Muziki kabla ya kikao cha Butiama

Status
Not open for further replies.

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,988
Nasikia wamerekodi CD yenye nyimbo tatu.. itachezwa Ijumaa asubuhi..ili wajumbe waweze kuburudika nayo huko Butiama. Na miye nimekaa mkao wa kula!
 
Nasikia wamerekodi CD yenye nyimbo tatu.. itachezwa Ijumaa asubuhi..ili wajumbe waweze kuburudika nayo huko Butiama. Na miye nimekaa mkao wa kula!

MC atakuwa nani ktk mziki huo?


sasa hizo ni nyimbo za taarab, au za jadi au za kuazima ulaya za kina bob lazima uwe umepata kichwani?

tupashe mkuu wa kijijini
 
Let me guess, CD ya kwanza "Bye Bye EL", ya pili "Funga Virago Karamagi", na ya tatu "Why Rostam why?"
Anyway I am not holding my breath
 
Aaaaaaaaaah, Mwana vipi tena, mambo ya nusu nusu si mazuri mtu wangu anza kukata ishu si unajua tena JF lazima tuwe wa kwanza kujua, bila hivyo itakuwa noma. Leta ishu tuanze kukomaa nao hao mafisadi. Baada ya kuharibu saaaana wanaleta unafiki wa kufanyia kikao chao kwa Nyerere, watakoma. Huko kaburini mzee kakasirika waangalie sana wasije kupigwa na radi kwa laana waliyo nayo hawa. Shame on them. Washauza nchi halafu wanaleta usanii, yaani wanaenda kumthibitishia mzee kwamba tushaharibu. Ole wao. sh.... kabisa
 
Nasikia wamerekodi CD yenye nyimbo tatu.. itachezwa Ijumaa asubuhi..ili wajumbe waweze kuburudika nayo huko Butiama. Na miye nimekaa mkao wa kula!

Naamini this time producer kashamaliza kazi yake ni suala la namna ya kurelease tu.

Nasikia Karibu wazee ya EPA ni kibao kitakachotikisa, Ikifuatiwa na Kamua, kamua shimoni na mwisho Ukame njoo tukamue a.k.a Roast kama monduli
 
Nasikia wamerekodi CD yenye nyimbo tatu.. itachezwa Ijumaa asubuhi..ili wajumbe waweze kuburudika nayo huko Butiama. Na miye nimekaa mkao wa kula!
KWa CCM Ipi??Ya Kina Makamba na chiligati??Hakuna jipya zaidi ya kwenda kurudisha Heshima na Nidhamu ya chama ambayo ilikuwa imepotea.na Ushauri walipewa na Mzee Mkapa,la sivyo wajue Chama Kitawashinda.

Nidhamu iliaanza kurudi pale Kina Mkuchika kuingizwa katika Serikali ,Pamoja Na Mizengo Kayanda pinda!

Ina Maana CHADEMA Mnasubiri CCM inapoishia na Nyie Muanzie??Tayari wameshamnyakkua Mwenyekiti wenu wa Chadema Musoma..

'NAHISI HAKUNA WAPINZANI NA KUNA WATUKINZANI', GEmBe
 
Mzee Mwanakjj,tunakutegemea kutuhabarisha juu ya nyimbo zitakazotumika huko Butiama,lakini sitegemei kupata kitu kipya kwa sababu wanaosoza mtumbwi ni walewale.Hawa ni warabu wa PEMBA.
 
Mmkjj,
Unajua hata mimi mwanzoni sikukuelewa,nilidhani unamaanisha alichokiimba Dr.Lemmy kwamba;
Hata katika sherehe za serekali
mbele ya mwenyekiti kuhutubia
ni mziki unaanza kuwakusanya watu
mziki asili yake wapieeee


Nilijiwa pia na mawazo kwamba labda wataibuka na nyimbo zinazoshangilia kudhibitiwa kwa mafisadi, mfano wa ule wimbo wa enzi za Sokoine v/s wahujumu;
Bomu limeisha pasuka
wahujumu wanatangatanga
milanguzi nayo imo ndanieee


Nimefikiria pia kile ambacho Mpoto na mwenzake wanakiimba katika salamu kwa mjomba, kwamba;
Rushwa ni wimbo wa sumu
ulioenea katika ubongo
wa kila mwana Taifa hili
tuondolee wimbo huu tafadhali
turejeshee nyimbo zetu za makuzi
Vibwayaaa...[/
I]

Mawazo mengine yalinituma kwamba sasa wazee wazima wameamua kutumia hazina waliyonayo na kuthibitisha ujuzi hauzeeki, maana nasikia mzee Makamba kilichomwibua hadi kufika alipo leo ni uongozi mahili wa kwaya. Hapo ongeza Mhe. Kolimba and ze TOT;
Tieni tieni
kwa moyo mmoja
nambari wani eeeh


Aidha kidogo niitimishe kwamba huenda mziki huo ukawa kama alichokisema Luck Dube R.I.P kwamba
But the music they played
was not good
for the Rastaman,yeah
was not good for the real jah man
I'm going back to my roots


ops,kumbe unamaanisha nyeti ambazo bila shaka soon utatushirikisha,fanya hima tafadhali.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom