Mvutano waibuka kati ya Kikwete na Magufuli juu ya ukatibu wa bunge, asita kuachia madaraka

Kwa mujibu wa taarifa rasmi za Team Membe:

Membe ilikuwa awe Rais kwani ndiye aliyekuwa chaguo la Mwenyekiti wa CCM. Membe alishaandaa mabasi yake branded kama 'Presumptive Nominee" wa CCM (2015). Mabasi haya yalikuwa yanaoshwa na kuandaliwa Masaki tayari kwa safari ya Dodoma, na wananchi wengi waliyaona. Team Membe ilishaandaa mkakati wa muda mrefu wa kupitia NEC hasa kutokana na kujiridhisha kwamba wafuasi wa Lowassa ndani ya NEC watasusa na kutoka nje ya kikao baada ya jina la Lowassa kukatwa. Watakaobakia watampigia kura Membe. Dakika ya mwisho, mkakati ukabadilika, hivyo historia kubadilika. Chaguo la Kikwete (Membe) safari yake ikaishia ukingoni pale wajumbe wa NEC (loyal to Lowassa) walipoamua kubaki ndani ya kikao kwa nia ya kumzuia Membe na Makamba. Kazi hiyo ikafanikiwa. Mabasi ya Membe ambayo yalishaanza safari alfajiri ya siku hiyo kuelekea Dodoma ikabidi yachepuke porini njiani baada ya taarifa kwamba team Lowassa ndani ya NEC imejipanga kumchinjilia mbali Membe na Makamba.

Kwa sasa historia inaandikwa upande mmoja tu kwamba - Kikwete alimzuia Lowassa asiwe mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM, hivyo asiwe Rais wa Tano wa JMT.

Lakini makabrasha yote yakishakaa sawa, historia itasema pia kwamba:
1. Lowassa alimchinjilia mbali mgombea wa JK (Membe).
2. Magufuli alipita kuwa mgombea na hatimaye kuwa Rais kutokana na kuungwa mkono na wajumbe wa NEC waliokuwa loyal kwa Lowassa.

Maudhui ya uzi huu ni sehemu ya uandikaji upya wa historia hiyo.

Sioni tatizo kujadili haya kwani ni maslahi ya CCM, sio ya "Taifa".

hahahahahaha endelea kujidanganya na hekaya zako za kutunga, lile dubwana lilikatwa na halikuwa na nguvu yoyote, unapojidanganya hapa Hao wafuasi wa Lowassa waliobaki kupiga kura kwanini wasingempigia kura mgombea dhaifu Makamba akashinda halafu bosi wao akajakushinda urais kilaini akiwa na CDM, Maana kwenye kinyang'anyiro ingekuwa MAKAMBA (CCM) VS LOWASSA (CDM) lowassa hapa angeshinda kilaini kabisa maana hata mimi nisingepiga kura.
Ukweli ni kwamba JK ndiye mshindi wa ule mpambano, LOWASSA fitina na mbinu za kimafia alikuwa hazijui bali yeye alijikita kugawa fedha kwa kila anayekuja mbele. Kumbuka kauli za JK kwenye kampeni " hachaguliwi mtu kwa ujivuni wake wa fedha" Jiulize pia heshima ya Magu kwa JK inatoka wapi?
 
...hivi, hicho kikao cha hawa jamaa kinachotumia bilioni mbili ni cha siku 100 au?!....
 
Naona huu uongozi wa media ukififia ukingoni. Yani hawa CCM sijui wamepigwa upofu na nani!? Magu nchi inakaribia kumshinda afu wanataka kumbambikizia zigo lingine la lichama.
Any way wahenga walisema "Mbio za sakafuni huishia...................."
 
Tulitegemea kabisa! JK anaona sasa nguvu zote zinachukuliwa na hana pa kujificha na anajua dhambi ya unafiki itamuandama! Haina jinsi ni sawa na jogoo awike asiwike kutakucha tu! Nguvu ni suala la muda na mpito! Aachie madaraka na kupumzika! Kama kuna makando kando yake ajiandae tu kuyakabili! Mwaka huu tutasikia na kuyaona mengi
 
JK aondoke tu hatumtaki. Katuharibia chama yeye na familia yake. Huyu naye wa nini? Atimuke tu na uislamu wake. Ukiangalia sana kwenye chaguo lake la Mama Chatanda au Ulega kuna mchepuko au uislamu tu. Chunguzeni sana mtaona.
Wewe chunga mdomo wako mchafu
 
Kikwete ajipumzikie tu, chama atakiacha tu, iwe June mwaka huu, ama Octoba mwakani!!
we unadhani jk ana usongo sana na kuendelea na umwenyekiti?,

na wala usidhani kuwa magufuli nae ana moto sana wa kuupokea huo umwenyekiti.

Na pia usidhani kuwa jk ataathirika kwa lolote pindi atapoachia uenyekiti.

Mengine haya ni hekaya za hawa Bavicha tu kwa ajili ya kupass time vijiweni
 
Back
Top Bottom