Mimi binafsi si mpenzi wa muziki wa taarabu lakini nimekuwa nikiufuatilia kwa muda sasa...Kitu kinachonivutia ni lugha ya picha ambayo inavutia sana endapo mtu unapata nafasi ya kuitafakari!!
Nimejaribu kuvuta kumbukumbu zangu, na kukutana na baadhi ya miziki ambayo kweli inavutia!! Naweka hii hapa chini na natumai wadau watanisaidia kutukumbusha nyimbo nyingine na ikiwezekana kutuwekea baadhi ya mashairi na nukuu ambazo zili/zinawakuna!
1. Wrong namba
2. Y 2 K
3. Zumbukuku
4. Kuna waimbo fulani siukumbuki jina ila ulikuwa unasema kwamba, "manahodha wa mashua kwa nini muwe nyuma, chombo kikienda mrama nani alaumiwe"?
5. Njiwa (Patricia Hilal)
6. Asu (Abdul Misambano.....my favourite song)!!
7.
Waimbaji mahiri: Najua wako wengi ila naweza kuwakumbuka baadhi tu....
1. Shakila
2. Issa Matona
3. Khadija Kopa
4. Nasma Khamis
5. Mzee Yusufu
6.......
Hata hivyo baadhi ya nukuu ambazo nimekutana nazo hivi karibuni ni kama hizi,
"Ukiona nanga inatupwa kwenye maji, ujue jahazi limefika. Ndimu changa haina maji na bamia ikikomaa sana inapoteza thamani"....by Khadija Mohamedi!!!
Naomba michango yenu wandau kwani naanza kuvutiwa zaidi na kutamani kuufahamu zaidi huu muziki!!
Kasikilize "TX Nipasue"
Mimi najiuliza jinsi 'gay culture' ilivyo popular na muziki wa taarabu
na jnsi vikundi hivyo vinavyo shirikisha wanasiasa
na sasa wanakuja juu walipoambiwa na david cameroon 'waheshimu haki za gays'
isnt it funny??????
Kweli mkuu???
Naomba usinifanye niwaombe wahusika wanifungie hii thread!
kuna wimbo kaimba Issa Matona kuhusu nyuki, sijui unaitwajwe lakini maneno yake yanauliza uhalali wa asali kwa sababu hata kwenye mzoga wa nyani, nyuki hupata material za kutengeneza asali...unaitwaje huu wimbo?
hata mashairi yao tu ni utata...
na all the gays in dar 'wanajaa' kwenye taarabu tu..
But usiombe waifunge thread. taarab is bigger than that....hiko ni kisehemu tu..
so sisemi taarabu ni gay music no..
taarab ni music na culture kubwa tu....na marijali ni wengi kuliko hao gays...
Dah! Nimeusikiliza huu wimbo wote na kumkumbuka Mzee Issa Matona jinsi alivyokuwa na kipaji cha kuzichangamsha harusi mbali mbali alizoalikwa kutumbuiza. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi~AMEN.
Bahati mbaya hii miziki haipo kwenye you tube...Ngoja wadau waje watusaidie,
Ila ukweli utabaki pale pale kwamba huyu babu alikuwa ni jabali la muziki wa Taarabu,
Karibu sana Teacher,
Nilishaanza kusikitika kwamba Muziki ambao unaonekana kuwa wetu kwa kila kitu hauna wadau!
Nitasikiliza kwa makini choice yako!! Nikikutana na mistari migumu nitakuja kuomba msaada, ....sawa teacher!!
Babu DC
Hapo sasa,
Hivi taarabu huwa inagusa theme moja tu....???
Karibu sana B!!
Wadau tupo tulikuwa mbali tu
"utakuna kutwa kichwa, kwa ndole na visigino
nazi haitoki chicha, japo bingwa wa mikuno..."
Bee aseme kama tumtafsirie hiyo part ...lolz