Mvuto wa Magufuli kwa Upinzani: Mbunge wa Ndanda (CHADEMA), Cecil Mwambe anadi Ilani ya CCM bungeni

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
cecil mwambe.jpg

Mbunge wa Ndanda kwa tiketi ya CHADEMA, Cecil Mwambe akiwa bungeni ameshikilia Kitabu cha Ilani ya CCM. Hii ni dalili njema kuwa, aliyoyafanya Rais Magufuli hasa ununuzi wa korosho, ni kibali kikubwa sana cha wananchi wa Jimbo la Ndanda mkoani Mtwara kwa Magufuli.

In fact, that's is an endorsement to the Omuzilankende!!
Ni fire...🔥🔥🔥.
 
kama ulisoma utakuwa ulifaulu kwa kuiba mitihani yako. habari ni nn hapo?
Kama ukitongoza mwanamke kwa kumdanganya akakupenda lakini wewe ukamtongoza mwanamke na kumwanikia ukweli wako akakushit, nani mwenye akili?
Kudai nimeiba Mtihani ndiyo nini? Inaonekana wewe uliishia form IV ndiyo maana unaongelea kuibia Mtihani, otherwise kama kuna mtu huwa anaibia mitihani kuanzia wa Darasa la VII, Form IV, Form VI na Chuo Kikuu, utamwitaje huyo kilaza? Huyo ujue ana akili sana, haiwezekani mtu kila mtihani aibie na kushinda huyo ni shujaa.

Bahati mbaya ni kuwa wewe ambaye ulikuwa unashinda mitihani bila kuibia haujawahi kupata namba 5 darasani, achilia mbali namba moja. So sorry mzee maana umeangukia wrong number.
You're dealing with something bigger than US Open - Bow wow.
 
KWAHIYO UNADHIHIRISHA ULE USEMI KUWA SASA HIVI CCM IMEISHIWA WATU WAELEWA HADI WAPINZANI WANAWASAIDIA KUNADI ILANI YENU
 
Anadhani atapewa Unaibu Waziri, au ndio analazimisha anunuliwe baada ya kuona CCM hawajamfata jimboni kwake, kama wenzake.

Kachelewa,
 
View attachment 933182

Mbunge wa Ndanda kwa tiketi ya CHADEMA, Cecil Mwambe akiwa bungeni ameshikilia Kitabu cha Ilani ya CCM. Hii ni dalili njema kuwa, aliyoyafanya Rais Magufuli hasa ununuzi wa korosho, ni kibali kikubwa sana cha wananchi wa Jimbo la Ndanda mkoani Mtwara kwa Magufuli.
In fact, that's is an endorsement to the Omuzilankende!!
Ni fire...🔥🔥🔥.
Mbunge yeyote yule awe wa Chama Tawala au Upinzani anatakiwa kuwa na sifa mbili - kuisifu Serikali pale inapofanya vizuri; na kuikosoa pale inapofanya vibaya. Kitendo cha Mbunge kuonekana na Ilani ya Chama tofuati na chake sio kosa, huenda anataka kuitumia katika kuipongeza Serikali au kuikosoa. Ili kumuunga mkono Mhe. Rais, washaurini Wabunge wote bila kujali itikadi wafanye kazi za Kibunge badala ya kazi za Uenezi wa vyama vyao; wasiunge mkono kila kitu na wasipinge kila kitu - mazuri wayaunge mkono na mabaya wayapinge. Kama wakiunga mkono mazuri, hata siku wakipinga mabaya kila mtu atawaona wa maana.
 
Tuache mawazi potofu Mbunge kutumia ilani ya chama tawala.Si dhambi ni wajibu.
 
Back
Top Bottom