SoC02 Muziki, Uchumi na Maisha

Stories of Change - 2022 Competition

Dr Yesaaya

Member
Jul 25, 2022
9
23
Muziki, Uchumi na Maisha

Mwandishi: Dr Yassayah – (Daktari wa binadamu, mtunzi na mwimbaji wa muziki tangu 2007)

Muziki ni jambo zuri katika jamii. Muziki umeumba jamii zetu na tamaduni zetu tangu vizazi na vizazi. Katika maisha yetu ya kila siku muziki husaidia kuibusha hisia, mitazamo na kuchochea mageuzi na mabadiliko. Muziki ni maisha, muziki ni uchumi. Muziki ni kazi. Muziki ni burudani.

Nassib Abdul Juma Issack (alizaliwa tandale 02/10/1989) maarufu kama diamond platnumz, ni msanii, mwanamuziki, mtumbuizaji bora wa muda wote hapa nchini Tanzania. Vilevile ni mfanyabiashara. Nassib anamiliki ni CEO wa makampuni wasafimedia (tv and radio) wasafi bet, WCB Wasafi record label. Ni msanii wa kwanza afrika nzima kufikisha watazamaji bilioni 1 katika youtube(Hizo ni pesa nyingi mno). Alianza muziki 2009 hadi sasa bado yumo. Ni balozi wa makampuni mengi sana yanayomuingizia pesa lundo kupitia muziki wake. Alianza muziki mwaka 2006 akiwa na miaka 17 akiwa anauza mitumba, wimbo wake wa mwanzo uliitwa “toka mwanzo” haukufanya vizuri hadi alipotoa “nenda kamwambie”mwaka 2010 ndio ukamtoa. Aliwahi kuchukuwa cheni na kidani cha mama yake akauza ili kupata pesa za kurekodi. Amepambana sana hadi kufikia mafanio yake

Lengo la hadithi ya Diamond Platnumz ni ili kuongea na kijana mwenzangu, msanii mchanga kwenye muziki.

Fursa zipo tele katika muziki


MAMBO MUHIMU ILI KUJIENDELEZA KICHUMI KUPITIA MUZIKI

1. Wingi kwanza kabla ya ubora.

Ed sheeran alisema “run the tap ‘til the dirty water runs clean” hiyo humaanisha unatakiwa kuwa na matoleo mengi ya muziki kabla hujatoa kazi bora. Yaan usiishie kazi moja ilipogonga mwamba ukakata tamaa, pambana utoe zingine mpya Zaidi. Malcom gladwel alisema “10,00 hour rule inayosema it takes 10,000hrs to practice to become an expert at something” yaan itakubidi kufanyia mazoezi mara elfu kumi ili uwe mbabe au bingwa katika eneo husika au jambo Fulani. Hakuna njia ya mkato katika mafanikio. Sio katika muziki pekee hata katika biashara, kilimo n.k

Fanya muziki au wimbo mmoja kwa haraka na kuumaliza ili ufanye wimbo au kazi mpya na sio kutumia miezi 6 katika kazi moja itakuchelewesha. Unapofanya nyingi inaongeza wigo wako w kufikiria nakujipa mazoezi ya kubuni vitu vipya vikali Zaidi. Nyimbo 5 ukiandika inamaana una mistari Zaidi ya hamsin na beats Zaidi ya tano na melody nyingi umetengeneza. Niamini mimi Utasonga mbele.


2. Tengeneza muziki unaoupenda wewe sio muziki unaohisi watu wengine wanapenda(trend).​

Ni rahisi sana kuanguka iwapo utafanya haraka kutafuta umaarufu au kutambaa na trendi bila kufuata kile moyo wako unapenda. Ukifanya muziki wako kwanza ni win win situation. Iwapo wengi hawatoupenda, ni kweli utaumia lakini wewe umeupenda hivyo wimbo huo utaburudisha moyo wako na utakupa faraja maana ni hisia yako na pendekezo lako. Ukifuata upepo wakati wewe hujapenda staili au aina hio ya muziki, na kwa bahati mbaya raia hawajaupenda vilevile kwanza utaumia Zaidi na wewe hutaburudishwa na wimbo huo. Maumivu na machungu maradufu. Tambua muziki ni endelevu na inakula muda hebu fanya muziki huku wewe pia unaburudika na kufurahia muziki wako. Pia kumbuka muziki unaotrend ni ubunifu wa mtu amebuni kitu chake cha tofauti ndio maana imebamba, wewe pia una kipaji buni chako.


3. Komaa na upambane (consistency)
Muziki ni mchezo wa kukomaa na kupambania kombe. Diamond platnumz alikomaa Zaidi ya miaka sita hadi kuona mwanga katika muziki wake. Kama wewe msanii mchanga na umetoa ngoma kadhaa mwaka jana kisha mwaka huu unakuwa kimya unapoteza momentum na ubora wako kimashairi na melodi/ala za muziki unadumaa. Pamoja na kushiriki mashindano na matamasha mbalimbali ya muziki, Jipangie kila mwaka unatoa ngoma angalau 3 za muziki. Tafuta pesa mahala pengine, ndugu zako wa karibu ,wadhamini na mameneja wakupige jeki kutimiza ndoto zako.


