Mvi kuota mapema. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mvi kuota mapema.

Discussion in 'JF Doctor' started by Anthony Lawrence, Oct 31, 2012.

 1. Anthony Lawrence

  Anthony Lawrence JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,544
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Siku hizi limekuwa ni jambo la kawaida kuwaona vijana kuanzia miaka 24 wakiwa na mvi kichwani. Asili inatuonyesha kwamba watu wanaoota mvi ni wazee. Je, kitu gani kinasababisha watu waote mvi wangali bado vijana? Naomba msaada
   
 2. ram

  ram JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,225
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Subiri wataalamu watakuja soon, wakupe majibu
   
 3. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nyingine za ukoo, mdogo wangu ako 16 na anazo....
   
 4. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Wengine wana bleach tu nywele..........ila nasikia ukipenda kuwa na wamama wenye umri zaidi yako mvi zinakuja
   
 5. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mafuta ya nywele mengi yanayotumika siku hizi ni cause pia ya mvi mapema.
   
 6. HP1

  HP1 JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 3,353
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Phenotype = genotype + environment
   
 7. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Duh!:mwaaah:
   
 8. Anthony Lawrence

  Anthony Lawrence JF-Expert Member

  #8
  Nov 1, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,544
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Sijakupata mkuu. Naomba ufafanuzi zaidi
   
 9. HP1

  HP1 JF-Expert Member

  #9
  Nov 1, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 3,353
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  phenotype ni muonekano wa nje wa kiumbe. muonekano huo unategemea sana chembe za uhai, namna ulivyochukua au kurithi kutoka kwa wazazi na vizazi mfano rangi ya ngozi, nywele, nk, pamoja na environment kwa maana ya kiumbe kinapoishi na kinavyoishi. Environment inaweza kuwa aina za vyakula, hali ya hewa nk. Kwa hiyo mvi zinaweza kurithishwa kiukoo, lakini pia vyakula. Kuna vijana wengi siku hizi wanajiingiza kwenye sigara, pombe kali, na nyingine hazijathibitishwa ubora wake. Matokeo yanaweza kuwa mengi, mojawapo ni mvi. Wengine wanaweza kuonekana wazee kuliko umri wao halisi
   
 10. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #10
  Nov 1, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mkuu Q Man,

  Nianze kwa kusema kwamba, kila unywele/nywele una sehemu mbili mzizi(root) na kishina chake(shaft).Na kila unywele huwa umejiviringa kwa vitu kama nyuzi nyuzi(strand) ambazo hujishikiza katika sehemu ya juu la fuvu la kichwa( scalp) kama follicle.

  Kila follicle huwa na seli(pigment Cells) ambazo hutoa kemikali/kichochezi cha MELANIN.Hii huipa sehemu ya pili tuionayo kishina(shaft), ukuaji na rangi yake tuionayo mfano rangi nyeusi, nyekundu, kahawia n.k.
  Ni melanin hii hii inayofanya rangi ya ngozi kuonekana jinsi ilivyo mfano(weusi, weupe, n.k).

  Sasa kwa kadri muda(miaka inavyokwenda) chembe chembe chochezi hizi(pigment cells) hupungua kwa kufa taratibu katika follicles na hivyo kusababisha kiwango cha melanin ya nywele kuwa kidogo na hivyo kufanya muonekano ule tuuonao..MVI.

  Sasa, katika kujibu swali lako kuna mambo kadhaa husababisha muonekano huo katika umri mdogo.Haya ni kama vile;

  URITHI:
  Wengi wa vijana wenye nywele za mvi, wazazi wao au wazazi wa wazazi walipata mvi pia katika umri huo(wakiwa vijana) kutokana na Genes ..seli zitoazo melanin(melanocytes) kushindwa kufanya kazi yake, na kurithiwa toka kizazi hadi kizazi(Ukoo).

  UVUTAJI SIGARA:
  Sigara huwa na kemikali iitwayo nicotine, ingawa sababu haziko wazi sana katika hili, tunahisi kuwa ni kutokana na kemikali hii kuwa katika damu kupunguza urutubishwaji wa kizizi cha unywele!

  UPUNGUFU WA MAFUTA:
  Sehemu ya juu ya fuvu la kichwa(Scalp) hutoa mafuta yaitwayo Sebum.Mafuta haya huzipa nywele mng'aro na rangi yake. Na hivyo upungufu wa mafuta haya husababisha nywele kuonekana zenye mvi.
  Upungufu wa madini ya shaba(copper),Iodine, chuma(Iron)na Vitamini(Vitamin B) husababisha upungufu wa mafuta haya.

  MAGONJWA:
  Matatizo ya kiafya mfano upungufu vichochezi(Hypothyroidism), magonjwa/hali zinazoadhiri uzalishwaji/urutibishwaji wa melanin(Vitiligo)...n.k  Matibabu:

  Cosmetic approach: Hutumia dawa kwa kupaka rangi na kupunguza muonekano wa rangi ya nywele(mvi).

  Kutumia vyakula vyenye virutubisho(nilivyotaja hapo juu) kama vile karoti, ndizi samaki, maziwa n.k
   
 11. Anthony Lawrence

  Anthony Lawrence JF-Expert Member

  #11
  Nov 1, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,544
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Asante kwa ufafanuzi, mkuu
   
 12. Anthony Lawrence

  Anthony Lawrence JF-Expert Member

  #12
  Nov 1, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,544
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Asante kwa darasa mkuu
   
 13. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #13
  Nov 1, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Karibu.
   
Loading...