magai
  MVUVI wa samaki katika kijiji cha Butata kata ya Bukima Wilayani Msoma Vijijini mkoani Mara, Stephano Mboyi amenusurika kutafunwa na mnyama aina ya kiboko, baada ya kupambana naye ana kwa ana na kumshinda maarifa.


  Tukio hilo ambalo kwa kadri Mboyi mwenyewe alivyolisimulia lilionekana kama ni filamu ya kusisimua ya mpambano baina yake na mnyama huyo hatari lilitokea Jumatatu majira ya saa moja za usiku ziwani.
  Akiongea na Mwananchi kwa njia ya simu kutokea katika Hospitali ya Murangi alikolazwa kwa matibabu baada ya kujeruhiwa na mnyama huyo wakati wa pambano hilo, Mboyi alisema alikumbana na tukio hilo wakati akifanya shughuli zake za uvuvi.


  “Nilikuwa nimekwenda kutega mtego (nyavu) wangu wa kwa ajili ya samaki aina ya furu. Baada ya kumaliza kuuzungusha, nilianza kuwafukuza samaki kuelekea kwenye mgeto;


  “Ghafla nikasikia maji yakifoka kunifuata, nikajua huyo ni kiboko nimeshapatikana. Hivyo ilinibidi nizame ndani ya maji ili nikimbie kando lakini kiboko akataka kunikanyaga, bahati nzuri nikawahi kupita miguuni mwake na nikaenda mbele,” alisema Mboyi.


  Aliongeza kuwa wakati anatapatapa akitafuta namna ya kukimbia kutoka ndani ya maji mara kiboko huyo akamsukuma akaanguka na akataka kumkamata mgongoni lakini akakwepa na kuamua kukimbilia kwenye maji marefu.


  Aliendelea kusimulia kuwa kiboko huyo alimfuata tena na katika harakati za kupambana naye mara kiiboko akaudaka mkono wake wa kushoto na kuingiza mdomoni mwake.
  “Baada ya mkono kuingia mdomoni aliachama zaidi ili anikamate kichwani na kisha anitafune lakini nikamshika kidevu nikamsukuma nikauchomoa haraka mkono wangu kisha nikazama majini,” alieleza Mboyi.


  Alisema hatua ya kuzama majini ndiyo iliyokuwa ikimsaidia hivyo aliendelea kuhangaishana na kiboko huyo hata baada ya kuweza kuudaka mkono wake katika kinywa chake kama mara tatu hivi lakini alifanikiwa kujinasua kabla hajatafunwa.


  Mboyi alisema kuwa wakati akiendelea kupambana na kiboko huyo watu wakafika ziwani hapo wakiwa na tochi baada ya kusikia kelele.


  Alisema yule kiboko alipoona ule mwanga wa tochi, alimwacha yeye kisha akawatisha kuwafukuza wale watu waliokuwa na tochi nao wakakimbia na kisha akamrudia tena na kuanza kusumbuana.Hata hivyo wale watu walirudi tena na kutumia mwanga mkali kummulika kiboko huyo ambapo mara hiyo sasa yule kiboko alimuacha, akasogea nyuma kidogo kisha likawatisha tena kuwafukuza.


  Alieleza kuwa hapo ndipo alipopata nafasi ya kukimbia hadi ufukweni upande mwingine, ambapo alikimbia na kiboko huyo kuanza kumfukuzatena, ambapo baada ya mwendo mfupi alianguka ndipo alipobaini kuwa alikuwa amesharudi kwenye maji.


  Aliongeza kuwa baada ya hapo ndipo wale watu waliokuwa na tochi walipomfuata na kumchukua na kisha kumpeleka hospitali.


  Hata hivyo alisema kuwa katika pambano hilo aliweza kupata majeraha katika mkono wake wa kushoto tu ambao kiboko huyo alikuwa akiudaoa na kuuingiza kinywani mwake, wakati wa harakati za kujinasua kuutoa mdomoni mwake.

  http://www.mwananchi.co.tz/habari/3-habari-za-mikoani/24102-mvuvi-ajinasua-kinywani-mwa-kiboko
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  siku hizi hawa viboko wamekuwa dhaifu sana...
   
 3. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  kama mkuu wa nchi ni dhaifu tutegemee nini? Pole sana bwana Mboyi get well soon!
   
 4. Mr. Bigman

  Mr. Bigman JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,848
  Likes Received: 627
  Trophy Points: 280
  Hivi udhaifu ni tusi? Naogopa kuchezea ban.
   
 5. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  una maanisha kama ingekuwa wakati ule enzi za mwalimu huyu jamaa asingepona?
   
 6. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,575
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  pole yake ndugu mvuvi kwa mkasa uliomkuta ila anaposema alimshika kidevu akamsukuma nitakubaliana na Kigogo kuwa siku hizi viboko nao ni dhaifu, anyway! alijitahidi kuokoa uhai wake usipokonywe na kiboko.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  ni tusi kwa watu legelege..
   
 8. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  ha ha haaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 9. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #9
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  kama baba mwanariz1
   
 10. Kisusi Mohammed

  Kisusi Mohammed JF-Expert Member

  #10
  Jun 23, 2012
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 442
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Ukitaka kula lazima uliwe! Pole mvuvi, hii ni dunia ya "survival for the fittest"
   
 11. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #11
  Jun 23, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Heri mimi sikusema
   
 12. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #12
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  Duuh hawa jamaa wa Musoma ni hatari sana. Imagine ingekuwa Huyo kiboko angepambana na mpemba hivi...."Wallah we kiboko wanila hivi hivi yakheee..toba mieeeee naliwa(accent ya kipemba). No offence to jamaa zangu wapemba.
   
 13. nsangaman

  nsangaman JF-Expert Member

  #13
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kiboko ni mla majani siyo nyama
   
 14. G

  GTesha JF-Expert Member

  #14
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 203
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mnamanenoo!
   
 15. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #15
  Jun 23, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Pombekali ndio kusema kawaambuliza mpaka viboko?......lol
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #16
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  Kuna takwimu nyingi zinaonyesha watu waliopoteza maisha kutokana na kiboko. Kama huamini mkuu nenda kamlishe hayo majani,halafu urudi kutujuza yaliyojiri.
   
 17. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #17
  Jun 23, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hahahahahahaha lol..
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Huyo kiboko alikuwa na hesabu "0".
   
Loading...