Wasanii wa zamani wa muziki wa band wanafaidika na chochote kutoka kwa watumbuizaji wa nyimbo zao kwenye hizi bar kubwa?

Vocal Fremitus

JF-Expert Member
Oct 20, 2016
1,187
5,996
Habari za muda huu ndugu zangu. Niende moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu. Miaka ya hivi karibuni kumeibuka mtindo wa hizi bar kubwa kubwa za mitaani kualika wasanii kutumbuiza kwa kuiga nyimbo za band za zamani.

Juzi nimeshuhudia band ikitumbuiza nyimbo kadhaa za Mwinjuma Muumini, Ally Choki, Msondo Ngoma, Waziri Sonyo, marehem Banza Stone n.k. katika moja ya bar kubwa na maarufu hapa mjini.

Nimeona wana vyombo vizuri vya kisasa, wapiga drumz na matarumbeta pamoja na waimbaji ambao wanafata ala na sauti za nyimbo zile za zamani. Kwakweli wanatupa burudani sana sisi wahenga wala sina baya nao kwani na wao wapo katika kutafuta mkate wao wa kila siku.

Nimejikuta napatwa na maswali mengi kichwani mwangu yasiyo na majibu. Je, wasanii halisi wenye hizo nyimbo wananufaika na chochote kupitia kazi zao kuimbwa na live bands? Na kama hawanufaiki, je ni busara kwa mtu yoyote kupanda jukwaani na kutumbuiza nyimbo zao bila ridhaa yao? Vipi wadau wa haki miliki za wasanii wetu wameliona hilo? Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom