USSR
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 9,896
- 22,666
Leo nikiwa napita maeneo mbalimbali nikitokea Dodoma hadi nafika Dar es Salaam naona watoto wadogo njiani wakiwa wameshika viatu huku wakitembea kwenye njia zilizojaa maji, wakinyeshewa, wakiloanishiwa madaftari na vitabu huku wakionesha kujuta kuzaliwa katika jamii iliyo na roho ngumu isiyojali hatari ya usalama wa watoto.
Kuna maeneo barabara zimefunikwa na maji, madaraja yamejaaa maji hupita juu ya maji. Kuna watoto walio upande wa pili wa mito, mabonde na mabwawa ya misimu ya maji sasa yamejaa watoto wanalazimika kuvuka ili waende shule.
Nilidhani kuwa zile kelele za El nino zilizingatia na usalama wa watoto wetu hasa miji mikubwa ambapo usafiri sasa ni kero sana.
Serikali isisubiri mpaka watoto hawa wafe au kupata madhara ndio eti waje kuchukua hatua za kuzuia huku tumeambiwa mvua bado zipo sana tu tena kubwa.
Note: Mimi nikiwa mzazi ninajali usalama wa watoto wagu nimezuia wasiende shule (japo huijiwa na gari la shule) mpaka hapo mvua hizo za El nino zitakapokoma.