Mvutano waibuka kati ya Kikwete na Magufuli juu ya ukatibu wa bunge, asita kuachia madaraka

How and Why? JK and his team had their time, sasa wameshamaliza they should kick out. Haya mambo ya kuweka warithi kwani JK marahii ameshasahau nini kilichotokea walipotaka kumchomeka Membe?
JK hata kama kastahafu bado atawasumbua kuliko Mwenyekiti yeyote aliyepita kwani kwa kitendo cha kudhamiria mke na watoto kuwachomeka kwenye nafasi ndani ya chama kitamtesa sana.
Hawezi kukubali heshima yake ishuke kwa watu wake hao waondolewe kwa kupigwa chini kwa kura, ataendelea kuingilia ili asipate aibu hiyo
 
Mtoto Wa kiume kuwa na chuki za waziwazi kwa mwanaume mwenzio ni mbaya hata shetan anakushangaa, ovyoo kabisa

Shetani anatakiwa amshangae Kikwete kwasababu katika maisha yake yote anaangalia sana hisia zake zinavyomtuma badala ya kuangalia hisia za walio wengi. CCM tumempata Magufuli ambaye haangalii sura ya mtu wa hisia zake ila utendaji kazi wa mtu, kwanini tubaki na Jk? Huwezi ukaongoza nchi kwa kujali sana hisia na matamanio yako tu. Nchi hii ni ya wote, lakini yeye alihisi tumeibinafsisha Tanzania kwenye familia yake na hisia zake kwa miaka kumi. Share on him!!!!

Kwa hiyo unataka Mkristo? Kumbe ubaya wa JK sababu alikuwa Muislam.

Si kwamba nataka Mkristo bali mchapakazi, atakayekiwakilisha chama vizuri. Huyu Chatanda si ndiye aliyetuvuruga sana kule Arusha na Tanga huyu? Ana mtaka wa nini kwa kipya kipi alichonacho?

JK alipenda sana kujitanabaisha uislamu wake katika utawala wa awamu ya nne bila kuangalia kuwa nchi hii haina dini wala haipaswi kuongozwa kwa kufuata dini yoyote.

Mimi namchukia sana mtu ambaye anaegemea dini yake, kabila lake, rangi yake katika utawala wa aina yoyote katika utumishi wa umma.
 
Watu wanatetea maslahi yao, lakini hali inavyooneka,Jk lazima atafute watu watakaolinda maslahi yake, maana hii ndio ticket pekee iliyobaki kwake kuweza kuukabili mfumo mpya. Maana zile loopholes zilizokuwa zimewekwa ili watu wauchezee mfumo zimetolewa, na watu waliokuwa wanafanya makosa wanaoneka.Kila jambo sasa linajulikana limeanzishwa na nani.Makosa mengi yametokea kwa uzembe au makusidi fulani, sasa watu wa kukulinda lazima.
 
mbona hakuna mvutano wowote, Inawezekana huyo aliyekupatia taarifa kakosea na wewe ukakosea nawe ,pole yako mkuu chama kipo imara sana

Kweli inawezekana kapata taarifa zisizo na ukweli naye akazirusha hivyo bila ukweli. Lakini kwa upande mwingine umeona lini Chama cha mapinduzi kukubali mavalangati yao yawe hadharani. Huwa kitabia nakifananisha hicho chama na mwanamke mfukunuku kitaani, ya wenzie anashadadia na kuyaanika kila kinachotokea kwenye ndoa au kwa majirani zake zinakuwa hadharani, lakini ngoja zikimpata yeye anapiga kimya na hodari kukanusha
 
Shetani anatakiwa amshangae Kikwete kwasababu katika maisha yake yote anaangalia sana hisia zake zinavyomtuma badala ya kuangalia hisia za walio wengi. CCM tumempata Magufuli ambaye haangalii sura ya mtu wa hisia zake ila utendaji kazi wa mtu, kwanini tubaki na Jk? Huwezi ukaongoza nchi kwa kujali sana hisia na matamanio yako tu. Nchi hii ni ya wote, lakini yeye alihisi tumeibinafsisha Tanzania kwenye familia yake na hisia zake kwa miaka kumi. Share on him!!!!

Si kwamba nataka Mkristo bali mchapakazi, atakayekiwakilisha chama vizuri. Huyu Chatanda si ndiye aliyetuvuruga sana kule Arusha na Tanga huyu? Ana mtaka wa nini kwa kipya kipi alichonacho?

JK alipenda sana kujitanabaisha uislamu wake katika utawala wa awamu ya nne bila kuangalia kuwa nchi hii haina dini wala haipaswi kuongozwa kwa kufuata dini yoyote.

