Robert Mugabe ameondoka. maandiko yametimia: Kila nafsi itaonja mauti.
Pamoja na kuondoka kwake maswali ni mengi yamebaki. Moja ya maswali ni kisa cha mauaji ya mvua za vuli.
Mapema miaka ya ‘80 wakati uhuru wa zimbambwe ukiwa katika uchanga wake kulikuwa na fukuto miongoni mwa washona kabila la robert na wandebele, kabila la nkomo. Robert na Nkomo walipambana kwa pamoja kuupigania uhuru wa Zimbabwe na baada ya kuwa umepatikana, Robert alipata kuwa waziri mkuu wa nchi kufuatia kupata wingi wa viti vya bunge. Nkomo akawa waziri muandamizi.
Pamoja na hayo na kama ilivyo kwa viongozi wengi wa kiafrika, robert hakuwa akijiamini. Alikuwa na hofu kubwa kuwa nkomo anataka kumpindua. Kuona hivyo robert akaamua kujihami na moja ya mkakati ulikuwa ni huu ulioitwa mvua za vuli. Mvua zenye tabia ya kusafisha mashamba kwa ajili ya kuiandaa ardhi na kilimo. Mvua hizi zikinasibishwa na uhuru wa zimbabwe wakati huo kwamba sasa tumepata uhuru basi na tuondoe au tuzime upinzani wa aina yoyote tutawale tukavyo.
Waskari wa kikosi cha 5 waliokuwa wamepata mafunzo Korea Kaskazini walitekeleza mauaji ya wandebele zaidi ya kati ya 20,000 na 80,000. Inasemekana walitumwa na mugabe japo hakuwahi kukiri lakini kuna siku akiomboleza kifo cha nkomo alitamka maneno ambayo hakuwahi kuyarudia tena wala kutoa ufafanuzi wake kwamba mauaji ya mvua za vuli kilikuwa ni ‘kipindi cha wazimu’.
Kwa uzalendo tunao brainwash-iwa juu ya Robert Mugabe alipaswa kufia kwenye hospitali za Zimbabwe aliyokuwa anadai kuipigania maslahi yale ila sasa kafia kwa mabeberu. Wazimbabwe ni hoi bin taaban kiuchumi. Itoshe tu kusema tu kuwa Robert siyo mwanamapinduzi kama tunavyo brainwash-iwa. Alikuwa ni muuaji mwingine tu kama walivyo wauwaji wengine na alitakiwa akumbane na mkono wa sheria.
je, Wandebele walimsamehe?