4. Weka malengo (set goals) halafu iwekee mikakati na mifumo(build systems)

Mimi pia ni muhanga wa kuweka malengo mengi isiotekelezwa kama ilivyo pia kwa wengi wetu. Bila shaka kuweka malengo na mipango mingi bila kuiwekea mikakati na jinsi gan kuitimiza itashia kuumiza moyo wako pale utapotazama malengo yako (goals) halafu huajitimiza. La kwanza, tabia njema (good habits) zitakuwezesha ufikie malengo. Tabia njema hutengenezwa na mifumo inayosapoti hizo tabia. Mfano. Lengo ni nyimbo 3 kwa mwaka. Tabia ni kutafuta pesa na kuwa na nidhamu ya matumizi ili upate hela uingie studio. Mfumo ni kuhakikisha kila mwezi umeingia studio na umetoa ngoma moja na ndani ya miez miatatu umeisambaza katika mitandao au vyombo vy habari. Laima utasogea.


5. Tumia muda wako kubuni vya kwako na sio kuiga (kukopi na kupaste)
Wakati mwingine ni kweli muziki wa walikutangulia inakuvutia na inakushawishi lakin kuiga kuimba kama wao haitokusaidia. Jifunze harakati zao ila usifanye kila kitu kama wao. Kuwa wa tofauti kiusanii hata kimavazi.


6. Tumia mtaji wa mitandao ya kijamii (followers)

Hao ndio mashabiki zako wa kwanza, watanunua muziki wako. Hakikishe wamesubscribe katika akaount zako youtube, sportfy, boomplay, na platform zote za muziki


7. Shirikiana na jamii ya muziki
Jenga urafiki na wasanii wakubwa, watayarishaji wakubwa, watangazaji wakubwa, madj wakubwa, mameneja wa wasanii waliofanikiwa usiogope kuwafuata na kuwasikilizisha kazi zako hujui ni lini kazi yako itakubalika. Muziki ni mbegu inaweza kuchipua wakati wowote mahali popote iwapo itamwagiliwa maji.


8. Jiamini (be bold!)

Kamwe usikubali hofu na uoga ukutawale na kuzuia usiziendee ndoto zako. Hofu ya kukataliwa, kukosolewa au kuambiwa hujui ama huwezi. Usisahau hormoniza alikataliwa pale BSS na aliambiwa hajui kabsa kuimba, leo yuko wapi?

- Kuna aina tatu(3) za kukosolewa (criticism)
  • Kukosolewa ili kujenga(constructive): hii ni nzuri na itakusaidia kukua. Sikiliza halafu Chukuwa maoni yao yafanyie kazi.
  • Kukosolewa ili kukupoteza(misleading): ukimuuliza mpenzi wa muziki wa taarabu kuhusu wimbo wako wa boring au bongofleva ni wazi atakwambia wimbo mbayaaa. Vivyohivyo kwa regen a muziki mwingine. Sikuzote tafuta ushauri kwa watu sahihi. Bongofleva mpelekee B12 akusahauri na sio Dida Shaaibu au Ally choki (japo hio ni mifano tu wapo watu wanajua kila aina ya muziki.
  • Kukosoa kwa kuharibu(destructive): tegemea hili kwa watu wenye chuki. Maoni yao yatakuumiza na kukuvunja moyo. Wafute na uwa-block kisha songa mbele. Maranyingi hawa ni watu wasiokujua wewe vizuri, halafu wengi wao wana chuki na kijicho na wivu. Hawapendi maendeleo yako, wengi wao maisha yao binafsi yanawachanganya wana stress na wameshashindwa maisha. Ukiwasikiliza hao huwez kufanikisha chochote katika muziki wako.
9. Jifurahishe na ujiburudishe mwenyewe – utang”ara kuptia muziki wako na kipaji chako

Huu ni ufunguo. Kumbuka unapoanza muziki ni safari ndefu na umeipenda mwenyewe wala haujalazimishwa. Furahi na ujiambie kuwa unaweza kuifanya na utatoboa hata kama sio leo basi kesho. Feel the love baby- life is too short not to enjoy( jisikie upendo, maisha ni mafupi sana kwann usifurahie unachofanya?)


10. Jitazame, jiangalie na kujitafuta mwenyewe

Ni muhim kuwa na afya bora, buheri kabisa ili kufanya muziki mzuri usiandike mashairi ukiwa umechoka au una mawazo na misongo. Usiandike au kufanya mazoezi ya muziki kwa muda mrefu au kushinda studio asubuh hadi usiku bila kupata usingizi wa kutosha au kupumzisha akili. Ukifanya hivyo utakosa utunzi bora wa mistari na melodies

Nakutakia harakati njema za muziki. Wewe ni supastaa kesho. Tukutane kileleni. Kilele cha mafanikio.
King Yassayah
 

Attachments

  • Muziki.docx
    17.4 KB · Views: 5
Back
Top Bottom