mcmzungu
Member
- Jul 11, 2015
- 48
- 65
Nakumbuka kipindi hicho muziki wa dansi ulipokuwa muziki Twanga wakitamba na nyimbo 'jirani' utunzi wa Ally Choki, TOT Band na wimbo 'Masimango' utunzi wa Waziri Sonyo, African revolution na 'Tunda special' utunzi wa Muumuni Mwinjuma, FM academia 'Dunia Kigeugeu' na Stono Musica wimbo 'Binadamu' utunzi wa marehemu Ndanda Kosovo ilikuwa ni Raja.
Nakumbuka Muumini Mwinjuma alikuwa anarap 'Wazimu Wangu Ukinipanda hata nguo Nitavua' na kweli mashabiki walikuwa wanavua kutokana uhondo wa muziki wa dansi. Au Ally Chocky alipoingia ukumbini na Farasi mpaka kuitwa 'Mzee wa Farasi'. Nakumbuka vijembe kati ya Ally Chocky, Banza,Muumin au Ndanda Kosovo na Totoo ze Bingwa ilikuwa ni burudani sana.
Najiuliza kwanini muziki wetu wa dansi la kizazi kipya limechuja wakati Ally Choki, Muumin, Totoo ze Bingwa, Badi Bakule, Lwiza Mbutu, Kalala Junior, Ferguson, Nyoshi el Sadaat, Patcho Mwamba, Mule mule FBI, Charles Baba, Chokoraa bado mpo mmeacha mzigo wote kwa Christian Bella ambacho ilibidi Mgawane riziki .
Mbaya zaidi hakuna Mwanamuziki wa dansi Mtanzania hata mmoja anayekimbizana na wasanii wa bongo flavour. Unaweza kusema tatizo ni Promo lakini zipo njia nyingi mno kuwafikia Mashabiki kama magazeti, TV, Youtube, Instagram, Blogs nk.
Tunaomba sana Mturudishie muziki Wetu kama zamani ulizeni hata bongo flavour Wanatumia mbinu gani.Nawatakia heri na fanaka Wasanii wa dansi katika mwaka huu mpya na Natamani ujumbe uwafikie popote walipo.Nakaribisha maoni ya Wadau mbalimbali.