Mimi namchukia sana mtu ambaye anaegemea dini yake, kabila lake, rangi yake katika utawala wa aina yoyote katika utumishi wa umma.
Ooooh Unatia huruma sana Jk ni rais mstaafu na ni mwenyekiti Wa chama chako CCM kwa lugha nyingine ni bosi wako mpuuzi wewe,

Humtaki kunywa sumu ufe, lkn chuki zako kwake hazitosaidia kitu, Jk ni rais bora kuwahi tokea Tanganyika, watanzania tuna jua na dunia inajua, ndio sababu bado anang'ara kimataifa, moyo wako unashuhudia hapo ulipo, acha unafiki na majungu aliyepata kapata, huna haya kweli wewe
 
JK aondoke tu hatumtaki. Katuharibia chama yeye na familia yake. Huyu naye wa nini? Atimuke tu na uislamu wake. Ukiangalia sana kwenye chaguo lake la Mama Chatanda au Ulega kuna mchepuko au uislamu tu. Chunguzeni sana mtaona.

Toa hoja vizuri kaka huku ukiacha mbali hoja zenye muelekeo wa kidini
 
Tunajali zaidi kwa yale yanayoendelea ndani ya serikali si ndani ya CCM.
 
Mm naona chadema kimepoteza mvuto kwa wanaunch kwahiyo kijitaidi kutafuta jinsi ya kurudisha hadhi yao ya kabla ya mwaka 2015 sio kusumbuana na vikao vya cc vya ccm wakija kushtuka itakuwa too late kama ccm imeweza kuimili mpepo mbaya wa kisiasa iweje hizi cheap propaganda za sijui kikao kumekuaje, sijui kinana na jk imekuaje
 
Ndugu zangu wana JF tayari kuna msuguano mkubwa umeibuka ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) baina ya katibu mkuu Kinana na mwenyekiti JK chanzo kikitajwa kuwa ni nafasi ya ukatibu mkuu wa bunge wa chama cha mapinduzi.

Hii ni baada ya kuibuka mvutano mkubwa mwingine baina ya Mh RAIS JPM NA JK kwakuwa kila mmoja kuwa na chaguo lake.Huku JPM akitaka Mh Rweikiza ndio awe katibu na JK akitaka awe kati ya mama Chatanda ama Mh Ulega

Kutokana na mvutano huo uliojitokeza Katika kikao hicho kilichofanyika jana Mh JK kasita kutangaza siku ya Mkutano Mkuu Maalum wa kuachia madaraka ya Uenyekiti

Kutoka kwa vyanzo vya ndani ya CC jana walikua na ajenda ya tarehe ya mkutano mkuu ila kabla ya mkutano kuanza ndio kilifanyika kikao kidogo likichohudhuriwa na watu 4 ambao ni JK,MAGU,MAMA SAMIA NA KINANA.

Na ndipo baada baada ya kikao hicho JK alirudi kuondoa ajenda hiyo kwa hoja kuwa ilikuwa haijaandaliwa vizuri na kuahirisha kikao cha CC.

Sasa kikao cha Baraza la wazee kitaitwa katika siku chache zijazo ili kumlazimisha JK kuacha.
Ally Ngomanzito tulia na kisha fikiria then andika, badiko lako linaweza kuwa na mantiki lakini halieleweki na kichwa cha habari hakina uwiano na content kabisa
 
Mm naona chadema kimepoteza mvuto kwa wanaunch kwahiyo kijitaidi kutafuta jinsi ya kurudisha hadhi yao ya kabla ya mwaka 2015 sio kusumbuana na vikao vya cc vya ccm wakija kushtuka itakuwa too late kama ccm imeweza kuimili mpepo mbaya wa kisiasa iweje hizi cheap propaganda za sijui kikao kumekuaje, sijui kinana na jk imekuaje
Oooooh ona sasa, mkiambiwa bangi mbaya hamtaki chadema walikuwapo kwenye hicho kikao? Acha bangi naona uchizi unakusogelea
 
Kwa hiyo huo mvutano mkubwa umeisha baada ya JK kuondoa hiyo agenda?

Teh teh teh
Hahahahaha naona unaongea kwa unyonge kweli, tuambie basi sababu za CC kuvunjika jana
 
Labda ujasoma vizuri sijasema chadema walikuwepo kwenye kikao sa mm na ww nani bangi
 
CCM hawajifunzi sijui kwann, wangemtumia Jk vizuri kwa kipindi hiki hata kumuongezea muda hata miezi sita ikiwezekana,
 
Back
Top Bottom